Kumbe huyu Trump ni bonge la comedian

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,281
117,176
Kuna jambo la kushangaza sana kwa viongozi aina ya Trump jinsi wanavyoweza kupata wafuasi wajinga wajinga wengi mno wa kuwapigania na kuwaaminia hata jambo la uongo kabisa.

Juzi imetangazwa kuwa Trump ame sign mswaada wa kuzuia au kuweka ugumu kwa raia wa nchi za kiislam kupata visa ya kuingia USA.

Mijitu yenye akili ndogo naona ilruka ruka mno na kusema huyu jamaa si mchezo hataki masihara.

Sasa zilipotajwa hizo nchi ndo nilicheeka kupita kiaisi eti Somalia, sijui Syria, Iran yaani vichekesho vitupu

Hakuna Saudia Arabia hata Egypt tu hakuna

Kama mtakumbuka Al Qaeda iliundwa na wasaudi Arabia na wa Egypt, zaidi kuliko watu wa nchi zingine, hata Kuwait trump kaiogopa licha ya kuchangia idadi ya kutosha ya terrorists

Huuu ndio ukweli, Trump ni comedian tu anae wachota watu wenye akili ndogo.

Kuna vitu hana ubavu navyo.

Kingine ni aliposema USA kwa miaka mingi imetumia utajiri wake kutajirisha nchi zingine
na kuacha wamarekani masikini, hii alisema siku ile ya kuapishwa

Swali la msingi ni hili? ana ubavu hata wa kupunguza tu misaada kwa Israel?

Naweza ku bet pesa nyingi tu ubavu huo hana. sio ttu wa kusimamisha hata tu kupunguza misaada kwa Israel, tusubiri tuone. kama hata Saudia Arabia tu anaiogopa itakuwa Israel?
 
hadi leo cant believe wa US walimchagua jamaa... hizo nchi alizozitaja ni vichekesho haswaaa

Yaani zinatajwa nchi za kiislam za middle east halafu na Somalia inaingizwa humo...hahahaa
huyu comedian
 
Egypt ina mpango na hawawezi kuwazuia, Iran wana beef na USA kitambo, Syria wana vita mpaka sasa, Somalia unaijua ilivyo ugaidi utashamiri zaidi baada ya muda kidogo tu huko Europe maana kama ni kuzuia waislam tayari wakimbizi wengi wameingia ujerumani kutoka syria Trump sio mjinga kabisa ana akili timamu.
 
Bossman, una uhakika hizo nchi ambazo hazikutajwa haitakuwa vigumu kwa raia wake kupata visa?

Manake kutotajwa tu haimaanishi hazipo kwenye nchi ambazo watu wake watakuwa wanaangaliwa kwa darubini zaidi.

The fact kwamba hazijatajwa ina maana kuwa kuna sababu
na hiyo sababu ndo naizungumzia hapa....usanii....hata kama nazo zitakuwemo....

Tofauti na anavyojitangaza haogopi lolote...
inaonekana kuna 'maslahi' mengine hata yeye anajua 'akigusa' tu kuna hatari zake
 
Hahaha!

Saizi kumeibuka Siasa Mpya za ulimwengu-viongozi wa Siasa hizo wakiziita za kizalendo au Utaifa,huku wakitoa Majibu rahisi,ya mkato na yenye mvuto katika matatizo makubwa na mara nyingi hotuba zao zimekuwa sizakuandika tena imebaki ni kuropoka hovyo-hovyo.!

Na wafaasi wao ambao ni wengi walishajikatia tamaa na wala hawatafakari undani wa hizo kauli zao.

- Hii Century tutaona na kusikia Mengi-
 
Anajua kuna sehemu akiigusa nini kitakachofuata....
Ametoa amri ukuta ujengwe kati ya Mexican na Marekani cha ajabu ghalama za ujenzi walipe Mexico!
Huyu jamaa ni mjanja sana aliejificha kwenye kimvuli cha ujinga...
 
Who are we to judge,Trump kashinda kura solery kwa kusema hayo anayoyafanya sasa hivi, anything else atakuwa ana wa short change Americans-Suala la Israel halihusiki-endapo angesema atawashugulikia Israel na bado akashinda then ingebidi awajibike

Ukisema utazuia raia wa nchi zinazotoa terrorists halafu
kati ya terrorists 19 walio attack USA September 11 2001 ....15 walitoka Saudia Arabia
2 walitoka Egypt.....

halafu uje useme nazuia kutoka Somalia huoni vichekesho?
 
Hahaha!

Saizi kumeibuka Siasa Mpya za ulimwengu-viongozi wa Siasa hizo wakiziita za kizalendo au Utaifa,huku wakitoa Majibu rahisi,ya mkato na yenye mvuto katika matatizo makubwa na mara nyingi hotuba zao zimekuwa sizakuandika tena imebaki ni kuropoka hovyo-hovyo.!

Na wafaasi wao ambao ni wengi walishajikatia tamaa na wala hawatafakari undani wa hizo kauli zao.

- Hii Century tutaona na kusikia Mengi-

Nimesoma sehemu Trump anaanzisha patriotic day huko USA nilicheka saana...
 
Hujui umhimu wa Israel kwa marekani mkuu? Hawezi marekani kumuweka pembeni Israel kwa sababu ni mhimili wa kuitengeneza marekani.
 
The fact kwamba hazijatajwa ina maana kuwa kuna sababu
na hiyo sababu ndo naizungumzia hapa....usanii....hata kama nazo zitakuwemo....

Tofauti na anavyojitangaza haogopi lolote...
inaonekana kuna 'maslahi' mengine hata yeye anajua 'akigusa' tu kuna hatari zake

Hmm...hapo sidhani kama criticism yako ina merit aisee.

Kwani kati ya hizo nchi ambazo hazijatajwa zipi ni state sponsors wa terrorism?

Na ni zipi ambazo si partner wa Marekani katika kukabiliana na huo ughaidi?
 
Ni kama unakubaliana kuwa karibu wasomali wote ni terrorists...
Somalia mfano nchi iko vitani...same na Syria...

Sasa kama nchi hizo ziko vitani...ina maana sanasana zina wakimbizi tu wengi
ukizuia visa sana watakao kuwa affected ni hao wakimbizi ambao pengine wengi sio terrorists...

nchi zinazo produce terrorists kama Saudia Arabia na Egypt hajazigusa....
 
Ukisema utazuia raia wa nchi zinazotoa terrorists halafu
kati ya terrorists 19 walio attack USA September 11 2001 ....15 walitoka Saudia Arabia
2 walitoka Egypt.....

halafu uje useme nazuia kutoka Somalia huoni vichekesho?

Mambo mengi yameshatokea toka 2001. Na inawezekana wale waliokua magaidi wakuu 2001 kwa sasa si tushio kubwa tena.

Na pia inawezekana kwa kipindi hiki Somalia,Syria nk ni tishio zaidi kuliko wale wa Saudi. Pengine wameahapata njia nyingine nzuri ya ku"contain" rogue elements within House of Saudi

Ila niungane ja wewe kuwa jamaa ni mcheshi tu. Jaribio la kwanza ni hapo akikutana na Pena Nieto tuone huo mpango wa kumlipisha gharama za ukuta.
 
Jana Mexico wamesema hawatoi hata centi tano ya huo ukuta...
 
Ni kama unakubaliana kuwa karibu wasomali wote ni terrorists...
Somalia mfano nchi iko vitani...same na Syria...

Somalia kuna stable government?

Serikali ya Syria ni rafiki kwa USA?

Sasa kama nchi hizo ziko vitani...ina maana sanasana zina wakimbizi tu wengi
ukizuia visa sana watakao kuwa affected ni hao wakimbizi ambao pengine wengi sio terrorists...

Hivi kwani hao maghaidi nao hawawezi wakajipenyeza humo kwa wakimbizi ili wapate mwanya wa kuingia kirahisi USA?

Kuna cases ambazo maghaidi walitumia mwanya wa ukimbizi na kwenda hadi Ufaransa, Ubelgiji, na kwingineko.

nchi zinazo produce terrorists kama Saudia Arabia na Egypt hajazigusa....

Nadhani hapa unachanganya mambo.

Ghaidi anaweza akawa anatokea Saudia na Misri lakini akaenda Yemen na kuendesha hayo mambo yake ya kighaidi huko kwa sababu serikali ya Yemen inaruhusu watu wa dizaini hiyo.

Hiyo ni kwa sababu serikali za Saudia na Misri ni kali na zinashirikiana na Marekani. Hivyo inakuwa vigumu kwa maghaidi kujikusanya na kufanya shughuli zao kwenye hizo nchi na ndiyo sababu ya/za wao kwenda huko kwingine ambako wanaruhusiwa kufanya hizo shughuli zao.

Sasa hapo wa kulaumiwa ni nani? Misri na Saudia au Yemen?

Naona umechanganya kati ya country of origin na sehemu ambazo maghaidi wanashamiri.

Hayo ni mambo mawili tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom