PreGE2025 Kulikoni polisi kuingia Kisutu na mask za majambazi? Je, hiyo ni sehemu ya sare yao? Kama sio kwanini wazivae?

PreGE2025 Kulikoni polisi kuingia Kisutu na mask za majambazi? Je, hiyo ni sehemu ya sare yao? Kama sio kwanini wazivae?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Yaani utafikiri waliomsindikiza ni gaidi lililoshindikana ambalo linamiliki magenge ya uhalifu., kumbe ni mwanasisa tu wa upinzani.
 
Wakuu,

Moja ya matukio yaliyonishangaza jana kwenye kesi ya Lissu pale Kisutu ni baadhi ya polisi kuvaa mask kama za majambazi ambao hawataki kujulikana sura zao!


Nilijiuliza mengi sikupata majibu! Kwanini wavae vile wakati zinahusishwa na matendo ya kiuhalifu? Kwanini wajizibe sura kwanza? Ni sehemu ya sare yao? Kama ndivyo ina maanisha nini? Kama si sehemu ya sare kwanini wazivae?


Matukio mengi ya asiyojulikana yamekuwa mengi wakatk huu na moja ya kitu wanafanya ni kujiziba sura (kutokana na maelezo ya manusura) ili wasitambulike. Sasa hawa kuvaa hivi, kuna ka uhusiano na wale wanaohusika kwenye utekaji, maana tunaambiwa huwa wanajitambulisha kama polisi na wana silaha za polisi, je mavazi hayo yanatoka huko?


Yaani maswali mengi, kama hiyo ni sehemu ya sare zao lengo ni nini hasa? Au Lissu alikuwa anatoa harufu mbaya ikabidi wajifunike gubi gubi wasitapike? 😂🤣

Utani pembeni, hili limenishangaza na kunifikirisha, mwenye majibu njoo utuondoe vumbi.
Tunaposema hawa ni majambzi wanaovaa uniform huwa hatuwasingizii
 
Askari anavaa sare haina badge number wala jina sio mchezo
 
Kwani hao polisiCCM na wao hawahofii maisha yao?Wanaogopa kutambulika kwa mambo wanaolazimishwa kufanya wakirudi uraiani!
 
Back
Top Bottom