Kula kwa kutumia mkono wa kushoto kwa mtu mzima ni uchafu

Binafsi, mkono wa kulia nautumia Kula Na kuandika tu, kaz zngne nafanyia kushoto..

Nakushauri uige lyf style yang, coz wakat wa kumenya/kukata chakula nashkia kisu mkono wa kushoto..lakn kwa maoni yako ingebidi nishke kisu mkono wa kulia then chakula/tunda likae kwny mkono usioupenda Kama ufanyavyo ww..!
 
mimi ni mdau na mtumiaji mkubwa sana wa mkono wa kushoto acheni hizo bana! jamii imetutenga kwa kiasi kikubwa na sisi tumenyamaza na wala hatulalamiki kwa zaidi ya 70% ya vifaa au vitu vilivyopo kwenye soko havina upendeleo kwa mashoto kuanzia milango ya nyumba ,majokofu (japo langu ni la kushoto kutokana na fundi aliyeenda kununua na kumshauri wife alikuwa mashoto hivyo akajipigia pande kwenye mlango).
acheni hizo bana!
zipo sababu za kitaalamu kwa nini mtu anatumia kushoto na kwanini sio kulia na hili halianzii katika mkono ila ni kwenye akili kwa bahati mbaya nimesahau maelezo ya utetezi lakini kwa kuwa wataalamu wako hapa wanauwezo wa kutueleza vizuri zaidi!
wengi wanatuona watu wa mashoto tuna akili sana ni kweli kwa kuwa muda mwingi tunajifunza zaidi kutokana na mazingira kutubagua hivyo tunahitaji nguvu ya ziada kujua kufanya kwa maumbile yetu na kwa kufanya hivyo tunaongeza uwezo wetu wa kuelewa zaidi!
uwezo wa mikono yetu ya kulia haufanani na uwezo wa wanaotumia kulia kwa mkono wa kushoto hivyo wamepoteza fursa !
kila mwenye mkono wa kushoto hatumii nguvu nyingi kutumia kulia akiamua ukilinganisha na nyie wenye kulia kutumia kushoto!
acheni hizo bana!
Uko sahihi kwa kiasi kikubwa. Mwanangu pia ni "mashoto". Nisipoteze muda kuelezea vipaji vyake ila ni extra ordinary. Mashoto ni minority ambao mifumo mingi hasa ya vifaa imewasahau na bado wanabaguliwa na wanadamu wenzao. Nilipambana sana na walimu wake wa madarasa ya awali. Nikawaambia wakome kunilalamikia mtoto ana mwandiko mbaya badala yake wagugo jinsi ya kumsaidia mtoto anayeandikia kushoto. Wanasahau mfumo pekee unaom-favour mashoto ni wa kiarabu unaoanzia kulia kwenda kushoto. Mtoto anayeandikia kushoto hawezi kunyoosha mwandiko ghafla kwa sababu haoni anakoelekea. Walinielewa, wakaacha kumnyanyasa na sasa anaandika vizuri sana. Ndugu zangu waswahiliswahili nao sikuwavumilia kujidai wanamkunja samaki angali mbichi kwa kumlazimisha mtoto tena kwa maneno mabaya kutumia mkono wa kulia eti wa kushoto ni wa chooni!! Sijui wanaongelea choo kipi wakati matumizi ya mikono kwa mashoto ni kinyume cha watumia kulia.

Faida ya ziada ya mashoto ni kuwa tofauti na sisi wa kulia, mikono yao ya kulia huwa na nguvu relatively kubwa kuliko ya kwetu ya kushoto. Hivyo akiamua anaweza kufanya vitu vingi kwa mkono wa kulia. Mtoto wangu nilikuwa nikimwambia mbali na kusalimia na kupokea atumie mkono wa kulia kwa hiari yake na si kwa kushinikizwa na ajiamini ameumbwa kwa namna ya kipekee kwa utukufu wa Mungu.

Tuache unyanyapaa dhidi ya mashoto.
 
Jaribu kufanya utafiti kidogo mtu kama anatumia mkono wa kushoto maana yake mikono wa kulia uliozoea wewe ndiyo mikono wake wa kushoto.
 
hadi kuandikia mkono wa kushoto ni uchafu? hebu watake radhi mashoto wote duniani tafadhali
 
Kwa ufahamisho wako, mimi ni mashoto. Nilipokuwa Preparatory mwalimu wangu alinichapa sana, nilijaribu kuandikia kulia lakini mwandiko wangu wa kulia kama wa kuku. Wewe unajitawaza na kushoto, mimi natumia kulia, wewe unalia kulia mimi kushoto. Wewe unawaza kikulia lia mimi nawaza kushoto. Ingia Google angalia watu wanaotumia kushoto ni watu wa aina gani. We are unique and genius people. Tunajiamini na we are creative na wakarimu sana. Fanya utafiti halafu ulete mrejesho.

Mwalimu wa mtoto wangu naye aliamua kuchukua jukumu la kumbadilisha mtoto mkono wa kuandikia. Nisingekuwa mkali kwa mwalimu mtoto angepata shida sana. Mtoto anakosa hamu ya kwenda shule kwa sababu ya harassment ya mwalimu kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wake.
 
Am nearly sixty hivyo unaweza kujua stigma niliyopambana nayo tangu nakua. Mama yangu mzazi alikuwa akiniambia nitaolewa na nani mimi mashoto siendi deep sababu mama kafariki hivi majuzi. Mme wangu mpenzi anapenda jinsi ninavyotumia mikono yangu yote miwili na hasa nilivyomzalia watoto wenye uwezo wa kufikiri na kutenda. Yeye lia ila watoto wangu wote mashoto na wote ni graduates ila mmoja bado hajamaliza ila wote Scientists na madaktari plus mfanya biashara and they are doing good. Watu wana perceptions mbaya bila kujua kuwa kuna watu tumeumbwa tofauti. Je, mmenitenga mimi akija gay ambaye kazaliwa anavaa chupi za kike na msichana anayetaka ashinde na wavulana mtafanyaje? Mimi wa shoto naweza ku highlight jinsi binadamu tulivyoumbwa tofauti. Sisi tupo wachache duniani ila sisi ni lulu ya ulimwengu you need us for innovation. Unaambiwa most of Nasa personnel ni mashoto kama nadanganya labda google. Madaktari wengi wazuri ni mashoto na inabidi wawe na special assistnaces wakati wa surgeries sababu sisi mashoto hatujui vizuri left and right that is our problmes. Tunachanganya sababu tunaishi dunia tofauti.
 
Salaam wandugu.

Mungu anisamehe kwanza. Ila mm nikiona mtu anakula, kuandikia au kushika kitu kwa kutumia mkono wa kushoto,halafu ni mtu mzima, inakera sana.Inakuwaje wazazi huwaacha watoto wao kutawala mkono wa kushoto ile hali na mkono wa kulia upo.

Kiutamaduni, mkono wa kushoto hushika vitu najisi (vichafu) sana. Kuutumia huo mkono kula ni kama kula hivyo vitu.Kuna jamaa yangu nimemsema mpaka nimechoka, amachukuq tonge la ugali kwa mkono wa kushoto anabugia mdomoni kiroho safi

Kutumia mguu wa kushoto kuchezea mpira its okay.

Najiuliza tu, ni nn huwa kinatokea mpaka mtu anakuwa comfortable kula, kuandikia mkono wa kushoto ile hali mkono wa kulia upo kabisa?

Asubuhi njema.
Wewe km sio muislam sijui. Nyie ndio mnakuwaga na ujinga huo wa mtazamo
 
Mikono yote imeumbwa na Mungu!
Mama yetu Janeth wa JPM huwa namuona wakati mwingi anatumia mkono wa kushoto
 
Pole sana ndugu! Sisi wanawake tunatumia mikono yote kupikia, tunatoka zetu chooni..tunakupikia kwa mikono yote, tunaandaa matunda na kachumbari kwa mikono yote na unakula unafaidi. Utakuwa unalishwa mavi kila siku. Kua makini! Mkono ni mkono tu! Sisitiza usafi!
Pewa hela na mkono wa kushoto ukatae...
Dadangu ishu hapo ni kula kwa mkono wa kushoto na wala sio kupika kwa mkono wa kushoto,hata Yesu alisema ataketi na wanafunzi wake 12 mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu,hili ni suala zito sana lkn watu mnachukulia kisport sport tu,
 
Ubongo una right hemisphere na left hemisphere.right handed wanatumia left hemisphere na left handed wanatumia right hemisphere, na right hemisphere iko vzr sana kwenye psychomotor na cognitive domain ndomana left handed wengi ni wachawi wa namba na michezo
 
Am nearly sixty hivyo unaweza kujua stigma niliyopambana nayo tangu nakua. Mama yangu mzazi alikuwa akiniambia nitaolewa na nani mimi mashoto siendi deep sababu mama kafariki hivi majuzi. Mme wangu mpenzi anapenda jinsi ninavyotumia mikono yangu yote miwili na hasa nilivyomzalia watoto wenye uwezo wa kufikiri na kutenda. Yeye lia ila watoto wangu wote mashoto na wote ni graduates ila mmoja bado hajamaliza ila wote Scientists na madaktari plus mfanya biashara and they are doing good. Watu wana perceptions mbaya bila kujua kuwa kuna watu tumeumbwa tofauti. Je, mmenitenga mimi akija gay ambaye kazaliwa anavaa chupi za kike na msichana anayetaka ashinde na wavulana mtafanyaje? Mimi wa shoto naweza ku highlight jinsi binadamu tulivyoumbwa tofauti. Sisi tupo wachache duniani ila sisi ni lulu ya ulimwengu you need us for innovation. Unaambiwa most of Nasa personnel ni mashoto kama nadanganya labda google. Madaktari wengi wazuri ni mashoto na inabidi wawe na special assistnaces wakati wa surgeries sababu sisi mashoto hatujui vizuri left and right that is our problmes. Tunachanganya sababu tunaishi dunia tofauti.

Wow! kumbe wewe ni wa long time hivi! Watoto wangu wawili ni left handed hawajafikisha miaka kumi. Nikajiuliza miaka hii nani hajui kutumia mkono wa kushoto ni kitu cha kawaida? Mwalimu especially, badala ya kumjengea mtoto kujiamini anamvunja moyo kumfanya ajione ana mapungufu wakati mtoto hana shida hata kidogo.
 
Salaam wandugu.

Mungu anisamehe kwanza. Ila mm nikiona mtu anakula, kuandikia au kushika kitu kwa kutumia mkono wa kushoto,halafu ni mtu mzima, inakera sana.Inakuwaje wazazi huwaacha watoto wao kutawala mkono wa kushoto ile hali na mkono wa kulia upo.

Kiutamaduni, mkono wa kushoto hushika vitu najisi (vichafu) sana. Kuutumia huo mkono kula ni kama kula hivyo vitu.Kuna jamaa yangu nimemsema mpaka nimechoka, amachukuq tonge la ugali kwa mkono wa kushoto anabugia mdomoni kiroho safi

Kutumia mguu wa kushoto kuchezea mpira its okay.

Najiuliza tu, ni nn huwa kinatokea mpaka mtu anakuwa comfortable kula, kuandikia mkono wa kushoto ile hali mkono wa kulia upo kabisa?

Asubuhi njema.
Eti Wanaiga Wazungu aibu kweli kweli mkono unao chamb** chooni ndo unalia chakula Aibu jamani badilikeni hakuna kujitia eti mm nmezaliwa mashoto!!!
 
Wow! kumbe wewe ni wa long time hivi! Watoto wangu wawili ni left handed hawajafikisha miaka kumi. Nikajiuliza miaka hii nani hajui kutumia mkono wa kushoto ni kitu cha kawaida? Mwalimu especially, badala ya kumjengea mtoto kujiamini anamvunja moyo kumfanya ajione ana mapungufu wakati mtoto hana shida hata kidogo.
Wape moyo na waambie they are the best hivyo waendelee hivyo. Kutumia kushoto kuna advantage nyingi sisi tunaweza tumia hata mkono wa kulia ikibidi ila ikibidi sababu we are not keen on that. Ila tupo fexible hivyo waambie wanaweza hata kutumia mkono wa kulia kubeba vitu. Mimi vitu vizito nabeba na mkono wa kulia ila when it comes for executing things kulia inakaa kando.. Keyboard natumia mikono yote sababu nimesomea kutumia keyboard kama typing tool na nimeweza kufanikiwa kwa hilo. other wise kisu hakiwezi guswa na mkono wa kulia hivyo nawashangaa wanaochukia sisi wakati tunapopika chakula chote tunakishika na mkono wa kulia sababu kisu, umma, mwiko ni mkonokushoto lakini chakula ni kulia. hao mnaowaamini wanatumia kushoto kushika chakula na ulia kukata amua leo na chukua hatua.
 
sio kosa lako bali wazungu ukisoma bible utakuta eti Yesu ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na shetani yupo mkono wa kushoto
 
Pole sana ndugu! Sisi wanawake tunatumia mikono yote kupikia, tunatoka zetu chooni..tunakupikia kwa mikono yote, tunaandaa matunda na kachumbari kwa mikono yote na unakula unafaidi. Utakuwa unalishwa mavi kila siku. Kua makini! Mkono ni mkono tu! Sisitiza usafi!
Pewa hela na mkono wa kushoto ukatae...
 
Hebu tuambie unapokunywa chai na mkate au andazi, hutumii mkono wa kushoto kwa namna yoyote ile?? Unapokatakata kachumbari mkono wa kushoto huwa umeshika nini??
 
Dah aiseee.., hivi kwani kabla ya kula hata kama ni mkono wa kushoto huwa hunawi kwa sabuni?!
 
emancipate yourself from mental slavery...no one but ourselves can free our minds..

Quoted from the late Great Bob Marley
 
huu utamaduni wa kutokula na mashoto uko afrika tuu, india china hawana haya mambo. ni ubaguz wa hali ya juu wa kiungo cha mwil kilichoumbwa na Mungu.
Kwelk mkuu, na kuna baadhi ya nchi za ulaya kila kitu ni mashoto.., kuanzia wananchi wao % kubwa kuwa ni mashoto, kuendesha magari yenye usukani upande wa kushoto na barabara unapita kushoto pia.
Sie tumeng'ang'ana kuutia najisi mkono wa kushoto!!
 
Najiuliza tu, ni nn huwa
kinatokea mpaka mtu
anakuwa comfortable
kula, kuandikia mkono wa
KULIA ilhali mkono wa
KUSHOTO upo kabisa
 
Back
Top Bottom