Kula kwa kutumia mkono wa kushoto kwa mtu mzima ni uchafu

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
720
Salaam wandugu.

Mungu anisamehe kwanza. Ila mm nikiona mtu anakula, kuandikia au kushika kitu kwa kutumia mkono wa kushoto,halafu ni mtu mzima, inakera sana.Inakuwaje wazazi huwaacha watoto wao kutawala mkono wa kushoto ile hali na mkono wa kulia upo.

Kiutamaduni, mkono wa kushoto hushika vitu najisi (vichafu) sana. Kuutumia huo mkono kula ni kama kula hivyo vitu.Kuna jamaa yangu nimemsema mpaka nimechoka, amachukuq tonge la ugali kwa mkono wa kushoto anabugia mdomoni kiroho safi

Kutumia mguu wa kushoto kuchezea mpira its okay.

Najiuliza tu, ni nn huwa kinatokea mpaka mtu anakuwa comfortable kula, kuandikia mkono wa kushoto ile hali mkono wa kulia upo kabisa?

Asubuhi njema.
 
Mkono wa kushoto hauna shida kwa kufanyia kazi zingine,

kwa sababu ndo unakuwa na Nguvu kuliko wa kulia kwa wale left handed,

ila linapofika suala la kula dah hapana kwa kweli mkono wa kulia utumike tu,

binafsi siwezi kula hata kama nitaweza nitapata shida sana kuwa karibu na mtu anayelia mkono wa kushoto
 
Mungu aliumba kila kitu safi, binadamu tukavifanya vingine vionekane najisi...
Nini kinakufanya uone kutumia mkono wa kushoto ni uchafu? au kwa sababu hutumika kujisafishia sehemu ya haja kubwa?
 
Pole sana ndugu! Sisi wanawake tunatumia mikono yote kupikia, tunatoka zetu chooni..tunakupikia kwa mikono yote, tunaandaa matunda na kachumbari kwa mikono yote na unakula unafaidi. Utakuwa unalishwa mavi kila siku. Kua makini! Mkono ni mkono tu! Sisitiza usafi!
Pewa hela na mkono wa kushoto ukatae...
 
Mkono wa kushoto hauna shida kwa kufanyia kazi zingine,

kwa sababu ndo unakuwa na Nguvu kuliko wa kulia kwa wale left handed,

ila linapofika suala la kula dah hapana kwa kweli mkono wa kulia utumike tu,

binafsi siwezi kula hata kama nitaweza nitapata shida sana kuwa karibu na mtu anayelia mkono wa kushoto
To me, hii ni perception yako tu.... Je wanaokula kwa miguu..!?
 
Yeah ni perceptio yangu kweli sijisikii vizuri kula na mtu anatumia kushoto,

wakati tupo wadogo ndugu yetu mmoja alikuwa mlemavu wa miguu some how na mikono so alikuwa anatumia kushoto wakatim wa kula nilikuwa napata shida sana nikienda kuwatembelea hata yeye akija home,

Nakubali wengine hawaoni tatzo yeah sawa ila kwangu mimi napata shida sana naweza hata kurudisha
 
Siku ukiumia mkono wa kulia ukashindwa kufanya kazi hutakula? Au utataka ulishwe?
 
Yeah ni perceptio yangu kweli sijisikii vizuri kula na mtu anatumia kushoto,

wakati tupo wadogo ndugu yetu mmoja alikuwa mlemavu wa miguu some how na mikono so alikuwa anatumia kushoto wakatim wa kula nilikuwa napata shida sana nikienda kuwatembelea hata yeye akija home,

Nakubali wengine hawaoni tatzo yeah sawa ila kwangu mimi napata shida sana naweza hata kurudisha
Pole sana. Mimi ukila kama mbwa ndio itakuwa shida.
 
Wale ambao ni left handed wakienda chooni wanatumia mkono wa kuume kujiswafi, hivyo ondoa mawazo yako kuwa wanatumia mkono wa kushoto kushika najisi. Mtu anapaswa kuandika kwa kutumia mkono wake ulio na nguvu na sio kumlazimisha atumie mkono ambao atapata shida katika kuifunza.

Kwa taarifa yako nchini India siku hizi wanawafundisha watoto kuanzia chekechea kutumia mikono yote miwili na wamefanikiwa sana.
 
Salaam wandugu.

Mungu anisamehe kwanza. Ila mm nikiona mtu anakula, kuandikia au kushika kitu kwa kutumia mkono wa kushoto,halafu ni mtu mzima, inakera sana.Inakuwaje wazazi huwaacha watoto wao kutawala mkono wa kushoto ile hali na mkono wa kulia upo.

Kiutamaduni, mkono wa kushoto hushika vitu najisi (vichafu) sana. Kuutumia huo mkono kula ni kama kula hivyo vitu.Kuna jamaa yangu nimemsema mpaka nimechoka, amachukuq tonge la ugali kwa mkono wa kushoto anabugia mdomoni kiroho safi

Kutumia mguu wa kushoto kuchezea mpira its okay.

Najiuliza tu, ni nn huwa kinatokea mpaka mtu anakuwa comfortable kula, kuandikia mkono wa kushoto ile hali mkono wa kulia upo kabisa?

Asubuhi njema.
Ni uchafu kwako na familia yako ila kwa Mungu kila mkono una karama, kuna mkono wa afya, utajiri, uzima, afya. Pole yako kama ni mkristo soma faida ya mikono
 
Pole sana ndugu! Sisi wanawake tunatumia mikono yote kupikia, tunatoka zetu chooni..tunakupikia kwa mikono yote, tunaandaa matunda na kachumbari kwa mikono yote na unakula unafaidi. Utakuwa unalishwa mavi kila siku. Kua makini! Mkono ni mkono tu! Sisitiza usafi!
Pewa hela na mkono wa kushoto ukatae...

hata yeye siku akitaka kupika hutumia mikono yote kumenya matunda hutumia mikono yote, hivyohivyo wakati wa kulikata vipande
 
Back
Top Bottom