Kulipa mahari kwa ajili ya kuoa ni adhabu

lutemi

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
1,743
1,379
Wadau nimesoma kitabu cha Mungu (BIBLIA) nimegundua kwamba utoaji mahari kwa ajili ya kuoa halipo katika maandiko matakatifu.

Bali nimeona kwamba zamani mtu anayetaka kuoa alipeleka zawadi anayoona yeye inafaa.

Mahari ni adhabu na hii ilitokea kwa mtoto wa Yakobo aliyeitwa Dina baada ya kubakwa na kubikiriwa na wafilisti na ilikuwa chukizo sana kwa kaka zake Dina na wakaamua kuwatoza wafilisti walete nyama za magovi yao yaani watahiriwe na walipofanya hivyo wakauawa.

Kwa hiyo mahari ni upagani. Mahari ni unyanyasaji. Mahari kwa wacha Mungu ni kushusha thamani (value) ya binti yako kwamba yeye analingana na kiasi hicho kilichotolewa.

Mahari inafanya vijana wengi wakimbilie makahaba wakawaacha mabinti. Mahari inavunja mmomonyoko wa maadili.

Nimeona hata waislamu hawatozi mahari. Naomba serikali ifute mahari.

Karibu wadau mchangie.
 
unaongozwa na umasikini

nina uhakika 100% ungekua una hela au maisha ya kina MO au Bakhressa

usingekubali kumchukua mpenzi/mke wako bure bila kutoa asante lkwa familia aliyotoka

tena wewe ndio ungetoa hadi Meli kwa baba mkwe kama asante ya jinsi gani umemfurahia mke waliekulelea

Ukiona mtu anapinga mahari ujue ni hali ya maisha tu ni ngumu ila ki uhalisia

Mahari nikiwa na hela naweza TOA mahari hadi ukweni wakanishangaaaa maana ni ntamwaga mipesa.

Lakini kwa sasa hivi sina pesa

naunga hoja mkono MAHARI IFUTWE
 
Mimi nilipomwoa wife niliamua kumlipia mdogo wake ada ya chuo first year na nikambeba. Sasa hapo sijui ile walihesabu kama mahari au la!.
Tunaishi na life linasonga.
 
Wadau nimesoma kitabu cha Mungu (BIBLIA) nimegundua kwamba utoaji mahali kwa ajili ya kuoa halipo katika maandiko matakatifu.

Bali nimeona kwamba zamani mtu anayetaka kuoa alipeleka zawadi anayoona yeye inafaa.

Mahali ni adhabu na hii ilitokea kwa mtoto wa Yakobo aliyeitwa Dina baada ya kubakwa na kubikiriwa na wafilisti na ilikuwa chukizo sana kwa kaka zake dina na wakaamua kuwatoza wafilisti walete nyama za magovi yao yaani watairiwe na walipofanya hivyo wakauawa.

Kwa hiyo mahali ni upagani. Mahali ni unyanyasaji. Mahali kwa wacha Mungu ni kushusha thamani (value) ya binti yako kwamba yeye analingana na kiasi hicho kilichotolewa.

Mahali inafanya vijana wengi wakimbilie makahaba wakawaacha mabinti. Mahali inavunja mmomonyoko wa maadili.

Nimeona hata waislamu hawatozi mahali. Naomba serikali ifute mahali.

Karibu wadau mchangie.

Ni Mahari na sio Mahali....

Turudi kwenye mada, umesema maandiko yameandika walikua wanatoa 'zawadi' wanayoona inafaa... hiyo zawadi ndio Mahari yenyewe, huwezi mchukua binti kwa wazazi wake kireja reja tu labda kama hujui maana ya mahari naomba nikujuze....

Mahari maana yake ni zawadi apewayo binti baada ya kujitunza mpaka anafikia kuolewa, lakini pia ni zawadi kwa wazazi baada ya kumtunza mtoto wao mpaka anafikia kuolewa je kujitunza ni nini?? Ni Bikraaaaa, lol.

Kwa waislam binti atataja yeye mahari aitakayo na mahari ni zawadi ya binti labda yeye aamue kuigawa na wengine wapate.
 
unaongozwa na umasikini

nina uhakika 100% ungekua una hela au maisha ya kina MO au Bakhressa

usingekubali kumchukua mpenzi/mke wako bure bila kutoa asante lkwa familia aliyotoka

tena wewe ndio ungetoa hadi Meli kwa baba mkwe kama asante ya jinsi gani umemfurahia mke waliekulelea

Ukiona mtu anapinga mahari ujue ni hali ya maisha tu ni ngumu ila ki uhalisia

Mahari nikiwa na hela naweza TOA mahari hadi ukweni wakanishangaaaa maana ni ntamwaga mipesa.

Lakini kwa sasa hivi sina pesa

naunga hoja mkono MAHARI IFUTWE

Mkuu mahali unapangiwa , lete mkaja wa mama mbuzi za ukoo sijui wakati unamtongoza ulipita niia hii yaani kama unakomolewa hivi. Hebu mahali ifutwe kabisa ila ibakie zawadi tu yaani mtu anaeoa yeye ndio atoe zawadi kwa wazazi wa mke sio wazazi wapange
 
Kwenye kitabu cha Mwanzo kinamuelezea Musa ambaye alitaka kuoa akaambiwa mahari yake ni kumfanyia kazi baba mkwe kwa miaka 7. Alipomaliza na kutaka kumchukua mke akagewa dada mtu wakati yeye alimtaka mdogo mtu, akaambiwa si vyema mdogo aolewe kabla ya mkubwa.

Akaulizia mahari ya mdogo, nayo ikawa ni kumfanyia kazi baba mkwe kwa miaka 7, akafanya na alipomaliza akachukua wake zake wawili akasepa.

Now dunia ya kina Musa mtu aliishi hadi miaka 300 so kupoteza miaka 14 kumfanyia kazi mkwe kama mahari ni sawa tu. Siku hizi ukifikisha miaka 70 yaani ni hautamaniki. Utakua radhi kupoteza miaka 7 kwa mkwe? Tena kipindi hicho chote hamna kumegana?

Badala yake ndiyo tunato vitu. Ukiambiwa lete ng'ombena wewe siyo mfugaji ng'ombe hauna si ndiyo unapeleka pesa? Sielewi wanaosema mahari apewe binti. Musa hakumfanyia kazi binti wa kwanza wala wa pili, alimfanyia kazi BABA.

Huu uzi kusema kulipa mahari ni upagani na inadaiwa umepata references za biblia. Hii ni biblia gani haukuona habari za Musa?
 
Mkuu kuna jambo halipo sawaa hapo, Mahali ipo kisheria kwa dini zote labda hoja yako ingekuwa mahali kubwa kuliko kipato cha mwoaji kidogo ungeeleweka.

Binafsi mie ni uwezo tu sikuwa nao ila ningetoa zaidi ya mke alichoomba nitoe. Japo naelewa bado ni wazazi wangu nitafanya mengi mema juu yao, Waswahili wanasema ukipatia kuoa huwa unatamani kufanya mengi zaidi kwa wakwe zako sababu unahisi ulichotoa hakiendani na unachopata/kufanyiwa kutoka kwa binti yako.
 
Ulipaji wa Mahari huwa unategemea jamii waliyopo waoaji na huwa haina kiwango maalum.

Ndoa katika Uislam haiwi ila kwa Mahari, kwa dalili ya neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :
وآ توا النساء صدقاتهن نحلة

“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)

Na Akasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Surat Al-Ahzaab:
يا أيها النبي إنا أحللنا لك أزواجك اللاتي آتيت أجورهن

“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-Ahzaab: 50)

Na Akasema vile vile katika Surat An-Nisaa:
فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة

“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)

Uislam haukupanga malipo maalum ya mahari, cha kuzingatia hapa katika mahari ni maridhiano ya pande mbili husika, lakini kinachopendeza ni kuwa iwe hafifu na kinachowezekana bila ya taklifa kwa yule muoaji.
 
Kama kweli umedhamiria kuoa mahali sio kikwazo cha kubweka kiasi hicho.Ni mapatano tu na tukumbuke huu ni utamaduni wetu kama waafrca.
 
Kuna baadhi ya makabila mahari ni kama kukomoana. Wanataka ng'ombe hai wanaotembea tena wanaingia wenyewe zizini na kuchagua walionona. Kwa hali hii wanaooza vijana wao walikimbilia zizini mapema na kuwatoa ng' ombe ambao waliona kuwa wana afya na muonekano mzuri. Kibaya zaidi idadi ya ng'ombe waliohitajika kama mahari ni kuanzia ishirini kwenda juu. Na ole wako binti awe mweupe, ndo utakomolewa haswa.
 
Kwenye kitabu cha Mwanzo kinamuelezea Musa ambaye alitaka kuoa akaambiwa mahari yake ni kumfanyia kazi baba mkwe kwa miaka 7. Alipomaliza na kutaka kumchukua mke akagewa dada mtu wakati yeye alimtaka mdogo mtu, akaambiwa si vyema mdogo aolewe kabla ya mkubwa.

Akaulizia mahari ya mdogo, nayo ikawa ni kumfanyia kazi baba mkwe kwa miaka 7, akafanya na alipomaliza akachukua wake zake wawili akasepa.

Now dunia ya kina Musa mtu aliishi hadi miaka 300 so kupoteza miaka 14 kumfanyia kazi mkwe kama mahari ni sawa tu. Siku hizi ukifikisha miaka 70 yaani ni hautamaniki. Utakua radhi kupoteza miaka 7 kwa mkwe? Tena kipindi hicho chote hamna kumegana?

Badala yake ndiyo tunato vitu. Ukiambiwa lete ng'ombena wewe siyo mfugaji ng'ombe hauna si ndiyo unapeleka pesa? Sielewi wanaosema mahari apewe binti. Musa hakumfanyia kazi binti wa kwanza wala wa pili, alimfanyia kazi BABA.

Huu uzi kusema kulipa mahari ni upagani na inadaiwa umepata references za biblia. Hii ni biblia gani haukuona habari za Musa?

Wale wazazi wao walikuwa wapagani..... nini nimeoa na nina watoto wa kike sitaweza abadani kuwauza watoto wangu.
 
Ulipaji wa Mahari huwa unategemea jamii waliyopo waoaji na huwa haina kiwango maalum.

Ndoa katika Uislam haiwi ila kwa Mahari, kwa dalili ya neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) :
وآ توا النساء صدقاتهن نحلة

“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)

Na Akasema tena Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Surat Al-Ahzaab:
يا أيها النبي إنا أحللنا لك أزواجك اللاتي آتيت أجورهن

“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-Ahzaab: 50)

Na Akasema vile vile katika Surat An-Nisaa:
فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة

“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)

Uislam haukupanga malipo maalum ya mahari, cha kuzingatia hapa katika mahari ni maridhiano ya pande mbili husika, lakini kinachopendeza ni kuwa iwe hafifu na kinachowezekana bila ya taklifa kwa yule muoaji.

Nani anapanga mahali katika uislamu muoaji au muolewaji? Au wazazi wa muolewaji?
 
Kuna baadhi ya makabila mahari ni kama kukomoana. Wanataka ng'ombe hai wanaotembea tena wanaingia wenyewe zizini na kuchagua walionona. Kwa hali hii wanaooza vijana wao walikimbilia zizini mapema na kuwatoa ng' ombe ambao waliona kuwa wana afya na muonekano mzuri. Kibaya zaidi idadi ya ng'ombe waliohitajika kama mahari ni kuanzia ishirini kwenda juu. Na ole wako binti awe mweupe, ndo utakomolewa haswa.

Fact Mkuu.... ndio maana inafikia hatua mtoto ananyanyasika sana kwasababu kisa mahali ilitolewa
 
Kama kweli umedhamiria kuoa mahali sio kikwazo cha kubweka kiasi hicho.Ni mapatano tu na tukumbuke huu ni utamaduni wetu kama waafrca.

Issue sio mahali ila maana ya mahali na kinachotozwa katika mahali
 
Kwanza jamani kinachotolewa ni MAHARI sio mahali. Pili wewe mtoa mada umesoma Biblia ipi? Soma Mwa 24:22. Mfanyakazi wa Ibrahimu aliyetumwa kumposea Isaka mtoto wa Ibrahimu mke, alimvika binti aliyemwona anamfaa Isaka pete yenye uzito wa nusu shekeli (gram 5) za dhahabu, na kumvika bangili mbili (vikuku viwili) vya dhahabu ya shekeli kumi yaani gramu ishirini. Hivyo kapewa binti. Wewe uko tayari kumpa binti unayetaka kumwoa zawadi inayolingana na gramu 25 za dhahabu? Halafu mstari wa 53 unasema:- Kisha akampa Rebeka (binti anayeolewa) vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na mavazi, na akampa mama yake na kaka yake vitu vya thamani pia. Hivyo vitu alivyotoa NDIO MAHARI YENYEWE. Tatizo linakuja wakati wazazi wa binti wanapotaka "kumuuza" binti yao wanamwekea kima (yaani toa ng'ombe kumi na mbuzi ishirini au milioni tano....n.k.). Huwezi kumchukua bure bure binti aliyegharamikiwa na wazazi wake na kusomeshwa nao mpaka akawa mtu mzima. Haiingii akilini. Kama unataka kuoa bila kutoa mahari basi humthamini mkeo. Akikudharau halafu siku ya siku akikwambia "narudi kwetu maana hujanitolea hata mahari utamwambia nini??
 
Back
Top Bottom