Kumbe Bombardier ni maumivu kwa Mtanzania kiasi hiki!? Bunge lagundua...

Wewe acha bombadiyaaa zetu ,hata zikileta hasara ya mabilion Hamna shida kwani ni zako,si kodi za wadanganyika ,kuwa na ndege ndio sifa na heshima
 
Mkuu Asante sana kwa hii taarifa..

Akili ya JPM anafikiria tatizo la ATCL ni kuwa na Ndege nyingi..

Tatizo pale ni uendeshaji wa Shirika..

Na kwa akili ya huyu mtu, atachota pesa ovyo Hazina kuipa ATCL ili lisionekane linayumba..

Jamaa ovyo kabisa.
Mkuu ni kawaida kwa miradi mlkubwa inayogharimu fedha nyingi kupata hasara kihasibu mali isiyohamishika,yaani non current assets kila mwaka wa fedha wanakokotoa asilimia fulani kwa ajili uchakavu wake yaani depreciation charge.chukuwa kwa mfano bombadia zimenunuliwa kwa Tshs 220,000,000,000 na asilimia ya uchakavu tuseme 10% kwa hilo kwenye gharama uendeshaji na kutafuta faida hii asilimia 10% inakuwa ni Tshs 22,000,000,000 .
Sasa Tuseme Atc wameuza tijeti za bilioni 20,000,000,000 ukifanya hiyo hesabu ndogo utaona ATC tayari wametengeneza hasara ya Tshs 2,.00,000,000 lakini kwenye kutengeneza hiyo hasara ya 2billion hakuna fedha ya makusanyo ya mauzo iliyotumika,lakini hasara imepatikana.
Kwa kukupa huo mfano nadhani sasa utakuwa umeelewa pamoja na wengine ni swala la utaalamu tu.
Vikiria hiyo reli inayojegwa ikikamilika kwa matrilioni ys shilling kwa mfano wa hapo juu watapata faida mwanzoni mwa mradi?
Ila kwa kadri thamani ya non current assets inavyoshuka thamani ndivyo shirika litakavyo weza kupata faida.
 
Nyie chadema Hanna jema acheni tupige Nazi bana,mtatutoa kwenye reli na hizo porojo zenu,wakati sisi tuko bize na kununua madiwani nyie mnaleta habari ya bomba dear ,acheni tuchape kazi
 
Acha ndege hata biashara ya kukodisha baiskeli ukininua baiskeli mpya kadhaa utaanza na hasara. Acheni chuki zenu za kichama. Magufuli anafanya ya maana. Wakati mihela ilipokuwa inaibiwa kwenye skendo baada skendo hamkutangaza serikali imepata hasara.
 
Hujui chochote kuhusu uwekezaji na faida unayozungumzia. Usikurupuke, uliza wenye taaluma zao. Huwezi kuwekeza leo ukapata faida kesho.
Mi sina taaluma kubwa ya uchumi illa nafikiri una maana uwekezaji lazima upate hasara kwanza halafu faida badae? Naelimishe tafadhali maana nataka kuwekeza kilimo cha mapapai
 
Mambo sio rahisi kama unavyotaka yawe. Mnajaribu kuweka siasa kwenye masuala ya kitaalam.

TCAA na ATCL wamekaguliwa mahesabu yao na yapo safi, hizi fitina zenu huwa zinapotea hewani, hazina mashiko.
Unaelewa unachoongea? Hesabu kuwa safi kuna ubusianao gani na shirika kupata hasara? Hopeless kabisa! Huelewi hata kinachojadiliwa.
 
Wanaozinunua hizi ndege sio wajinga, ni watu wanaoelewa wanafanya nini.

Kilichoiua ATC miaka ya nyuma ni hii tabia ya watu kuingilia masuala ya kitaalam wakati hawayaelewi.

This time JPM ametambua hasara za kuendekeza siasa kwenye masuala ya sekta ya anga, kahakikisha sekta imekabidhiwa kwa wataalam.

Haiwezekani shirika ulifufue leo na kesho uanze kuhesabu faida, hakuna kitu kama hicho duniani kote.
Wewe inawezekana huna hata ABC ya business. Mradi wowote unaoanza kuna uwezekano wa kuanza na hasara lakini kinachotazamwa ni trend. Haiwezekani hasara ikawa inapanda kila mwaka halafu ukaamini unaenda vizuri.

Kumbuka pia ATCL hawajanunua ndege bali wamekodishiwa. Hivyo matumizi makubwa ya ununuzi hayapo katika vitabu vya mahesabu ya ATCL, halafu hasara inazidi kupaa!
 
Acha ndege hata biashara ya kukodisha baiskeli ukininua baiskeli mpya kadhaa utaanza na hasara. Acheni chuki zenu za kichama. Magufuli anafanya ya maana. Wakati mihela ilipokuwa inaibiwa kwenye skendo baada skendo hamkutangaza serikali imepata hasara.
Wanafiki nyie!
 
Wabunge walichfanya inaweza kuwa si sawa. Wameweka mtaji kwenye operating capital ndo maana unaona hasara ni kubwa. Lakini kama wangeweka operating capital peke yake ungeona jinsi ATC inavyoendelea vizuri. Sijajua ni kwa nini wameamua kufanya hivyo wakati wanajua Mataji wa kunua ndege ni pesa nyingi na tumenunua kwa Cash
Wewe ni mwongo. Ununuzi wa ndege haujawekwa kwenye operating costs. Ndege siyo mali ya ATCL. Wao wamekodishiwa. Hasara hii haitokani na ununuzi bali inatokana na operation. Jambo la ajabu gharama inazidi kukua kila mwaka.
 
Mkuu hesabu za ATCL hazitengenezwi na wabunge! Zinatengenezwa nao wenyewe kisha zinaenda kukaguliwa na CAG na kutolewa ripoti.
Na ATCL hawawezi kuweka fedha za ununuzi wa ndege kwani sio zao na hawajui hata bei ya hizo ndege ila ukitaka bei ya hizo ndege nenda kwa Wakala wa ndege za serikali ndio wanajua. Mbona taarifa hii iko wazi kabisa hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa uhasibu anaweza kuelewa!
Umefafanua vizuri sana. Kama bado kuna mjinga hajaelewa hata haya maelezo yako, basi ni wa kumsamehe.

Watu wamekazania kuwa eti ATCL wana hasara kubwa kwa sababu ya ununuzi wa ndege! Sijui ni nani anayewadanganya kuwa ATCL imenunua ndege. Ndege siyo mali ya ATCL. Hasara inayotajwa ni ya kiuendeshaji. Haihusishi ununuzi kwa sababu ndege wamekodishiwa, hawakununua na hawamiliki.
 
Bunge limedhibitisha kwamba ununuzi wa ndege aina ya Bombadier umeliongezea shirika la ndege ATCL hasara maradufu kuliko ilivyokuwa awali.

Tofauti na ripoti ya serikali iliyopotosha kwamba ATCL inajiendesha kwa faida, kamati ya bunge ya uwekezaji mitaji ya umma (PIC) imeeleza kuwa ATCL imebeba mzigo wa hasara kwa asilimia 121% tangu kunuliwa kwa Bombadier.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Albert Ntabaliba amesema mwaka wa fedha 2014/15 (kabla ya kukunua Bombadier) ATCL ilipata hasara ya Shilingi Bilioni 94.3. Mwaka 2015/16 (baada ya kununuliwa Bombadier mbili kwa mbwembwe), ATCL ilipata hasara ya Bilioni 109.3, ikiwa ni ongezeko la Bilioni 15.
Ntabaliba ameongeza kuwa mwaka wa fedha 2016/17 uliomalizika September mwaka jana, (wakati huo Bombadier zikiwa na mwaka mmoja sokoni), ATC ilipata hasara ya Shilingi Bilioni 113.8 za kitanzania.

Kwa maana hiyo ni kwamba ujio wa Bombadier umeongeza matumizi yasiyo ya lazima na kupelekea shirika la ATCL kuendelea kupata hasara mwaka hadi mwaka.

Hata hivyo, viongozi wakuu wa serikali wamekuwa wakinukuliwa mara kwa mara wakieleza kuwa ATCL inajiendesha kwa faida, hadi leo bunge lilipoeleza hali halisi.

Kwa taarifa hii ya bunge inamaanisha kuwa kuna mengi tunadanganywa. Kama ATCL ina hali mbaya kiasi hiki halafu inasifiwa kila kukicha na viongozi, je kuna mangapi tunedanganywa hatujui? Naanza kuwa na mashaka na zile taarifa za BOT za uchumi kukua, au zile za TRA za kuongezeka kwa mapato.

Hasara ya Bilioni 113.8 is not a joke. Ni pesa zinazotosha kulipa madai yote ya watumishi wa umma nchi nzima na chenchi ikabaki. Ni pesa inayotosha kuwapa mikopo wanafunzi wote wa vyuo vikuu. Ni pesa inayotosha kujenga zahanati 1,138 (almost kila kijiji nchini) kwa gharama ya milioni 100 kwa kila zahanati.

Lakini pesa zote hizo zimeteketezwa na ATCL kwa mwaka mmoja tu. Na bahati mbaya viongozi wamekua wakipotosha kwa makusudi kuwa shirika hilo linajiendesha kwa faida huku wakijua ni hasara tupu. Inasikitisha sana. Kama bunge halikufichua aibu hii, tungeendelea kudanganywa kwamba shirika linapata faida kumbe hakuna kitu.

Shirika kujiendesha kwa hasara maana yake serikali inasaidia operating cost maana vinginevyo litakufa. That means serikali imekuwa ikiipa ruzuku ATCL ya Bilioni 100 kila mwaka ili kucompensate hiyo hasara. Maana bila hivyo ATCL ingeshacolapse. Kama ndivyo, je ATCL ilipewa hizo pesa kwa ridhaa ya bunge? Je bunge lilishirikishwa? Au ilifanywa siri kwa kuwa tulishadanganywa linajiendesha kwa faida? Pesa hazionekani mtaani kumbe zimeenda kusaidia kufidia hasara mahali.

Kwanini serikali haikusema ukweli mapema kuwa ujio wa Bombadier umeongezea ATCL mzigo? Hii ingesaidia wataalamu wa uchumi kutoa mawazo yao kusaidia jinsi ya kuikwamua ATCL. Tuna wachumi wabobevu wapo nje ya system kama ZZK, Prof.Tibaijuka etc. Hawa wangeambiwa ukweli tangu mwanzo wangeweza kusaidia.

Lakini serikali imeficha weee hadi leo ilipoumbuliwa na bunge. What a shame? Halafu kuna watu wanasema serikali hii ni ya kizalendo. Uzalendo wa kusababishia nchi hasara na kufanya iwe siri? Uzalendo wa aina hiyo hata shetani hana.!

Historia ni mwalimu mzuri sana asiyesahau kitu
Tatizo watu hawasomi na hawajawahi kufanya biashara.

Hivi walitegemea ATCL ianze kutengeneza faida mara moja??? Wanasahau elimu kidogo tu ya "Product Life Cycle"! Elimu za hawa watu ziangaliwe jamani!

Ndege ni sawa na product na zipo stage one....kasomeni kipiindi kama hichi nini hutokea?

Rais wangu unewashika pabaya ufahamu umewatoka! Hapa kazi tu

Queen Esther
 
Mkuu ili ueleweke vizuri ni vyema ukasema ulipakia ndege mara ya mwisho enzi Nyerere akiwa rais. Hii itasaidia kuonyesha kwamba ulipakia ndege mara ya mwisho enzi za awamu ya kwanza, na baada ya hapo mpaka leo vyuma vyako vimekaza.
teh..teh...teh...we! niko vizuri kuliko Kakobe sema usiseme TRA watakuja bure..kwani hata safari zenyewe ninazo?
 
Tatizo watu hawasomi na hawajawahi kufanya biashara.

Hivi walitegemea ATCL ianze kutengeneza faida mara moja??? Wanasahau elimu kidogo tu ya "Product Life Cycle"! Elimu za hawa watu ziangaliwe jamani!

Ndege ni sawa na product na zipo stage one....kasomeni kipiindi kama hichi nini hutokea?

Rais wangu unewashika pabaya ufahamu umewatoka! Hapa kazi tu

Queen Esther
Hivi shirika limeanza baada ya kukodi Bomberdier? Hebu cheki hizo hesabu jee hiyo hasara ina decrease au ina increase baada ya kila mwaka? Huyo Rais "wako" anakuingiza chaka bibie!
 
Tuonane tarehe 26, nimerudi Tanzania na siondoki hadi tarehe 26 ipite.
 
Jinsi hili swala linavoenda kuna pande kwa maono yangu...na kila pande inaeza kuwa na makosa au faida...tatizo mtizamo wa hawa wanasiasa ndio unaochanganya jamii na nchi in general...swala la uwekezaji lipo la aina nyingi...unaeza invest kwa malengo ya badae au kwa malengo ya muda mfupi...afu ishu ya hasara katika business ipo na hiko kiasi cha upotevu ni kikubwa ....kuna kitu nahisi kinaendelea hapa baina ya pande mbili upinzani na chama tawala...huu ubabe na kuona kila kitu unajua...kutaka maamuzi yote yawe kwako ...kudharau mawazo ya wengne ndio yanayofanya support iwe ndogo ..tatizo mzee hajui kama hii ni nchi...!! Na swala la ununuzi ndege nipo tofauti sana na mheshimiwa kwakuwa sijaona maana ya kupewa kipaumbele kiasi hiko afu kesho unadai rais wa maskini ..how is that
 
Back
Top Bottom