Kumbe Jairo hakuanza mwaka 2010/2011

Kumbe Jairo hakuanza mwaka 2010/2011

Jamani hili jambo sio tena la kuchunguzwa na CAG,hii lazima tume ya bunge iundwe ili ichunguze mpaka na wabunge wanaohongwa ili kupitishwabujeti
 
Ndugu wanabodi,

Ningeomba sana tujifunze kusoma between the lines kisha kama mbayuwayu tuchanganye na za kwetu..
Maelezo haya hapa yanajieleza vizuri sana toka barua aliyoandika Jairo na kipande hiki ndicho hasa tunatakiwa kukitazama. Kinasema hivi:-

"Gharama hizi kubwa zimesababishwa na kupanda kwa gharama za posho kutoka Sh60,000 mpaka Sh200,000, Sh50,000 hadi Sh150,000 na Sh30,000 hadi Sh100,000 kwa wenyeviti na makatibu, wajumbe na sekretarieti sawia," inaeleza sehemu ya waraka huo uliondikwa na Jairo na kuongeza:

"Kwa kuwa bajeti ya wizara ya 2009/2010 ilikadiriwa kwa viwango vya zamani, ni dhahiri wizara haiwezi kubeba gharama hizi peke yake. Hivyo inashauriwa Wizara igharamie 96,626,000 na wadau muhimu wa wizara wagharamie 90,000,000".

Barua hiyo haifafanui kuhusu wenyeviti, makatibu, wajumbe na sekretarieti ambao wanapaswa kulipwa posho hizo.

Kwa malezo haya pekee kuna maswali yanajitokeza na muhimu zaidi kuyafuatilia.

1. Posho zimepanda mara tatu zaidi ya posho za awali (AWALI)! - Hivyo posho hizi zilikuwepo na kiwango kimeelezwa Je, ni nani aliyepanga posho hizi na kwa kutumia kifungu gani cha sheria?..Bunge na wajumbe wake walitegemea hizi posho zitatoka kifungu gani cha matumizi haya toka wizara hizi..

2. Wanaolipwa ni Wenyeviti, makatibu, wajumbe na sekretariet... Hawa ni kina nani? kwani yaonyesha wazi utamaduni huu haukuanza jana wapo wenyeviti, makatibu , wajumbe na sekretariet waliokuwa wakipokea POSHO hizi kwa kiwango cha zamani cha Tsh 60,000, 50,000 na 30,000.
 
Nashauri wa kusulubiwa si jairo pekee, bali na wengine wote ambao wamekuwa wakihusika na uhuni huu!!!!
 
Nakubaliana na wewe kabisa Mkuu. Ingewezekana kuitisha special audit kwa Wizara zote tungeweza kufahamu mengi na kuokoa Fedha nyingi za Umma zinazopotea kwa hongo mwaka hadi mwaka.
Kinachohitajika sasa wala si uchunguzi maana yote yako wazi.tutana tatizo la kuchukua hatua za dhati.viongozi wenye uchungu na nchi hawawezi kufanya mambo ya hovyo hovyo na kuacha mambo yaende kama nchi haina wenyewe.nilimshangaa sana PM kusema kumwajibisha katibu mkuu ni mpaka rais arudi.rais ni taasisi na wala si JK kama tunavyamnishwa hapa.kuna mtu antenda shughuli za raisi wakati raisi akiwa amesafiri.lingeshughulikwa mapema ili wananchi waone uwajibikaji wa serikali.pale rwanda jambo kama hili lingetokea Jairo angekuwa na wakati mgumu.yeye ndie anapaswa kuthibitisha hana hatia beyond reasonable doubt.
 
Jamani hili jambo sio tena la kuchunguzwa na CAG,hii lazima tume ya bunge iundwe ili ichunguze mpaka na wabunge wanaohongwa ili kupitishwa bajeti
Hapa pana ugumu sana, kwa kiwango kilichokusanywa ni wazi ilikua wabunge wengi wahusishwe, katika hiyo tume ya bunge unayoitaka badala ya CAG, una uhakika gani wajumbe wake hawatakua miongoni mwa waliopewa/waliolengwa kupokea rushwa?Tuchukue mfano mdogo wa naibu spika bwana ndugai,wakati anafungua kikao cha bunge kujadili hii wizara alidai kua walioomba kuchangia walikua wengi hivyo ilibid afanye selection ya hali ya juu kuchagua wale ambao hawakuwahi kuongea, haiwezi kua nae ni mhusika, so may be alikua na list yake ya wahongwaji ili awape nafasi?Kwa nchi inayofuata utawala, Bw. Ndugai na Jairo wangekua ndani muda huu.''Tanzania hakuna amani kabisa, Tunavumiliana tu''
 
Back
Top Bottom