Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,470
Dakika chache zilizopita nikisikiliza kipindi cha michezo Radio One, nimesikia kituko cha mwaka. Ndani ya ardhi ya Zanzibar, mchezo wa Kick Boxing ni marufuku.
Waziri wa michezo wa Zanzibar amemjibu mjumbe wa Baraza la Wawakilishi aliyetaka kujua ni lini sheria ya kupiga marufuku mchezo wa Kick Boxing itaondolewa na Zanzibar iruhusiwe kushiriki mchezo huo hatimaye kuipa Zanzibar jina katika ramani ya mchezo huo duniani.
Waziri amejibu kuwa sheria hiyo haitaondolewa kamwe, ili kumuenzi Hayati Karume aliyepiga marufuku michezo ya ngumi zenye muelekeo huo. Pamoja na hilo, waziri pia amesisitiza kuwa mashindano ya Tusker Challenge Cup hayatafanyika Zanzibar kwa kuwa yana udhamini wa POMBE.
Maswali yangu:
1. Tunaacha kufanya michezo itakayotoa ajira kwa ajili ya kumuenzi mtu?
2. Kuna nchi ambayo TENDE na HALUA ziliwahi kudhamini mashindano mpk Zanzibar ikatae pombe?
3. Zanzibar haipokei misaada toka nje? Kama inapokea, hawajui kuwa kuna kodi za mivinyo katika hizo fedha wanazopokea?