Kulikuwa na faida gani ya kubadili jina la shirika letu la habari kutoka TVT (Televisheni ya Taifa) na kuitwa TBC (Tanzania Broadcasting Corporation)?

Hili swali hata ukiwauliza IPP watakupa jibu moja tu (Mabadiliko).

Hata IPP walikuwa na ITV na ITV2. Wakabadilisha ITV2 kuwa EATV. Its all about branding. Kumbuka TBC sasa inatazamwa dunia nzima sio Tanzania pekee. Na Radio tanzania Dar es salaam sasa inasikika dunia nzima sio Dar es salaam pekee wala Tanzania pekee.

Brand name TBC inatosha, japo contents zao ni za chama kimoja.

Cc Pascal Mayalla
ITV bado ipo...
EATV ni new brand.

Why from TVT to TBC!?
Mambo yasiwe mengi. Jibu shortly.
 
Radio Tanzania Dar es Salaam "RTD" na "Televisheni ya Taifa" katika kuanzishwa kwake hayakuwa mashirika ya umma bali idara ndani ya wizara ya habari vikiwa kama vituo tu vya kutoa habari kwa njia ya redio na luninga.

Lakini mwaka 2007 idara hizi mbili za kiserikali ziliunganishwa ili kuunda shirika moja la habari (kuwa shirika la umma) kwa kuzingatia sheria ya mashirika ya umma ya mwaka 1992. (Tafuta faida zilizoanishwa kwenye sheria ya mashirika ya jmma ya 1992).

Ukisoma historia ya vyombo vya habari, hapo awali wakati wa ubeberu kulikuwa na sijui Sauti ya Dar es Salaam, baadaye mwaka 1955 ikaja TBS(Tanganyika Broadcasting Service) kama kituo cha utangazaji cha serikali ya ukoloni na makao makuu yakawa pale ilipokuwa RTD Pugu Rd, halafu mwaka 1956 ikaja TBC (Tanganyika Broadcasting Corporation) ambayo ilidhamiriwa iwe kama ilivyo BBC.

Mwaka 1965 TBC ikavunjwa na bunge la wakati huo kwa shinikizo la wazalendo (maana ilikiwa ikiendeshwa kwa sera za wakoloni na hata habari ilikiwa ikiandaliwa na BBC n.k). Baada ya hapa ndipo ilipozaliwa RTD (Radio Tanzania Dar es Salaam).

Sasa kwa nini tuliendelea kuwa na matangazo ya redio tu na hatukuwa na televisheni hata baada ya ukoloni, jibu ni kuwa Mwl Nyerere hakupendelea nchi iwe na kituo cha televisheni kwani aliona ni gharama kubwa kukiendesha, ungekuwa na utegemezi sana wa ruzuku.

Mwaka 1999 kwa mara ya kwanza serikali ikaanzisha kituo cha televisheni "TVT" na mwaka huu kilianza kwa majaribio tu, mwaka 2000 kikaanza kazi rasmi.

Mwaka 2007, TVT na RTD zikaunganishwa tena kurejelea mfumo ule wa TBC ya ukoloni ya kufanya kuwa shirika la habari, utofauti na ukoloni this time around likawa ni shirika lenye kurusha matangazo ya redio na televisheni.
 
TBC ilizaliwa baada ya kuunganisha RTD Radio Tanzania Dar Es Salaam na TVT Tanzania Television na kwakua vyombo hivyo viliunganishwa ili viwe chini ya shirika moja la umma ili kuleta ufanisi kwenye muundo wa utendaji na uendeshaji na uwe wa kisasa zaidi na kiushindani ndio Leo hii tuna TBC
Tbc ilikuwepo kabla ya Rtd, hii Tbc ya sasa ni kujirudia kwa historia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini ndani ya TBC kusingebaki TVT na Radio Tanzania (RT)? Kwanini walibadili majina? Kulikuwa na ulazima gani wa kubadili majina?
Mfumo wa uendeshaji ulikuwa unabadilishwa kutoka idara na kuwa shirika la umma.

Kiserikali unapobadilisha sera, ni lazima mfumo na uendeshaji nao ubadilike kulingana na matakwa ya wakati huo.

Sasa yatakuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma kuwa na mashirika mawili ya habari yaani RTD na TVT, ilihali maudhui unayotaka kuyafikisha kwa umma ni yale yale.
 
Radio Tanzania Dar es Salaam "RTD" na "Televisheni ya Taifa" katika kuanzishwa kwake hayakuwa mashirika ya umma bali idara ndani ya wizara ya habari vikiwa kama vituo tu vya kutoa habari kwa njia ya redio na luninga.

Lakini mwaka 2007 idara hizi mbili za kiserikali ziliunganishwa ili kuunda shirika moja la habari (kuwa shirika la umma) kwa kuzingatia sheria ya mashirika ya umma ya mwaka 1992. (Tafuta faida zilizoanishwa kwenye sheria ya mashirika ya jmma ya 1992).

Ukisoma historia ya vyombo vya habari, hapo awali wakati wa ubeberu kulikuwa na sijui Sauti ya Dar es Salaam, baadaye mwaka 1955 ikaja TBS(Tanganyika Broadcasting Service) kama kituo cha utangazaji cha serikali ya ukoloni na makao makuu yakawa pale ilipokuwa RTD Pugu Rd, halafu mwaka 1956 ikaja TBC (Tanganyika Broadcasting Corporation) ambayo ilidhamiriwa iwe kama ilivyo BBC.

Mwaka 1965 TBC ikavunjwa na bunge la wakati huo kwa shinikizo la wazalendo (maana ilikiwa ikiendeshwa kwa sera za wakoloni na hata habari ilikiwa ikiandaliwa na BBC n.k). Baada ya hapa ndipo ilipozaliwa RTD (Radio Tanzania Dar es Salaam).

Sasa kwa nini tuliendelea kuwa na matangazo ya redio tu na hatukuwa na televisheni hata baada ya ukoloni, jibu ni kuwa Mwl Nyerere hakupendelea nchi iwe na kituo cha televisheni kwani aliona ni gharama kubwa kukiendesha, ungekuwa na utegemezi sana wa ruzuku.

Mwaka 1999 kwa mara ya kwanza serikali ikaanzisha kituo cha televisheni "TVT" na mwaka huu kilianza kwa majaribio tu, mwaka 2000 kikaanza kazi rasmi.

Mwaka 2007, TVT na RTD zikaunganishwa tena kurejelea mfumo ule wa TBC ya ukoloni ya kufanya kuwa shirika la habari, utofauti na ukoloni this time around likawa ni shirika lenye kurusha matangazo ya redio na televisheni.
Well said...
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Kwanza ninaomba kuanza kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo pamoja na shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) kwa kuamua kuwa Wazalendo kwa vitendo zaidi na kuamua kuboresha muonekano wa TBC.

Sasa hivi huwa nikiwa ninatazama TBC ARIDHIO ile saa moja jioni ni kama vile ninatazama CNN, BBC au Al Jazeera kwa maana camera na majukwaa ni ya kisasa, watangazaji wa kiume ni watanashati sana, hao akina dada ndio usiseme yaaani ni warembo saaaaana hususan yule dada wa kipare wanamuita Elizabeth Mramba.

I congratulate you guys once again. Huyo Elizabeth Mramba kama hajaolewa mpaka sasa ninaomba mwenye number zake anipe mara moja wakuu kwa maana sio kwa weupe ule. Hahahahahaaaa, I am joking.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kulikuwa na umuhimu gani wa kubadili jina la shirika letu la habari kutoka TVT (Televisheni ya Taifa) na kuitwa TBC (Tanzania Broadcasting Corporation)?

View attachment 1589921

Kama suala ni structual change (shake up) kwani isingeweza kufanyika bado ikibeba jina hilo hilo pamoja na logo ya TVT?

Kulikuwa na umuhimu gani wa kubadili jina la shirika letu pendwa, muhimu na la kizalendo katika kutangaza misimamo ya taifa hili imara barani Afrika lililojaa mashujaa na wachapakazi?

Ninajua kuna watu watakuja na hoja kwamba TBC ilizaliwa baada ya kuunganisha RTD (Radio Tanzania Dar Es Salaam) na TVT.

Lakini mbona kampuni ni moja ya Microsoft lakini bidhaa ni tofauti tofauti kama vile Windows, Office, Internet Explorer, Visual Studio na Xbox.

Kwanini TBC isingebaki kama TBC lakini ndani yake kuwe na TVT pamoja na Radio Tanzania? Kwanini walibadili majina? Kulikuwa na ulazima gani kufanya hivyo?

Mbona Serengeti, Manyara na Kilimanjaro ni vivutio vya kimataifa lakini bado vinabeba majina yale yale ya zamani na wazungu hawaja-ignore?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

huyu mtoto Eliza ni mzuri sana ila jamaa ake aliyemnunulia Benzi c class ndiye anasugua mtoto na jamaa anamlinda mbaya
 
Huyu mtoto anapaswa kuwa festi ledi 2030,
 
Lugha ya mabeberu tamu aisee. Kuna watu hapo juu wanasema kua TVT+RTD = TBC. na mimi nauliza kwani hakuna jina la kiswahili mpaka waite TBC.
 
Siku aliyofukunzwa Tido Muhando ndo siku niliyoacha kuangalia TBC,

Hata hivyo Ni ubeberu tu uliokomaa, Mana sisi vitu vyote tinavyofanya tumechabo kwa mkoloni Muingereza mapaka football tunaendesha kwa mfumo wa uingereza , nadhani katiba mpya tungechabo kwa Mmarekani. Tuwe na siasa za mabeberu, Mana vingi tunachabo kwao
 
Back
Top Bottom