kumaliza biashara ya unga hukumu ya kifo kwa wauzaji na watumiaji

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,465
Ili kuhakikisha biashara ya madawa ya kulevya inapotea Tanzania hukumu iwe ya kifo kwa kunyongwa uwanja wa Taifa saa saba mchana kwa watumiaji, wasambazaji wauzaji na waingizaji na kwa yeyeote atakayekamatwa na madawa ya kulevya. Kusiwe na huruma hata kama ni mtoto au ni kigogo mwenyewe .

Kwa kuuwa wote wanao jihusisha na madawa ya kulevya nchi itakuwa haina tena hili tatizo , hatutakuwa tena na nyumba za sober au kuhitaji dawa za kutibu waathirika wa madawa ya kulevya hauwezi kupoteza fedha za masikini kutibu magonjwa ya kujitakia. Wote wanyongwe watumiaji na wauzaji na wote wanaoingiza bila.

kama haya hayafanyiki mengine yote ni maigizo
 
Balaa la Philippines liachwe huko huko musituletee huku. Isiwe sababu ya kutaka kuua watu bila sababu kama wanavyofanya kule.
 
Mwaka 2015 wakati wa mjadala uliohusu kuifanyia mabadiliko sheria ya kudhibiti na kuzuia matumizi ya madawa ya kulevya,kuna wabunge walikuwa wanapendekeza adhabu ya kifo ila nakumbukwa walipingwa sasa sijui kama kweli tunaweza kuwa na adhabu ya aina hii katika nchi yetu.
 
Kunyonga ni sheria mbaya sana.. Madawa ya kulevya ni mabaya kupindukia, lakini Kama kuna msafi hata mmoja na awe wa kwanza kuweka sheria ya kuondoa wenzao duniani
 
Back
Top Bottom