Kindeena
JF-Expert Member
- Sep 27, 2017
- 9,031
- 15,736
Baadhi ya viongozi wa Wafanyabiashara wadogo katika Soko la Kariakoo, Dar es Salaam, kwa kushirikiana na askari wa Jiji wanadaiwa kuwatesa na kuwanyanyasa Wafanyabiashara wadogo, na kuwatoza Wafanyabiashara hao faini kubwa kati ya Tshs 50,000/= hadi 300,000/= kama adhabu ya "makosa" mbalimbali na hawatoi risiti.
Mfano leo Jumamosi, 26/03/2022, baadhi ya Wafanyabiashara wadogo walikamatwa na mizigo yao kuchukuliwa kisha kupelekwa ofisini kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kufungua biashara wakati Mkuu wa Wilaya ya Ilala anafanya usafi. Kwa hiyo wao pia walipaswa kwenda kufanya usafi na siyo kufungua biashara.
Katika kujitetea, Wafanyabiashara wadogo hao wameamriwa kulipa laki 3 ili warudishiwe mizigo yao, na wakikaidi watapelekwa Mahakama ya Jiji.
Mmoja ya Wafanyabiashara hao kanieleza kwamba waliwaomba wapunguziwe ndipo wakaafikiana kwamba walipe elfu 50 (cash mkononi) kila mmoja na wasipolipa watakiona.
Inaelezwa kwamba, ofisini hapo kuna namba ya akaunti kwa ajili ya kwenda kulipia adhabu, lakini viongozi wanapokelea pesa mikononi na hawatoi risiti wala maandishi yeyote.
Mmoja ya viongozi hao, alisikika akimwambia mfanyabiashara mmoja kwamba hiyo pesa ya adhabu asiitoe hadharani kwa sababu ukutani kuna namba maalumu ya kulipia kwa hiyo asije akawaingiza matatizoni kwa kupokea fedha kinyume na utaratibu uliowekwa na Serikali.
Nimedokezwa kwamba hata mfanyabiashara akikomaa kwamba apelekwe mahakamani, hapelekwi na badala yake wanashikilia tu mizigo yake na au kuzunguka naye kwenye gari ili aingie hofu na alipe fedha ambazo wanakula hao viongozi.
Taarifa zinasema kwamba kuna sehemu Wafanyabiashara wataotuhumiwa hupelekwa na hiyo sehemu panaitwa "depo"; yaani ni kama mahabusu fulani hivi ya kuwatesea wakosaji.
Hata kama ni kushughulikiwa, sheria ifyatwe. Iweje mtu afanye kosa halafu bidhaa zinashikiliwa, anatozwa hela kubwa na hapewi risiti???
Kwanza hakuna uwiano kati ya kutenda kosa na kisha mgambo kuchukua bidhaa za wamachinga. Huo ni uhuni na ni unyang'anyi.
Machinga walipagwa na Serikali kwa agizo la rais, sasa iweje wanafanyiwa ukatili?
Tafadhali sana, wadau wa serikali hususani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ilala na maafisa wengine wa chama na Serikali fuatilieni hili ili kuweka mambo sawa na hao viongozi warudishe pesa za hao Wafanyabiashara wadogo.