Kumbe kua na Kiongozi aliyeandaliwa ni vizuri zaidi kuliko kiongozi anayejaribu uongozi kama bahati.

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Wakubwa nadhani mtanielewa juu ya hili!

Nakumbuka enzi za Mwalimu viongozi wa vyama na serikali walikua wanasndaliwa tangu hata walipokua shuleni wakiwa wadogo kabisa, hii iliwapelekea kujua majukumu yao hata kabla ya kuanza kuihudumia jamii kwa sababu walishaufamu wajibu wao mapema, na pia ilisaidia sana kupata viongozi wazuri,waadilifu na wenye umakini dhabiti katika kufanya maamuzi.

Tumeshindwa kuelewa kua kuna tofauti kubwa kati ya kiongozi mtendaji na kiongozi mtawala! Ndio maana tunakurupukia maamuzi bila kufahamu ama kutathmini madhara yake hapo baadaye. Kiongozi mtendaji hulala usiku na kuamka asubuhi na mawazo ya nini atende ili afanikishe mipango yake! Lakini kiongozi mtawala hupanga mipango yake mapema kwa kupima madhara na faida ya maamuzi yake kabla ya kulala usiku na anapoamka asubuhi ni kuyafanyia kazi maamuzi ya jana.

Tukubaliane kua uongozi ni kipaji na sio hisia wala jaribio.
 
Tanzania imegeuka taifa la walalamishi. Hatuelewi hata tunataka nini. Hovyo kabisa
 
Watanzania tuna bahati mbaya sana ya kutopata viongozi wenye vipaji vya uongozi na walioandaliwa vizuri. Angalia kuanzia mkuu wa nchi mpaka mawaziri wote ni hovyo. Hawajui wafanye nini kwa maslahi ya wananchi. Wanachofanya ni kuwaumiza wananchi waliowachagua. Waliwadanganya kwa maneno/ahadi tamu tamu na sasa wamewageuka. Wananchi wanaambulia majuto.
 
Mpiga pushap inchi ishaanza kumshinda hivyo Namuona rais wa watanzania mh ngoyai akiwa ikulu
 
Kuwa kiongozi mwongozaji ni kipaji toka kwa Mola ila kuwa kiongozi nyapala, dikteta, mkurupukaji au mpenda sifa binafsi hiyo no nafasi ya kidunia tuu na unaweza kuipata hata kwa kura za wizi
 
Back
Top Bottom