Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 309
Wakulima wa Tanzania ni miongoni mwa watu wenye dhiki na shida zisizomithilika.
Kodi wanalipa lakini serikali yao haiwapatii huduma za jamii-shule wanazosoma watoto wao ni vichekesho vitupu, miondombinu (barabara, mawasiliano, etc) ni kejeri kubwa, mbwa wa watawala wanapatiwa huduma za afya zilizo bora kuliko wanazopata zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura (wakulima).
Lakini kejeri kubwa kuliko zote ni kuwazuia wakulima kuuza mazao yao nje ya maeneo fulani wanayotaka watwawala, kuwalazimisha wauze mavuno yao kwa wateja inaowataka serikali!
Kwanza huku ni kukiuka haki ya msingi kabisa ya uhuru wa kuchagua lakini pia ni kuhakikisha kuwa wakulima wanaendelea kuwa masikini kwani.
Ninapoandika kuna zuio la kuuza mchele wa Tanzania nje ya nchi, mwaka jana ulikuwa mwaka wa mavuno mazuri na wakulima wengi walitarajia kuwa wangenufaika na jasho lao lakini watawala wetu wamepiga marufuku mchele wetu kuvuka mipaka ambako ungewezesha wakulima wa TZ kupata bei nzuri (tunasikia waligombana na marais wa nchi jirani hivyo kuwakomoa ni kuzuia mchele, ambao wanautegemea utoke TZ).
Kwa nini wenye viwanda wanahamasishwa kuuza bidhaa zao nje ya nchi? Au wakulima wetu ni second class citizens (daraja la chini, aka watawaliwa)?