Kukuza Uchumi wa Nchi na Watu

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,038
3,479
Wakuu,

Kama mmojawapo wa raia mjenzi wa nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) ambayo ni zao la Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Zanzibar

Uchumi nufaishi kwa nchi na watu
A:
1. Uchumi wa mazao ya Bahari
2. Uchumi wa Utalii (mali kale, viumbe adimu, wanyama asili lugha, utamaduni)
3. Uchumi wa mazao ya viungo
4. Uchumi wa usafirishaji kwa njia ya Maji, Anga na Bandari
5. Uchumi wa historia ya Visiwa vya Zanzibar (Unguja, Pemba, Tumbatu, Uzi, Vundwe, Bawe, Changuu, Fundo, Chumbe nk)
6. Uchumi Huduma (Usafiri, hoteli, mawasiliano, usafi wa mazingira nk)

B:
1. Uchumi Kilimo mazao chakula (kwa kuongezwa thamani tangu shambani hadi kwenye hatua kabla ya mlaji
2. Uchumi mazao Biashara (ubora na thamani kwa kulingana na soko ikizingatiwa kwa manufaa yenye tija)
3. Uchumi Utalii (Mali kale, viumbe adimu, wanyama pori asili, mbuga za mimea na uwanda asili, lugha, utamaduni)
4. Uchumi Madini (Gold, Copper,, Silver, Diamond, Tanzanite, Coal, Iron ore Tin, Aluminium, Uranium, Helium, Uranium, Soda Ash, Salt, Platinum, more gemstones of different species)
5. Uchumi Usafirishaji bidhaa ndani na nje ya nchi (barabara, reli, meli majini, na ndege angani
6. Uchumi Ufugaji mazao ya wanyama, Samaki nk
7. Uchumi huduma (Usafiri, Hoteli, Usafi wa mazingira, utunzaji mizigo, ulinzi binafsi nk)
8. Uchumi wa mazao ya Bahari. maziwa na mito
9. Uchumi ujenzi miundo mbinu bora, toshelezi na gharama nafuu
10. Uchmi wa Nishati (Umeme, Gesi, Upepo, Jua na Joto Ardhi)
11. Uchumi Bidhaa za Viwanda vya ndani ya nchi
12. Biashara za kati na kubwa kwa kodi rafiki isiyoua mtaji na ukuaji wake kwa ajili ya faida kwa maendeleo ya mmiliki, mtu mmoja mmoja na nchi pia
13. Uchumi wa habari na mawasiliano ijapokuwa kuna tishio la udukuzi siri na mashambulizi kwa njia ya mitandao
14. Uchumi sanaa, mziki na michezo
15. Kulinda uchumi kwa kuwekeza kwa nia ya kujitegemea kufanya maamuzi yenye maslahi ya nchi na kupanga matumizi ya mapato kwa maendeleo ya taifa bila masharti ya udhalilishaji.

Kwa maana hiyo serikali pamoja na watendaji wake, wajasiriliamali, wakulima, wafugaji,, wavuvi, wafanyabiashara, wafanyakazi na makampuni binafsi wajikite kwenye maeneo tahwa hapo juu kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na desturi tulizojiwekea ni imani yangu nchi na mtu mmoja mmoja watanufaika na mpango huo kwa kufanya kazi kwa bidii na kupata malipo stahiki yenye kukidhi mahitaji muhimu pamoja na kujiendeleza kimaisha kama familia au nchi yenye kujitegemea.

Mada iko mezani wenye fikra pevu.
 
Ujenzi wa miundombinu yote ya maana wamepewa wanajeshi na wachina,mtu wa Undendeule hata afanye nini hapewi.

Umewahi kusikia yale makampuni makubwa ya ujenzi ya wazawa yakipewa tenda yoyote awamu hii?

Labda yule mume mwenza anayejenga uwanja wa Chato.
 
Nimeshindwa kuelewa hii ni mada gani, na hizo A&B umezitenga kwanini. Kwani ukilewa lazima uanzishe mada?
 
Hamna kipya ulichoorodhesha hapo kati ya "A" na "B" ambavyo havifanywi na mtanzania mmoja mmoja, mambo ya kilimo, uvuvi, uchimbaji madini na mengine yote yanafanywa.

Ulichotakiwa kuonesha ni kwa jinsi gani hivyo vitu tajwa hapo juu vinaweza kufanywa kwa ufanisi ili kumnufaisha muhusika afurahie matunda ya kazi yake.

Watanzania hasa maeneo ya vijijini wanahitaji mitaji, mbolea, vifaa vya uchimbaji hasa madini, masoko ya uhakika ya mazao yao, wapate matrekta angalau kwa vikundi waachane na jembe la mkono, na vitu vingine kama hivyo.

Serikali ikiweza kufanya hayo nina hakika itakuwa imesaidia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hapa nchini, jinsi ya kufanikisha hayo serikali ihakikishe inapunguza matumizi makubwa ya pesa yasiyo ya lazima mf. malipo ya wabunge, ili kiasi kitakachopatikana kielekezwe kwenye kuboresha shughuli za kiuchumi za mtanzania.
 
Mkuu mada yako ni fikirishi mno, ijapokuwa inahitaji tafakuri na ithibati za kiuchumi zaidi. Umefanya vyema kuainisha maeneo ya kimkakati ambayo yanaweza kuchochea mabadiliko chanya yenye muelekeo zaidi wa sera za kifedha.

Vichocheo vya kiuchumi yaani "stimulus packages" zinaweza kutumika kama njia ya majaribio ya kutaka kutumia sera ya kifedha (i.e. monetary policy) ktk kuchochea uchumi ikiwa kama njia ya kipekee, muhimu na yenye tija ya kuweza kuinusuru serikali kwa hivi sasa.

Serikali imeamua kukumbatia "fiscal policy" peke yake kwa kuwa naweza kusema haioni umuhimu wa sekta binafsi. BoT ni lazima ichukue na kisimama ktk sehemu yake ili iweze kuishauri vyema serikali. Wataalamu wa mambo ya fedha wanapaswa kuishauri serikali yetu vyema kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote toka awamu ya tano ilipoingia madarakani.
 
Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
Mkuu mbenge

Unashauri wako uliojazia kwenye hii mada ni wa muhimu mno mawazo yako ni ya ujenzi makini natarajia mamlaka husika watauchukua kuboresha palipopungua.

Hii mada haikuleta kama mawazo mbadala ya moja kwa moja ila ni mchokoo kwa wazalendo halisi kuchangia ili kila mmoja kwa kadri anavyoweza asaidie kusonga mbele kwa pamoja. Asante JF members
 
Nimeshindwa clueless hii ni mada gani, na hizo A&B umezitenga kwanini. Kwani ukilewa lazima uanzishe mada?

Mkuu,

Kama huna cha maana cha kuchangia kuboresha mawazo ni bora ungekaa kimya kuliko kuwa raibu wa ukosoaji kwa kila kitu mpaka kile kinachokufurahisha mtima wako tu. Wewe siasa za mkumbo zimekuharibu. We do not talk politics on this agenda rather we are pooling in constructive ideas on how to collectively participate in improving country, enterprise and individual economy iamid the challenging hurdles.
 
Mkuu ukitaka kujua huna jipya uliloleta hapa, angalia mpaka sasa ni watu wangapi wamechangia mpaka leo. Post yako imetazamwa na watu 180+, lakini ukitoa post zangu na zako, nyingine hazizidi 7. Jitafakari ni nini umeleta hapa.
 
Ujenzi wa miundombinu yote ya maana wamepewa wanajeshi na wachina,mtu wa Undendeule hata afanye nini hapewi.

Umewahi kusikia yale makampuni makubwa ya ujenzi ya wazawa yakipewa tenda yoyote awamu hii?

Labda yule mume mwenza anayejenga uwanja wa Chato.
Wanajeshi ujira wao ni ugali maharage wanajitolea kwa uzalendo
 
Mkuu ukitaka kujua huna jipya uliloleta hapa, angalia mpaka sasa ni watu wangapi wamechangia mpaka leo. Post yako imetazamwa na watu 180+, lakini ukitoa post zangu na zako, nyingine hazizidi 7. Jitafakari ni nini umeleta hapa.
Wewe inawezekana hata unapopumua unajipinga kwanini unapumua ni hasara tupu; kwani ukiona watu wengi wamechangia hata bila mawazo tatuzi wewe unajiona umetoa wazo la maana kumbe wanakudharau. Wachache hata mmoja pekee mwenye mawazo ujenzi huyo ndio amewekeza kwa tija sio wewe debe tupu la maneno yasiyo na maana yoyote ile. Kila ukiwaza ni siasa uchwara ambazo zimekulevya hadi kuwa raibu na mtumwa wa pinga pinga na kosoa kosoa iliyojaa chuki binafsi kutokana na kuzibiwa mirija fisidi. Waachie intellectuals wachangia wewe kaa kimya tafadhali kuliko kujifanya mjuaji kwa kila kitu.
 
Mkuu mada yako ni fikirishi mno, ijapokuwa inahitaji tafakuri na ithibati za kiuchumi zaidi. Umefanya vyema kuainisha maeneo ya kimkakati ambayo yanaweza kuchochea mabadiliko chanya yenye muelekeo zaidi wa sera za kifedha.

Vichocheo vya kiuchumi yaani "stimulus packages" zinaweza kutumika kama njia ya majaribio ya kutaka kutumia sera ya kifedha (i.e. monetary policy) ktk kuchochea uchumi ikiwa kama njia ya kipekee, muhimu na yenye tija ya kuweza kuinusuru serikali kwa hivi sasa.

Serikali imeamua kukumbatia "fiscal policy" peke yake kwa kuwa naweza kusema haioni umuhimu wa sekta binafsi. BoT ni lazima ichukue na kisimama ktk sehemu yake ili iweze kuishauri vyema serikali. Wataalamu wa mambo ya fedha wanapaswa kuishauri serikali yetu vyema kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote toka awamu ya tano ilipoingia madarakani.
Badala ya stimulus sisi tumeamua kuvinyonya vivyo vilivyohitaji huo usaidizi na vingine kuhakikisha tunavizonga hats vijifie ama vifilisike.
 
Wewe inawezekana hata unapopumua unajipinga kwanini unapumua ni hasara tupu; kwani ukiona watu wengi wamechangia hata bila mawazo tatuzi wewe unajiona umetoa wazo la maana kumbe wanakudharau. Wachache hata mmoja pekee mwenye mawazo ujenzi huyo ndio amewekeza kwa tija sio wewe debe tupu la maneno yasiyo na maana yoyote ile. Kila ukiwaza ni siasa uchwara ambazo zimekulevya hadi kuwa raibu na mtumwa wa pinga pinga na kosoa kosoa iliyojaa chuki binafsi kutokana na kuzibiwa mirija fisidi. Waachie intellectuals wachangia wewe kaa kimya tafadhali kuliko kujifanya mjuaji kwa kila kitu.

Nilijua lazima utapanick, sio ww peke yako. Wako wenzako mpaka kuingia humu ndani hawataki, maana wamezoea kuja na mawazo ya kuburuza. Huku ndani utafurahi na taratibu utazoea. Hili ni jukwaa la kisiasa, huenda umeingia humu bila kujua maudhui ya huku ni ya kisiasa. Nahisi ww ni mzee, au kijana mshamba ndio maana hujui mijadala ya kwenye jukwaa la siasa inajadiliwa kisiasa.
 
Rubbish..................
 
Nikae sawa na umaamuma huo, hiki sio kichwa maji kama cha kwako usiyejielewa; it is you who will end up into stomach rush and diminish in thin air.

Www

Huku umeingia kwenye uwanja mpana, hicho unachokieelewa, humu ni kidogo sana. Humu kuna kila Eli kuanzia ya darasani, ya mtaani na kuzunguka dunia. Jitahidi tu usipanick ndio utapaeweza humu. Humu ndani kitakachokubeba sio ukubwa wa elimu yako, wala wingi wa hoja bali uvumilivu. Na sisi watu tunaojua kuwaprovoke vilaza mnaopanick wa aina yako huwa tunawapiga bao asubuhi na mapema.
 
Back
Top Bottom