Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,587
EROLINK YATOA UFAFANUZI KWA WANANCHI
FRIDAY, FEBRUARY 14 2014, 9 : 27
GAZETI LA MAJIRA
KAMPUNI ya uwakala wa ajira ya Erolink imesema itaendelea kutoa huduma za biashara ya ajira kwa Watanzania zilizo bora na kutoa fursa sawa kwa kila mtu mwenye sifa na vigezo vya kuajiriwa.
Taarifa hiyo imetokana na habari zilizoenea katika vyombo vya habari kuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo ametoroka nchini kukwepa mkono wa serikali kutokana na kampuni hiyo kushindwa kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitatu ya utoaji huduma.
"Tunapenda kutoa wito kwa Watanzania, wafanyakazi wetu na washirika wetu katika biashara kuwa kampuni yetu iko imara na inaendelea kutimiza majukumu yake ya kila siku na itaendelea kutoa huduma zilizobora na kutoa fursa sawa kwa kila mtu mwenye sifa na vigezo vya kuajiriwa," alisema meneja uhusiano wa kampuni hiyo, Larry Makala.
Alisema anayetajwa kuwa mkurugenzi wa kampuni hiyo hana uhusiano wa moja kwa moja katika shughuli za utendaji wa kila siku wa kampuni hiyo kwani ni mmoja tu wa wanahisa katika kampuni hiyo ambaye ahusiki kwa namna yoyote na shughuli za kiutendaji.
"Tunapenda kuwajulisha Watanzania kwamba Bw.Elvis Kamanyile ahusiki moja kwa moja na shughuli za kampuni hii na hana uhusiano wowote katika utendaji au uendeshaji wa kampuni hii, Sisi hatuna taarifa za kutoroka kwake na kuhamisha familia yake nje ya nchi ila tunajua kwamba yupo katika safari zake za kibiashara," alisema Makala .
Meneja huyo alifafanua zaidi kuwa kampuni hiyo haina mpango wa kubadili jina kutokana na kuwa na utendaji bora na kuaminika kwa wadau wote wanaofanya kazi na kampuni hiyo katika biashara.
"Tatizo kubwa ni kwamba kumekuwa na upotoshaji kwa namna ambavyo tunafanyakazi za kila siku, sio kweli kwamba kampuni yetu inakata watu mishahara yao ili kujipatia faida katika biashara zetu, jambo hili ni upotoshaji hauna ukweli wowote bali ni uzushi unaoenezwa katika jamii yetu.
"Suala la uwakala wa ajira ni sehemu mojawapo ya kuendelea kutengeneza fursa kwa Watanzania na kutoa nafasi sawa kwa wote, ajira zinazotolewa na kampuni yetu ni kwa mtu yoyote ambaye anavigezo stahiki,
Tumekuwa tukifanya kazi hii kwa umakini na uaminifu na kutoa fursa sawa kwa watu wote wenye vigezo vya kuajiriwa tumekuwa msaada mkubwa kwa maelfu ya Watanzania katika kupata ajira na ni sehemu ya mafanikio katika kampuni," alisema.
Meneja huyo alisema kwamba wafanyakazi wa kampuni yake pia wanajipatia faida zao za kisheria zikiwemo, NSSF, huduma za hospitali, usafiri na mahitaji mengine kulingana na bajeti ya mteja.
"Tunapenda kutoa wito kwa Watanzania, wafanyakazi wetu na washirika wetu katika biashara kuwa kampuni yetu iko imara na inaendelea kutimiza majukumu yake ya kila siku na itaendelea kutoa huduma zilizobora na kutoa fursa sawa kwa kila mtu mwenye sifa na vigezo vya kuajiriwa," alisema
TANBIHI:NANI MKWELI SASA? EROLINK,WIZARA AU WAFANYAKAZI WANAOAJIRIWA KUPITIA EROLINK?