Kumbe Jarida La The Economist Sometimes Linaweza Kuandika Jambo Jema Kuhusu Tanzania!, Laisifu Ifakara Health Institute kwa Utafiti wa Malaria Afrika.

Hawa jamaa wa ifakara tafiti zao hatuzioni saiti zikisaidia binadamu,ila wako vizuri
IHI wanafanya kazi kwa ushirikiano na wizara ya afya! Matokea ya tafiti zao hufanyiwa Kazi na WIZARA, japo sio lazima sisi tuambiwe kuwa mradi x wa wizara ya afya ni matokeo ya tafiti za IHI!
 
Mayalla nimeyaelewa sana maandishi yako hasa hasa paragraph ya kwanza.

Hilo jarida linaendelea kuandika kazi nzuri za mabeberu wenzao, shirika la ifakara health institute lilianzishwa na mmbeberu wa kiswizi miaka ya kabula hatujapata uhuru wilayani ifakara. Kuna stori nzuri sana juu ya kuanzishwa shirika hili.
Mpaka sasa mfadhili mkuu wa shirika hili ni mbeberu uswizi akifuatiwa na mabeberu wengine. Kazi zao ni nzuri sana na tunamatumaini chanjo ya maralia soon itakuwa tayari maana kuna jamaa yangu miaka ya nyuma walimchukua kwa ajiri ya majaribio ya chanjo yao na imefanya vizuri. Tangu wamuwekee chanjo jamaa hajawahi uugua malaria
Wanabodi,

Mimi ni subscriber wa hili jarida linalotoka weekly, siku zote likiandika chochote kuhusu Tanzania, huwa linaandika only the negatives tuu ya nchi yetu, rais wetu na serikali yetu, hivyo mimi kama Mtanzania Mzalendo, kiukweli nakereka. Mfano rais Magufuli na serikali yake wanafanya makubwa, licha ya utajiri mkubwa wa madini na maliasili wa nchi yetu, na umasikini uliotopea wa wananchi wetu, na makusanyo yetu yote ya ndani, hayatoshi hata kukidhi mahitaji yetu ya kibajeti hali inayoifanya bajeti yetu siku zote kuwa ni bajeti tegemezi kwa wahisani, misaada na mikopo, lakini rais Magufuli kwa utashi wake, tena bila fedha hizo kuidhinishwa na Bunge, kwa ushujaa mkubwa aliamua kununua ndege kwa cash money kutoka fedha zetu za ndani, na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu barani Afrika kumiliki ndege kubwa ya kifahari ya dreamliner, na labda Tanzania ndio nchi ya kwanza duniani kununua ndege kubwa kwa cash money, haya ni maendeleo makubwa ambayo jarida la the economist walipaswa kuyaona na kuyaangazia,kuhusu uchumi wa Tanzania, utajiri wa Tanzania, umasikini wa watu wetu maamuzi ya kishujaa ya viongozi wetu katika kugharimia miradi mikubwa ya kimaendeleo, ambapo japo wananchi wa hali ya chini wanazidi kupigika, lakini in a long run faida wataiona.

Rais Magufuli amefanya utashi mkubwa wa kisiasa kutekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, Mradi wa umeme wa Stigler Gorje, miradi mikubwa ya miundombinu ya mabarabara na madaraja zikiwemo barabara za juu kwa juu, ni maendeleo makubwa ambayo the economist walipaswa kuyaona na kuyaangazia lakini wapi, wao kila siku ni negatives tuu na negativity.

Leo kwa mara ya kwanza, nimeshuhudia jarida hili la the economist likizungumzia kitu positive kuhusu Tanzania
Combating tropical disease Scanning mosquitoes with infrared light could help to control malaria
Their spectra are full of valuable information

Print edition | Science and technology
Dec 18th 2018

This article appeared in the Science and technology section of the print edition under the headline"Learning the lines"

Kumbe hawa jamaa wanaweza kuandika something positive kuhusu Tanzania, kwa nini haindiki mazuri yetu, kila siku ni mabaya tuu.

Pascal
Rejea
Haya ni baadhi ya makorokocho ya The Economist kuhusu Tanzania.
 
Yawezekana tatizo likawa ni wewe na siyo The Economist. Kwa sababu wewe unataka waandike mambo mazuri tu, na huenda mengi ni ya kawaida, wakiandika mabaya, badala ya kuona uhalisia wa kilichoandikwa, kwa sababu ya biasedness ya akili yako, unaona wanaandika wasiyostahili kuandika.

Kujenga intetchange au daraja, ni jambo la ajabu? Miaka minne iliyopita nilienda Bamako na kukaa kwa muda nchini Mali, nilistaajabu sana kuona flyovers 3, na nyingine mpya 1 zlilikuwa ikijengwa. Kulikuwa na viwanja vizuri vya mpura wa miguu pembeni ya barabara vya ukubwa tofauti tofauti, mimi nilishangaa kwa sababu Tanzania hakuna. Wenyeji wa pale, hakuna hata aliyekuwa akiongelea hizo flyovers au vile viwanja vya mpira au mpangilio mzuri wa mji, na wala viongozi sikuwasikia wakiongelea. Nadhani ni kwa sababu waliona ni jambo la kawaida.

Hivi daraja la pale TAZARA na interchange ya pale Ubungo, ni kitu cha ajabu Duniani, kiasi kwamba ushangae kwa nini Economist hawakuandika? Nadhani cha kuishangaza Dunia, ni pale ukimsikia Rais anasema:
1) Sitapokea ushauri wa mtu (Dunia inatarajia kiongozi awe msikivu na apokee ushauri)
2) Nitawafanya watu waishi kama mashetani (Dunia inatarajia kiongozi awafanye watu wake waishi vizuri)

3) Watoto wa kike waliopata mimba ndiyo mwisho wao, hakuna kusoma (Dunia inatarajia jukumu la msingi la serikali ni kuwapa nafasi raia wake kujieleimisha)

4) Polisi akiua mtuhumiwa, asishtakiwe bali apandishwe cheo (Dunia inatarajia Rais asisitize umuhimu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama kufanya kazi kwa kuzingatia sheria)

5) Ole wake atajayeandamana (Dunia iliyostaarabika inaamini maandamano ya amani yenye ujumbe maalum ni namna ya umma kumfikishia ujumbe kiongozi)

Sasa unapokuwa na kiongozi anayetamka na kusimamia hayo, ni lazima vyombo vya kimataifa viripoti ili kuionesha Dunia kuwa kuna nchi ina kiongozi wa ajabu anayetoa kauli na kusimamia mambo ya ajabu tofauti na vuongozi wote wa Dunia nzima.

Kujenga daraja au barabara, si serikali zote Duniani zinafanya? Je, wewe Pascal unaona kujenga barabara au bwawa la umeme ni habari kwa Dunia? Ni nchi gani ambayo serikali haijengi miundombinu ya barabara, madaraja, maji au umeme? Kwetu hapa nchini inaweza kuwa news lakini siyo UK! Kwani Nipasgmhe, Uhuru, the Gurdian, Jambo leo, Mwananchi, hawakuandika juu ya hayo unayoyataja?
Maandiko yanaweza kubadili kizuri kikawa kibaya, kibaya kikawa kizuri lakini hakiwezi kubadili ukweli.

Nukuu nyingi za kuupindisha ukweli huwa ni "out of context".

Jipime zako.
 
Waandishi mpo biased sana. Nani anasimamia hizo tafiti za Malaria hapo Ifakara Health Institute?

Tunafahamu kutaja jina lililo nyuma ya tafiti hizo ni muhali sana kwenu na inawawia vigumu sana.

Wacheni hizo.

Hongera na pongezi zote za tafiti hizi za malaria zinazoendeshwa IHI zimuendee Dr. Salim Abdallah ambae ni Executive Director wa Ifakara Health Institute.

Na hii siyo tafiti ya kwanza, zipo nyingi mbona hamziandiki mpaka aje The Economist?

Mbona nilisikia dr Salim alishatoka? Manake ni mda sana nakumbuka 2010 niliwahi fanya shughuli moja hapo ofc ya mikocheni FAM akiwa mzee Lugendo.
 
Asilimia kubwa ya waandishi wengi wa habari ni makanjanja wa masuala ya duniani, wao na habari za kimataifa wako tofauti.Paschal hayumo kwenye kundi hilo,
 
Mkuu rais anafanya makubwa lakini yote yameelekezwa kwenye ujenzi na miundo mbinu. Huku mtaani mazungumzo wa hela hakuna kabisa, ajira hakuna, ujambazi unaongezeka.

Hela za kubeba kwenye magari kutokea bandarini, Ile kuwahi happy hour New Africa, Holiday Inn na Southern Sun hazipo tena. Ila inauma kweli. Magufuli anajenga miundo mbinu ili wale watakaoamua kuchalalika wasilale na njaa. Wale wa bandari kavu waendelee kusubiri ila watasubiri sana
 
Waandishi mpo biased sana. Nani anasimamia hizo tafiti za Malaria hapo Ifakara Health Institute?

Tunafahamu kutaja jina lililo nyuma ya tafiti hizo ni muhali sana kwenu na inawawia vigumu sana.

Wacheni hizo.

Hongera na pongezi zote za tafiti hizi za malaria zinazoendeshwa IHI zimuendee Dr. Salim Abdallah ambae ni Executive Director wa Ifakara Health Institute.

Na hii siyo tafiti ya kwanza, zipo nyingi mbona hamziandiki mpaka aje The Economist?
Dr. Salim Abdallah....anafanya hayo yote yeye peke yake?
Maana institution ikitajwa inawaunganisha wote. Sasa Dr. Salim kinachovutia ni hilo jina lake?
 
Wanabodi,

Mimi ni subscriber wa hili jarida linalotoka weekly, siku zote likiandika chochote kuhusu Tanzania, huwa linaandika only the negatives tuu ya nchi yetu, rais wetu na serikali yetu, hivyo mimi kama Mtanzania Mzalendo, kiukweli nakereka. Mfano rais Magufuli na serikali yake wanafanya makubwa, licha ya utajiri mkubwa wa madini na maliasili wa nchi yetu, na umasikini uliotopea wa wananchi wetu, na makusanyo yetu yote ya ndani, hayatoshi hata kukidhi mahitaji yetu ya kibajeti hali inayoifanya bajeti yetu siku zote kuwa ni bajeti tegemezi kwa wahisani, misaada na mikopo, lakini rais Magufuli kwa utashi wake, tena bila fedha hizo kuidhinishwa na Bunge, kwa ushujaa mkubwa aliamua kununua ndege kwa cash money kutoka fedha zetu za ndani, na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu barani Afrika kumiliki ndege kubwa ya kifahari ya dreamliner, na labda Tanzania ndio nchi ya kwanza duniani kununua ndege kubwa kwa cash money, haya ni maendeleo makubwa ambayo jarida la the economist walipaswa kuyaona na kuyaangazia,kuhusu uchumi wa Tanzania, utajiri wa Tanzania, umasikini wa watu wetu maamuzi ya kishujaa ya viongozi wetu katika kugharimia miradi mikubwa ya kimaendeleo, ambapo japo wananchi wa hali ya chini wanazidi kupigika, lakini in a long run faida wataiona.

Rais Magufuli amefanya utashi mkubwa wa kisiasa kutekeleza miradi mikubwa ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, Mradi wa umeme wa Stigler Gorje, miradi mikubwa ya miundombinu ya mabarabara na madaraja zikiwemo barabara za juu kwa juu, ni maendeleo makubwa ambayo the economist walipaswa kuyaona na kuyaangazia lakini wapi, wao kila siku ni negatives tuu na negativity.

Leo kwa mara ya kwanza, nimeshuhudia jarida hili la the economist likizungumzia kitu positive kuhusu Tanzania
Combating tropical disease Scanning mosquitoes with infrared light could help to control malaria
Their spectra are full of valuable information

Print edition | Science and technology
Dec 18th 2018

This article appeared in the Science and technology section of the print edition under the headline"Learning the lines"

Kumbe hawa jamaa wanaweza kuandika something positive kuhusu Tanzania, kwa nini haindiki mazuri yetu, kila siku ni mabaya tuu.

Pascal
Rejea
Haya ni baadhi ya makorokocho ya The Economist kuhusu Tanzania.
Congratulations IHI mmewahi kunihifadhi hapo na Avecnet na MTC projects
 
Sema hivi:LAISIFU IFAKARA
 
Dr. Salim Abdallah....anafanya hayo yote yeye peke yake?
Maana institution ikitajwa inawaunganisha wote. Sasa Dr. Salim kinachovutia ni hilo jina lake?
Yeye alikuwa kinara wa hizo tafiti. Ni kama vile sasa hivi utasikika Magufuli anajenga SGR au ananunua ndege.

Nafahamu kuna vingine kumeza ni vichungu lakini kama ndiyo dawa inabidi ustahamili tu.

Salim Abdulla | IHI
 
Sasa kuna ubaya gani mtu akisifia kizuri na kukosoa kibaya? Ni wa kujali maslahi yao binafsi pekee ,psychophants na (labda baadhi ya watu wa Kanda ya Ziwa) ndio wanaoona kila kinachofanywa na serikali ya awamu ya 5 ni sawa. Ukweli ni kuwa uchumi umedorora, Tanzania si attractive tena kwa wawekezaji, hofu inaanza kutanda kutokana matamshi ya kiwehu ya kiongozi (kama, polisi akiuwa apandishwe cheo!) .
Kama ninayeishi nje, nilichokishuhudia mara kadhaa ninapokuja nyumbani tangu awamu hii ni kuwa Tanzania imeacha kuwa nchi ya furaha na watu kujiamini. Mahali pake imemkubwa na wasi wasi na shida ya maisha (tofauti na mkuu alivyokusudia, labda). Ukija kwa wafanyibiashara, wengi wameamua kusitisha shughuli zao na kungojea kipindi kipite.....
Mtu kama wewe Mayalla ilibidi umwambie ukweli kiongozi na wala usisifie tu, hata kama una maslahi yako binafsi. Nchi inakwenda kubaya.
Ni ukweli kuwa hakuna serikali yeyote duiniani imeweza kufanya kila kitu, na hilo wala siyo jukumu la serikali. Jukumu la serikali ni kuwasimamia raia wajiletee maendeleo. Serikali haiwezi kuwaletea maendeleo watu. Kwanza kimantiki tu maendeleo ni nini. Kwangu maendeleo ni kupata huduma za lazima bila taabu, mwingine ataona maendeleo ni kuwa na ndege na madaraja, lakini kwa mwingine maendeleo ni kuwa na nchi yenye usalama bila kunyanyaswa na polisi.
 
Back
Top Bottom