Morning guys!
SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, kukiri kwamba Uchaguzi Mdogo Jimbo la Buyungu ulikuwa mgumu, mengine mapya yameibuka.
CCM ilishinda uchaguzi huo uliofanyika Jumapili, huku pia ikishinda uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 36, zilizofanya uchaguzi siku hiyo na 41 ambazo madiwani wake walipita bila kupingwa baada ya wapinzani kuenguliwa katika hatua za awali.
Taarifa kutoka Buyungu ambazo gazeti hili limezipata, zinadai kuwa moja ya mbinu walizotumia CCM kuibuka na ushindi ni kuweka ngumu katika kata nne ambazo wapiga kura wengi hawakushiriki kupiga kura mwaka 2015 kwa sababu ya umbali wa makazi yao na vituo vya kura.
Baadhi ya kata hizo ni pamoja na Mtukuza na Nyambibuye zenye wapigakura zaidi ya 8,000.
CCM wanadaiwa waliweka pia nguvu kwenye Kata ya Kiziguzigu, anayotoka aliyekuwa mgombea wao, Christopher Chiza, ambayo kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, walishindwa.
Kwa upande wao, Chadema, waliweka nguvu nyingi katika kata za Gwarama, nyumbani kwa aliyekuwa mgombea wao, Elia Michael, Kasuga ambako ni nyumbani kwa marehemu mwalimu Mwalimu Kasuku Bilago aliyekuwa mbunge, Kasanda na Kakoko mjini.
“Mwaka 2015 walipata kura nyingi kwenye maeneo haya, na mwaka huu waliweka tena nguvu nyingi wakijua kuna kura zao za kutosha, lakini wakasahau kwenye uchaguzi mdogo mwamko wa wapiga kura huwa si mkubwa,” kilisema chanzo chetu.
Source: MTANZANIA.
(Optional)