Hii kali ya kufungia mwaka 2010, viagra na kahawa! Uongo mwengine hauna hata mwelekeo jamani.
Hii kali ya kufungia mwaka 2010, viagra na kahawa! Uongo mwengine hauna hata mwelekeo jamani.
Mkuu hapo hakuna uongo. Kumbuka kuwa Kahawa inasababisha mapigo ya moyo kuwa juu, hii ni kweli na haipingiki. Halafu tena viagra ni kiboko kwa mapigo ya moyo, ndiyo maana unashauriwa kabisa uzingatie kipimo kwa kuzingatia umri, uzito, magonjwa hatarishi kama kisukari, blood preasure, etc. Sasa basi kwa umri wa mzee wetu yule marehemu halafu uchanganye kahawa na viagra kwa hakika ni umauti. Siamini kama mjumbe aliyesema hili atakuwa ametunga. Kumbuka kile kifo, hakikusemewa sana!!! Hukujiuliza kwa nini?
Kuhusu Mzee Jumbe hicho ndicho kifungo chake cha maisha ndani ya makazi yake. Alijengewa nyumba ile na serikali na kutengwa kabisa na wazanzibari ili kukata mawasiliano. His movements and actions are subject to watchdogs!! Hivi jamani watoto wake wako wapi?
Hivi, Karume alipoamua kupindua utawala wa Sultani alitoa fursa gani kwa Wazanzibari kujadilia na kutoa radhi yao?
Hilo nalo nenooo!Watu wanapotosha historia ya mapinduzi ya Zanzibar!! Aliyeongoza mapinduzi huko Zenj mwaka 1964 ni mganda aliyejulikana kwa jina la Field Marshall John Okello!! Wazanzibari hawataki kumtukuza huyu bwana kwani wanadhani atawapunguzia sifa wakina Natepe!!
Aboud Jumbe Mwinyi alikuwa Rais wa pili wa Zanzibar toka mwaka 1972 hadi mwaka 1982 alipotimuliwa na CCM baada ya kuchafuka kwa hali ya hewa.Nasikia siku hizi anaishi mji mwema kigamboni Dar es Salaam akisubiri siku zake ziishe hapa dunia.
Hivi, Karume alipoamua kupindua utawala wa Sultani alitoa fursa gani kwa Wazanzibari kujadilia na kutoa radhi yao?
Nilikuwa sijui kama nyerere alikuwa dikteta kiasi hiki. yaani alikuwa analotaka ndo linalokuwa. Hii ni aibu kwa mtawala ambaye kila kukicha anasifiwa. Alietaka awe rais ndo aliekuwa. Hakupenda kupingwa wala mtu kuwa na mawazo mbadala. Hii ni hatari kwani akiwa hata na maoni ambayo hayana tija kama ya muungano hamna wakumshauri. we do not need a leaders of such kind. KULIKUWA NA UBAYA GANI WA KUACHIA HOJA KAMA ILIKUWAPO KWA MFANO HII YA MUUNGANO KUJADILIWA NA KUWA NA RADHI YA JAMII ZOTE HUSIKA? AU KWENYE HUO MUUNGANO KUNA SIRI GANI? KWA NINI HAKUTAKA KUJADILIWA? MATOKEO YAKE NAONA WATU WANAMKEJELI TU MZEE JUMBE. SISHANGAI HUENDA HUYU MZEE ALIKUWA SAHIHI. This is a century shame!
kama muungwana alivyosema huko juu mkuu, usipende kusema ni uogo tu kwa sababu hujakipenda kilichoandikwa, we toa sababu kuonyesha ni the other way around vinginevyo unataka kuleta ubishani usio na tija! kwani kutumia viagra kwa mtu mzima kama yule ni ajabu? alikufa gen.sani abacha kwa viagra tena sio kwa mkewe kwa hooker wa kirusi itakua yeye bana! mda aliotangazwa kafa ni mida flan ya ndio kwanza watu wanaenda kulala na pia hadi anaenda kulala alikua mzima kabisaaaaa!