Kulipeleka kombe Ofisi za GSM badala ya Jangwani ni dharau kubwa kwa uongozi, wanachama na mashabiki wa Yanga

Mwishokambi

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
303
1,158
Kwa kweli ni kioja cha mwaka, Yanga na Simba zinajulikana makao makuu yao ni wap, Yanga wapo pale Twiga na Jangwani na Simba wako pale kariakoo Msimbazi, wote wawili wako Kariakoo.

Jana, Yanga wamepita na kombe la ligi jiji zima la dar es salaam na kwa kweli nawapongeza sana kwa kuhamasisha umati ule bila kujali nini wala nini, sasa nachojiuliza sababu za kombe kupelekwa ofisi za GSM ni zipi badala ya pale jangwani, huo kama sio undondocha ni nini, GSM kama anadhamini yanga kwa kulipa mishahara, posho na kila kitu hiyo haiondoi heshima kwa viongozi wetu, in fact hata kama wanadhamini bado heshima na tamaduni ya yanga iwepo, kwahiyo uongozi wa yanga upo GSM, kwann uongozi wa yanga akiwemo Mshindo Msolla walibaguliwa jana na kuonekana hawana maana, yaani kwa sababu GSM inawafadhili yanga basi ndio tuwe mahayawani namna hii, kwamba GSM kila wanachokifanya ndio iwe ndio mzee, najiuliza kama GSM wamelibeba kombe na kuondoka nalo, je likiibiwa ataulizwa Msolla na uongozi wake au aulizwe Hersi.

Haya mambo haya Mo dewji hana ulimbukeni nao, waandishi wa habari mnaogopa kujadili hili kwa kumhofia Manara, yaani kombe libebwe had ofc za GSM na sherehe zifanyikie huko halafu mnashindwa kuelimisha umma kama hiyo ni sawa au hapana.

Kwann sasa tusiamini kuwa ubebaji wa kombe msimu huu kwa gharama za GSM ulikuwa na 'namna', kwamba bila GSM Yanga isingeweza kushika hata nafasi ya 2.

Miaka ya nyuma akina marehemu akilimali walipinga habari hizi, ni bora ufe maskini ubaki na heshima kuliko kufa tajiri ukiwa na fedheha.

Hongera Seneta Imani Mahugila Madega kwa kujitokeza hadharani na kupinga baadhi ya mambo ndani ya timu.
 
Kwa kweli ni kioja cha mwaka, Yanga na Simba zinajulikana makao makuu yao ni wap, Yanga wapo pale Twiga na Jangwani na Simba wako pale kariakoo Msimbazi, wote wawili wako Kariakoo...

Kombe ni la GSM lile, hao wanaojiita wananchi wameshawahi kuchangia hata cent kwenye usajili na uendeshaji wa Club kwa ujumla wake? Yanga ni Mali ya Ghalib.
 
Kwa kweli ni kioja cha mwaka, Yanga na Simba zinajulikana makao makuu yao ni wap, Yanga wapo pale Twiga na Jangwani na Simba wako pale kariakoo Msimbazi, wote wawili wako Kariakoo...
Baada ya timu kuwasili airport ilienda Jangwani tena kupitia msimbazi
Ratiba.jpg
 
Ishu ya kujua kusoma na kuandika inetuletea matatizo makubwa sana,mambo yetu wananchi yanakuumaje we kolo?
 
Back
Top Bottom