Kula kwa mkono

tofali

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
4,010
Reaction score
3,423
Jameni nauliza swali kuna ubaya kula kwa mkono..mfano umeenda hotel kubwa kubwa unakula chips na kuku au samaki...maana kutumia umma na kisu kukatia kuku mwenzenu naona napoteza mda halafu difaidi...naombeni ushauri ni kujiaibisha au naonekana mshamba kula kuku na samaki kwa hand...herhe
 
Hiyo ni hiyar yako mkuu..., unaweza kula kwa mkono au hata mguu...,na huo si utamadun wetu bali ni watu wa majuu..., usikirihishe nafsi yako kwa kuyataka makuu..., huo ni ulimbukeni kuigaiga kama ndege kasuku, ukakaa mezan ukaambulia patupu....!
 
Fanya kitu roho inapenda kaka usiangalie wengine wanafanyeje!! Binafsi siwezi kula samaki kwa uma au kijiko shurti nitumie mkono ndiyo mautamu nayafeel!!
 
ni vizuri ukala kwa namna unayoiweza na inayofaa ikiwa hizo zingine zinakupa kero. na wakati mwingine kuogopa kuaibika maana ulaji wa kisu na uma una utaalamu wake kwa kila chakula.
 

yaani wewe unaomba ushauri kwenye kula alaa vipi bana..
 
Hata kijiko, uma na kisu vinashikwa na mkono...huyo anayekuona mshamba mwambie ajaribu kutumia kiungo kingine...
 
Kula tu kwa mkono mwaya.........tena mbona burudani..!, mi mwenyewe mambo ya fork & knife siyawezi
 
Inategemea,kuna watu wanakuwa offended akikaa meza moja moja na mtu anayekula kwa mikono.
Angalia mazingara kisha ndo uamue mikono or no mikono. Mathalan uko kwenye interview unaomba kazi wakubwa wanakualika lunch unadhani itakuwaje mkuu kama kampuni ni ya watasha na wewe ndo unaomba uwe PR meneja wao?
 
Hata kijiko, uma na kisu vinashikwa na mkono...huyo anayekuona mshamba mwambie ajaribu kutumia kiungo kingine...
Ha ha ha ha, duh kweli vinashikwa kwa mkono.. kiswahili ni kigumu
 

eat more the slogan says.mi natwangwa tu kumla kuku kwa umma na kisu hata sifaidi hasa mifupa nitatafunaje? halafu samaki siwezi kumla kwa hotel shurti kuliwa home huku napunga upepo na kanga moja kichwa kinatafunwa kitakachoonekana ni mifupa tu tena ngoja niende kuwatafuta tii kiu yako
 
yaani wewe unaomba ushauri kwenye kula alaa vipi bana..

Ushauri muhimu ndugu...sasa ukute napo unakula pizza eti nitumie uma...hapana jameni...namwaga tomato yangu mkono uko wapi.....yummy yummy🙂
 
Umenena bana:thumbup:
 
Kula ni kula tu ilimradi unashiba ila ukila kwa Mguu sio vibaya lol Jr
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…