Kulikoni mabucha ya wanyama pori

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,862
2,000
Serikali ya Awamu ya Tano ilitoa utaratibu wa kuwezesha Watanzania kufungua mabucha ya wanyamapori mradi tu wawe wamefuata utaratibu. Hapa Mwanza kuna rafiki yangu alifuata taratibu zote na alianza kujenga bucha kwa gharama kubwa, alinunua gari ya kuwindia, alinunua bunduki ya aina yake kwa ajili ya kuwindia, alinunua mafriji kwa ajili ya kutunza nyama kutoka porini, alinunua mashine ya kukata nyama na vifaa vyote vinavyohitajika ili bucha yake ianze kazi.

Pamoja na kutimiza masharti yote alipigwa dana dana mpaka Rais wa Awamu ya Tano akafariki. Juzi nilipomuuliza kulikoni majibu niliyopata kwake yanasikitisha sana licha ya hasara kubwa aliyoingia. Yeye alinieleza kuwa vile vitalu ambavyo walitakiwa kwenda kuwinda tayari vimeishagawiwa na Serikali na hivyo hakuna yeyote atakayekuruhusu kuwinda kwenye kitalu chake. Aliendelea kunieleza kuwa awali nyati mmoja alitakiwa kuuzwa na Serikali kwa Tshs.600,000 sasa wenye vitalu ukitaka kumnunua nyati mmoja ni Tshs.1m/-. Anasema amepata hasara zaidi ya Tshs.150m/-. Tuiulize Serikali huu mradi nini hatma yake na kwa wale waliopata hasara watafidiwa?.
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,562
2,000
Ulikuwa ubabaishaji tu, nilikuwa Katavi huko, nyama polo ikawa inauzwa buchani tsh.12,000!! Wananchi wakawa wanalalamika kuwa ni aghali, wakajibiwa kuwa mnafikiria hizi ni nyama za ng'ombe? Kwanza haziwezi kuwa zinapatikana kila siku la sivyo wanyama wakakwisha wote!!!
Kifupi ni mizuka tu ya jiwe ndio ililianzisha hili kwa kusaidiana na Kigwangala
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
91,094
2,000
Ulikuwa ubabaishaji tu, nilikuwa katavi huko, nyama polo ikawa inauzwa buchani tsh.12, 000!!wananchi wakawa wanalalamika kuwa ni aghari, wakajibiwa kuwa mnafikiria hizi ni nyama za ng'ombe?kwanza haziwezi kuwa zinapatikana kila siku la sivyo wanyama wakatkwisha wote!!!
Kifupi ni mizuka tu ya jiwe ndio ililianzisha hili kwa kusaidiana na kigwangala
Jiwe bhana!
 
Just Distinctions

JF-Expert Member
May 5, 2016
1,120
2,000
Ulikuwa ubabaishaji tu, nilikuwa katavi huko, nyama polo ikawa inauzwa buchani tsh.12, 000!!wananchi wakawa wanalalamika kuwa ni aghari, wakajibiwa kuwa mnafikiria hizi ni nyama za ng'ombe?kwanza haziwezi kuwa zinapatikana kila siku la sivyo wanyama wakatkwisha wote!!!
Kifupi ni mizuka tu ya jiwe ndio ililianzisha hili kwa kusaidiana na kigwangala
Wakati anahutubia bunge alisema ulikuwa mpango ambao upo kwenye maandalizi, na alisisitiza kwa kusema wana mpango

Tofautisha na kitu ambacho kipo tayari, the same applies leo hii waseme wana mpango wa kutolipisha umeme afu we kesho uanze kuchemsha maharage kwenye jiko la umeme, itakula tu kwako.

Ila yote kwa yote, aliesimamia huo mpango hayupo tena.
 
Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,824
2,000
Hata hivyo ulaji sana wa nyama siyo mzuri. Serikali isikataze ndio lakini iongeze kodi hadi nyama kwa kilo iwe elfu 20 ili watu wasile sana nyama au kuacha kabisa.
 
nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
13,185
2,000
Wakati anahutubia bunge alisema ulikuwa mpango ambao upo kwenye maandalizi, na alisisitiza kwa kusema wana mpango

tofautisha na kitu ambacho kipo tayari, the same applies leo hii waseme wana mpango wa kutolipisha umeme afu we kesho uanze kuchemsha maharage kwenye jiko la umeme, itakula tu kwako.

ila yote kwa yote, aliesimamia huo mpango hayupo tena.
Unasemaje ulikuwa mpango wakati nyama tayari ilikuwa inauzwa mabuchani
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,562
2,000
Wakati anahutubia bunge alisema ulikuwa mpango ambao upo kwenye maandalizi, na alisisitiza kwa kusema wana mpango

tofautisha na kitu ambacho kipo tayari, the same applies leo hii waseme wana mpango wa kutolipisha umeme afu we kesho uanze kuchemsha maharage kwenye jiko la umeme, itakula tu kwako.

ila yote kwa yote, aliesimamia huo mpango hayupo tena.
Mbona huo mpango ulishaanza tayari? Tatizo hakukuwa na utaratibu mzur tu, nyama ilishaanzwa hadi kuuzwa mabuchani(KATAVI)
 
MtuloBM

JF-Expert Member
Feb 26, 2020
292
250
Wakati anahutubia bunge alisema ulikuwa mpango ambao upo kwenye maandalizi, na alisisitiza kwa kusema wana mpango

tofautisha na kitu ambacho kipo tayari, the same applies leo hii waseme wana mpango wa kutolipisha umeme afu we kesho uanze kuchemsha maharage kwenye jiko la umeme, itakula tu kwako.

ila yote kwa yote, aliesimamia huo mpango hayupo tena.

Ni ujinga tu wa msukuma
 
Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
2,439
2,000
Another braa braaa from wendawazimu politicians,
Hii Nchi viongozi wa CCM hawajawahi fanya kitu kikafaulu Kwa asilimia 💯 bila ukiritimba!
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,489
2,000
Nyati anauzwa laki sita!!? Kumbe bei yake ni chini ya bei ya ng'ombe?! Kwa mtazamo wangu, walioanzisha mpango huo hawakua sahihi
 
Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
861
1,000
Huyo rafiki ako alikuwa na fedha za kuchezea, yaani atumie 150M maandalizi ya butcher, alikuwa anajipanga kuwa jangili huyo.
Hata hivyo hii ishu ingekuja kuleta shida huko mbeleni, tuendelee kula nyama za wanyama wetu wa kufugwa na wanyamapori wale nyama zao, mnataka Simba waanze kula nyasi au watuvamie kwa uhaba wa swala?
 
42774277

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
5,265
2,000
Serikali ya Awamu ya Tano ilitoa utaratibu wa kuwezesha Watanzania kufungua mabucha ya wanyamapori mradi tu wawe wamefuata utaratibu. Hapa Mwanza kuna rafiki yangu alifuata taratibu zote na alianza kujenga bucha kwa gharama kubwa, alinunua gari ya kuwindia, alinunua bunduki ya aina yake kwa ajili ya kuwindia, alinunua mafriji kwa ajili ya kutunza nyama kutoka porini, alinunua mashine ya kukata nyama na vifaa vyote vinavyohitajika ili bucha yake ianze kazi. Pamoja na kutimiza masharti yote alipigwa dana dana mpaka Rais wa Awamu ya Tano akafariki. Juzi nilipomuuliza kulikoni majibu niliyopata kwake yanasikitisha sana licha ya hasara kubwa aliyoingia. Yeye alinieleza kuwa vile vitalu ambavyo walitakiwa kwenda kuwinda tayari vimeishagawiwa na Serikali na hivyo hakuna yeyote atakayekuruhusu kuwinda kwenye kitalu chake. Aliendelea kunieleza kuwa awali nyati mmoja alitakiwa kuuzwa na Serikali kwa Tshs.600,000 sasa wenye vitalu ukitaka kumnunua nyati mmoja ni Tshs.1m/-. Anasema amepata hasara zaidi ya Tshs.150m/-. Tuiulize Serikali huu mradi nini hatma yake na kwa wale waliopata hasara watafidiwa?.
Tunaooshauri nchi iingozwe kwa system inayoeleweka na si utashi wa mtu, huwa hatueleweki.

Ila huu ni mfano mmoja wapo
 
christeve88

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,374
2,000
Ulikuwa ubabaishaji tu, nilikuwa katavi huko, nyama polo ikawa inauzwa buchani tsh.12, 000!!wananchi wakawa wanalalamika kuwa ni aghari, wakajibiwa kuwa mnafikiria hizi ni nyama za ng'ombe?kwanza haziwezi kuwa zinapatikana kila siku la sivyo wanyama wakatkwisha wote!!!
Kifupi ni mizuka tu ya jiwe ndio ililianzisha hili kwa kusaidiana na kigwangala
Acha kumlaumu JPM wewe uwe na adabu inaonesha ni jinsi gani umejawa chuki na mtu aliyetaka kila mtanzania afaidi rasilimali za nchi yake.

Samaki na dagaa wanavuliea kila siku huko maziwani na mtoni uliwahi lusikia wamekwisha? hao wanyama pori wanaowindwa kila siku na kupelekwa huko ulaya na uarabuni uliwahi kusikia wamekwisha? au tukianza kula sisi ndio wataisha ila dagaa ziwa Victoria na Tanganyika hawawezi kwisha.

JPM alisema watu wafungue mabucha ya wanyama pori wakati huo huo watu wawekeze kwenye ufugaji wa wanyapori ilikupngeza idadi ya wanyama.

Ni vigumu mno JPM kueleweka na watu wenye fikra za ubinasfi na wasiongalia mbele. Kuna wakati nahisi kuwa waaferika hutukupewa uhuru kwenye rasimali zetu na wakoloni ndio maana maliasili kama madini na wanyama ni kama bado zipo mikononi mwao na watawala wetu wachache.
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
7,337
2,000
Hata hivyo ulaji sana wa nyama siyo mzuri. Serikali isikataze ndio lakini iongeze kodi hadi nyama kwa kilo iwe elfu 20 ili watu was ile sana nyama au kuacha kabisa.
Takwimu zinaonyesha tinakula nyama kiaai kidogo sana, binadamu anatakiwa ale nyama kg 50 kwa mwaka, wewe umekula kiasi gani ndugu?
 
Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
4,643
2,000
Acha kumlaumu JPM wewe uwe na adabu inaonesha ni jinsi gani umejawa chuki na mtu aliyetaka kila mtanzania afaidi rasilimali za nchi yake.

Samaki na dagaa wanavuliea kila siku huko maziwani na mtoni uliwahi lusikia wamekwisha? hao wanyama pori wanaowindwa kila siku na kupelekwa huko ulaya na uarabuni uliwahi kusikia wamekwisha? au tukianza kula sisi ndio wataisha ila dagaa ziwa Victoria na Tanganyika hawawezi kwisha.

JPM alisema watu wafungue mabucha ya wanyama pori wakati huo huo watu wawekeze kwenye ufugaji wa wanyapori ilikupngeza idadi ya wanyama.

Ni vigumu mno JPM kueleweka na watu wenye fikra za ubinasfi na wasiongalia mbele. Kuna wakati nahisi kuwa waaferika hutukupewa uhuru kwenye rasimali zetu na wakoloni ndio maana maliasili kama madini na wanyama ni kama bado zipo mikononi mwao na watawala wetu wachache.
Huwezi kumfuga mnyama pori kama unavyofuga Mbuzi, Kondoo or Ng'ombe! Atakufa kwa stress za kiikolojia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom