Kumbe CCM waliibiana kura uchaguzi EAC!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe CCM waliibiana kura uchaguzi EAC!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Apr 5, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Kweli mjasiri haachi asili. Nimeipata hii habari kwenye gazeti la Mtanzania. CCM hata wenyewe kwa wenyewe wameibiana kura duh!!!!!

  CCM waibiana kura

  [​IMG][​IMG][​IMG]
  Imeandikwa na Maregesi Paul, Dar es Salaam: Thursday, April 05, 2012 09:44

  UCHAGUZI wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeingia doa. Chanzo chetu cha habari kilichokuwa katika uchaguzi huo, kilisema jana kuwa, uchaguzi huo uliofanyika juzi kwenye Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam, ulijaa kasoro kwa baadhi ya wagombea kuibiwa kura.

  Chanzo hicho kilisema kuwa, mmoja wa wanaodaiwa kuhujumu kura hizo ni aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi huo, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. Nape alikuwa akisaidiana na kada wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.

  Chanzo hicho kilisema kuwa, dalili za kuwapo hujuma katika uchaguzi huo, zilianza baada ya wabunge kukataa kura kuhesabiwa chini ya usimamizi wa meza kuu iliyokuwa ikiongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  “Mimi nilikuwapo ukumbini na niliingia kama mmoja wa mawakala waliokuwa katika chumba cha kuhesabia kura, kwani nilikwenda kumsimamia jamaa yangu ambaye alikuwa anagombea.

  “Kwanza kabisa kabla ya kuingia katika chumba cha kuhesabia kura, kura zilipigwa kama kawaida, zoezi hilo lilipokamilika, ukafika wakati wa kwenda kuhesabu kura.

  “Kabla ya hapo, Kinana alisimama na kutueleza kwamba, kura za wagombea zitasimamiwa na meza kuu, aliposema hivyo, wabunge wakalipuka kwa kusema hatutaki na wengine walidiriki hata kuzomea.
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unashangaa CCM kuibiana kura? Ni sawa na kushangaa kumuona simba serengeti.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  HUJATWAMBIA WALIIBIANAJE! Mkuu hebu kuwa specific, nani kwamwibia nani na nani kaibiwa na nani? hit the point please!
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,132
  Likes Received: 2,154
  Trophy Points: 280
  Habari zingine hazina kichwa wala Miguu
   
Loading...