Kulipa kodi ni amri ya mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulipa kodi ni amri ya mungu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mateso, Aug 4, 2009.

 1. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wakuu nimepitia andiko takatifu na kukuta kumbe kila kiongozi anatoka kwa Mungu kwa hivyo aheshimiwe na kupendwa. Warumi 13: 1. Unasema 'Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile ilyopo imeamriwa na Mungu.' mstari 6-7 inasema ' Kwa sababu hiyo tena muwalipe kodi kwa kuwa wao ni wahudumu wa Mungu, wakidumu katika kazi hiyo hiyo. Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahili hofu, hofu; astahili heshima, heshima.' Sasa msimamo wetu kwa hali ya sasa hivi ni upi kwa uongozi huu.
   
 2. I

  Ivilikinge Member

  #2
  Aug 4, 2009
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Da mi nadhani ni haki kweli kulipa kodi ni muhimu sana ila sasa kwa hizi mamlaka zetu kodi wanatumia kwa vitu ambavyo havistahili ndio maana watu wengine wanagoma kulipa kodi.e.g.angalia sehemu kama mwenge watu wanalipa kodi sana pale kituoni lakini mitaro haifai,angalia ubungo na masoko almost yote tanzania nzima
   
 3. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Lakini maandiko hayo yanasema anayestahili hofu apewe hofu, hivyo kama mambo ndo hayo kwa nini tusihofu kulipa kodi?
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mi nafikiri hilo andiko lifanyiwe ammendment ili liendane na wakati.

  Linatakiwa liseme Kiongozi mwaadilifu anatoka kwa Mungu ........
   
 5. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #5
  Aug 4, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiukweli ni kwamba maandiko ya kwenye biblia mara nyingi inabidi uyatafari kwanza na siyo kuyachukulia vile yalivyo...Inawezekana maana haikuwa hiyo unayoifikiria...!
  m out!
   
 6. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #6
  Aug 4, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wa mmoja hebu jaribu kusoma fungu hilo halafu uone kama kuna different interpretation. Maana hata Yesu aliwaambie wafarisayo ya Kaizari mpeni Kaizari na ya Mungu mpeni Mungu. Mimi nilitaka kujua kama tunaweza kugoma kulipa kodi iwapo haitumiki ipasavyo kwa kuwa sehemu ya mwisho ya mstari wa saba tajwa hapo juu unasema anayestahili hofu mpeni hofu na anayestahili heshima mpeni heshima. Je uongozi wa sasa kwa upnde wa kodi haustahili kupewa hofu?
   
 7. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #7
  Aug 4, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  biblia haiwezi kubadilishwa, hutakiwi kupunguza wala kuongeza neno.
   
 8. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #8
  Aug 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Je wewe umelinganisha mambo hayo ya kwenye Bible na reality on the ground Tanzania?

  Ni lazima ufanye malinganisho na uone uzito umeegemea wapi.

  Kiongozi hatoki kwa Mungu hio ni imani ya kiroho. Je kama wao ni wahudumu wa Mungu wanajihusishaje na UFISADI?

  Kuhusu heshima, kila mtu anastahili heshima na kuthaminiwa utu wake lakini ukumbuke kwamba pale Mungu anapoona kwamba umeshindwa kulinda heshima na utu wako yeye ataamua kukuanika hadharani na umati utakuona wewe ni fisadi, mwizi, laghai, na sifa zote mbaya.

  Hali hii ikitokea wewe tena hufai mbele ya Mungu na jamii inayokuzunguka.
   
Loading...