Kumbe CHADEMA nao wasikitishwa!!

Kumbe CHADEMA nao wasikitishwa!!

Mkuu wewe ni muongo, mchonganishi , mfitini, mnafiki na mzandiki.
Mimi sikuweko huko!!
Hayo maneno aliyoyatunia Kikwete kumshambulia Lissu kwa kusema Lissu ni muongo, mchonganishi , mfitini, mnafiki na mzandiki je Kikwete alikuwepo wakati Lissu anayasema aliyoyasema?
 
Hayo maneno aliyoyatunia Kikwete kumshambulia Lissu kwa kusema Lissu ni muongo, mchonganishi , mfitini, mnafiki na mzandiki je Kikwete alikuwepo wakati Lissu anayasema aliyoyasema?
Ameambiwa!
Hilo tosha.
 
Sasa huoni kwa baba mwenye nyumba kuleta lugha za mitaani nyumbani mbele ya watoto ni kujidhalilisha. Nani kaonekana mmbea, mzandiki? Yule mwenye kusema ukweli au yule mwenye kusikia ya kuambiwa baada ya kurudi toka kutalii, mtu mwenye kuelezwa bila kujua kilichojadiliwa kwa kusoma Hansard? Mtu wa kusubiri kufahamishwa ukiwa wewe ndio mwenye nyumba? Kwa hiyo hakuna alichokumbushwa badala yake Lisu kamjibu vizuri kwa kumpa ukweli kuliko kusuburi kuongea umbea wa kuambiwa, kusikia na kufahamishwa
Hata hivyo rais alimheshimu sana huyu bana mdogo;
Alitakiwa akumbushwe maadili kidogo.
 
Mamndenyi

Ni heshima gani unayozungumzia Raisi kuitoa kwa Tundu Lissu, na unadhani Lissu anahitaji kufundishwa maadili gani ambayo hana hadi hapo alipo.

Ni bahati mbaya kuwa Tanzania kwa sasa tumekubali kuongozwa na viongozi wenye mitizamo na mashindano ya kimakundi hivyo tumejikuta tunapata viongozi wasiojua uongozi wa nchi bali uwezo wa kuongea kimipasho pasipo kujali anaongea ukweli ama uongo. Huwezi kuwa kiongozi wa nchi kama Raisi (Cheo ambacho chenyewe ni Taasisi pana), lakini unapokuja kulihutubia Taifa, kwa jambo la kitaifa unabaki kudeal na mtu as individual na kutumia muda mwingi kumjadili mtu huyo pasipo sababu za msingi. Hicho kwa kwa hakika ni kielelezo tosha cha aina ya viongozi wanaoasisiwa na makundi ya kisiasa kwa kuangalia nani anaweza kuongea sana pasipo kujali anajua nini. Tunapokuwa tunajadili swala la kitaifa tusijitoe akili zetu kwenye ubongo na kuziweka pembeni hadi mwisho wa mjadala, Mwenyezi Mungu ametupa hizo akili na uwezo wa kutafakari mambo ili tuutumie vema.

Any way nilikuwa napita tu.
 
Last edited by a moderator:
Tundu lisu ni MUONGO,MNAFIKI,MFITINI na MZANDIKI kupindukia.
Message sent and received.. Let them choke with it.
Hawa wahuni wa CDM hawana hata aibu na hii ni kwa sababu ya akili za bangi
 
Ni kawaida kwa chadema kulalama pale yanapofika makubwa hili la lisu linawasumbua kila kukicha,
Lisu amezoea kutukana wenzake na kutumia maneno ya kuudhi hata akiwa bungeni,
Lisu pia hajaanza leo huu unafiki wake ni wa siku nyingi ila jk alimvumilia sana kwani daima za mwizi ni arobaini sasa zimetimia kwa lisu kuambiwa ukweli wake kazidi umbea na unafiki.

hivi we ni nani uko ccm... kila kitu unatetea au umelaaniwa nini?????????????????????
 
Alichofanya Rais wetu hakikubaliki.Kama Rais hakutakiwa kuongea namna alivyoongea mwisho wa siku wenye akili zao wataanza kutafiti ukweli na uongo wa kauli za Rais,na pale Rais akionekana amepotoka basi heshima yake itashuka sana.Kama kwenye hotuba ya kambi ya upinzani haikuwa na ukweli kwa nini Rais akasirike na kufyatua maneno ya kejeli kwa mtu binafsi?Kwa ufupi Rais wetu amejidhalilisha mwenyewe pamoja na watendaji wake wanaotakiwa kumshauri vyema.Kwa nini hakuchanganya akili za kuambiwa na za kwake?
 
Cheki unavyohangaika na lisu wako kutwa kumtetea kwa talifa yako lisu ni bidhaa chakavu hanunuliki ni sawa na nyanya mbovu ambayo sokoni haikaa zaidi ya siku moja.

Hivi unafanya kazi wakati gani? Maana siku nzima upo jamiiforums
 
Katumia lugha nyepesi inayoeleweka;
Kuhusu safari unashangaa nini,
huyu rais wenu kafuata nini, hapo tu hana madaraka
siku akiyapata itakuwaje?

Lissu naye ni wale wale tu ...pangu pakavu tia mchuzi.......

Sasa huoni kwa baba mwenye nyumba kuleta lugha za mitaani nyumbani mbele ya watoto ni kujidhalilisha. Nani kaonekana mmbea, mzandiki? Yule mwenye kusema ukweli au yule mwenye kusikia ya kuambiwa baada ya kurudi toka kutalii, mtu mwenye kuelezwa bila kujua kilichojadiliwa kwa kusoma Hansard? Mtu wa kusubiri kufahamishwa ukiwa wewe ndio mwenye nyumba? Kwa hiyo hakuna alichokumbushwa badala yake Lisu kamjibu vizuri kwa kumpa ukweli kuliko kusuburi kuongea umbea wa kuambiwa, kusikia na kufahamishwa
 
Naona hapa kuna tatizo katika kujibu hoja. Nimekuuliza maswali kadhaa umejibu kitu kingine tofauti. Tunasema kuhusu Lisu na JK nani mmbea na nikakuuliza umbea unapatikanaje. Unapatikana kwa kusikia ya kuambiwa, kuelezwa bila kujua bila kushuudia au kupata ushaidi kamili (hapa ni kwa kusoma Hansard), kusubiri kufahamishwa halafu katika hayo ukayafanya unayajua na kuyapigia debe. Huyo ndo mmbea ila msema kweli ni yule alikuwepo kwenye tukio, aliona au kushuudia, alishiriki katika tukio au alikuwa ni mmoja wao waliotenda tukio huyo akikueleza si mmbea wala mnafiki au mzandiki bali amesema kile aliona, alishuudia, alishiriki. Mamndenyi unasemaje hapo bado hujaridhika na jibu? Usiporidhika nitakuchukulia unafanya mdhaa wakati ukweli unaujua. Nieleze hujaridhika??
Katumia lugha nyepesi inayoeleweka;
Kuhusu safari unashangaa nini,
huyu rais wenu kafuata nini, hapo tu hana madaraka
siku akiyapata itakuwaje?

Lissu naye ni wale wale tu ...pangu pakavu tia mchuzi.......
 
Back
Top Bottom