Kulikoni Mh.January Makamba Kutokuonekana kwenye Mitandao ya kijamii?

Emmanuel R. Ntobi

JF-Expert Member
Sep 23, 2014
691
1,490
Heshima Mbele!

Namuulizia yule kijana, aliejiaminisha kuwa yeye ndiye rais wa awamu ya tano Tanzania.

Bwana January Makamba, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia awamu ya Nne, alikuwa mgombea urais ndani ya CCM ( mpaka Tano bora) Mwanye mbwembwe nyingi, Ambaya sasa ni waziri wa Mazingira (uchafu) na muungano (Zanzibar-inamuhusu)

January Makamaba, kwa hulka yake ni kijana anaependa sana kutumia social media kuliko vingozi wengi wa CCM. Ana kundi la wana mtandao, ( Dogo janja)

Cha ajabu toka 05 November 2015, haonekani si FB, Tweeter wala Instagram.Kulikoni Mh. January Makamba kutokuonekana kwenye Mitandao ya kijamii?

Je! Anaogopa issue ya Zanzibar?
Je! Hana hoja kwa sasa?
Ama kapigwa mkwara na JPM ( kwa kumkosoa)?

Je! Serikali hii ya awamu ya Tano, haina lolote ambalo Mh.January anaweza ku-share nasi mitandaoni kama kipindi cha JK? Kulikoni bwana Waziri Dogo Janja?
 
Back
Top Bottom