Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,187
- 42,013
Wasalaam wanajamvi!
Sasa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu Mh Rais Samia achague mkurugenzi mkuu mpya wa TANESCO bwana Chande Maharage na baada ya hapo Waziri wa Nishati alivunja bodi ya tanesco na kuteua sura mpya ambayo alisema ni ya wataalam na wabobezi wanaojua biashara na ni weledi sana.
Waziri alikwenda mbali zaidi na kuweka wazi kuwa TANESCO ya sasa haitakuwa kama ile iliyopita kwani kwa sasa kila mtambo utafanyiwa matekebisho au matengenezo maana uko nyuma viongozi waliopita walizuia kufanyiwa matengenezo hivyo mitambo kulemewa kwa miaka mitano bila kufanyiwa marekebisho.
Mh Waziri na Mkurugenzi mkuu wa TANESCO walikwenda mbele zaidi na kusema wanakuja na tenesco ya kidijitali na inayojali wateja maana yake wateja watafungiwa umeme kwa haraka sana na umeme hautokatika katika kwani mitambo itafanyiwa matengenezo kila wakati.
Je, baada ya mwaka mmoja na zaidi ni kweli tuliyo ahidiwa na Makamba na Maharage yamefanikiwa?
Ni mchango wa wataalam wapya waliowekwa na Makamba kwenye bodi?
Ni mchango gani wa wafanya biashara walio wekwa kwenye bodi ya tanesco?
Tanesco ya January Makamaba na Maharage Chande imefanikiwa kwenye nini?