Mandla Jr.
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 3,098
- 631
Wanabodi habari ya leo,
Binafsi naomba kusema ni vyema kuwajali na kuwahifadhi wapendwa wetu waliotutoka kwa njia nzuri na ambazo ziko kihalali kulingana na mila, desturi, tamaduni na dini tunazoziamini. Lakini pia niseme ni masikitiko sana kuondokewa na mtu katika jamii yetu na kaya zetu, lakini hayo huwa ni mapenzi ya Mwenyenzi Mungu kikubwa ni kuwaombea wapumzike kwa amani waliko tangulia.
Sasa, naomba nishangae mambo yanayoendelea kwa wenzetu Wachaga, kwakweli misiba yao ni sherehe kubwa, majigambo, ufahari mkubwa hakika hii sidhani kama ni jambo zuri hasa kwa wale ambao wanakuwa wamempoteza ndugu yao.
Misiba inakuwa mpaka na Pombe na vinywaji vingine vikali? Ufahari wa magari ya bei kubwa? Yote haya ni kwa faida ya nani? Mfano ukikaa barabara ya Arusha - Moshi utastaajabu utitiri wa magari ya kifahari kwenda kwenye msiba Moshi, hivi hili linawasaidia kweli wafiwa?
Utakuta mtu anatoka msibani analalamika, hoo mimi sikupata bia au hoo mimi sijala nikashiba. Kweli kweli ndugu zangu mmefikia huku....Hakika inaumiza sana.
Nimeyaona ndio maana nimesema, nisichukiwe kwa kusema ukweli!!
SIO JAMBO JEMA AU LENYE AFYA.
Mandla.