Kukuru kakara za maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukuru kakara za maisha

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kitalolo, Jun 28, 2012.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kabla sijaoa nilikuta na msichana mmoja ambaye tulianza mahusiano na kabla hatujajuana vizuri, namaanisha kabla hatuaelezena historia zetu za maisha ikiwa kuna mmoja kati yetu ni mwana ndoa au ana mtoto tulijikuta tukipeana mapenzi moto moto. nilijikuta nikimpenda sana na kufikiri kuwa nimepata mwanamke wa maisha yangu. Siku moja baada ya kuwa naye nyumbani kwangu na kama kawaida mapenzi, aliondoka, na baadae nilipigiwa simu na mtu nisiyemfahamu akinitaka niache uhusiano na mke wake.

  Duh nilistuka sana maana kwa muda wote nikiwa naye sikuwahi kumuuliza ikiwa ana uhusiano na mtu mwingine na kibaya zaidi kumbe ni mke wa mtu na ana watoto wawili na mumewe huyo.

  Kesho yake asubuhi nilipigiwa simu na huyu mwanamke na kwanza nilistuka na kusita kuipokea haswa ikizingatia kuwa jana yake jioni nilikwishapokea simu ya vitisho, siku nzima sikuwa na raha maana kwanza nilikuwa najiuliza ikiwa yule kweli ni mke wa ntu kwanini alinificha hadi nimekwishazama katika mapenzi naye, pili na ambacho ni kibaya zaidi sikuwa napenda kuishi bila amani yaani kwamba natembea na mke wa mtu na mwenye mke anaweza wakati wowote ikiwa anatanifahamu basi maswala ya uhasama na kumwagiwa tindi kali niliona kuwa ni hatari kwa maisha yangu na sasa ningeshindwa kuwa huru mjini na kufanya shughuli zangu.

  Baadae niliamua kumpigia simu yule mwanamke na kupata ukweli ili niweze kufanya maamuzi magumu.
  Aliipokea ile simu huku akilia kwa maumivu na kunitaka niende kumsalimi hospitali Muhumbili kwa kipigo alichokipta kutoka ka bwana yake huyo.
  Niliiona hatari nyinhgine katika maisha yangu kuwa sasa swala hili limefikia kwenye mikono ya sheria kwani ikiwa alimuumiza na sijui amemuumiza kwa kiasi gani na iwapo ingemgharimu maisha yake pengine ningekuwa mtuhumiwa nambari wani. Nilipoteza amani kweli kwani sababu ya mimi kufahamika kwa huyo mwanamke ilikuwa ni mawasiliana ya simu kwa kupiga pamoja na sms nyingi za mapenzi na ahadi za kukutana na sehemu za kukutamnia tulizokuwa tukipanga kwani nilikuwa nikimpeleka nyumbani na kuna sms nilizomwagiza jinsi ya kufika kwangu hivyo ilikuwa rahisi sana mimi kupatikana.

  Ilinibidi nikate mawasiliano kwa muda kwani ilikuwa kama nimechanganyikiwa, ilinichukua muda sana kuja kujaribu kuipiga tena namba hiyo na haikuwa ikipatika kabisa, nilijaribu kumfwata mahali alipokuwa anafanyia kazi sikumkuta na nilipouliza majirani walikuwa wakifanya naye kazi walisema hawana taarifa zake. huo ukawa mwisho wa mimi na yeye kuwasiliana.

  Ilipita miaka kadhaa nikiwa nimehamia mkoa mwingine, ndipo siku moja kurejea Dar. nikiwa nakatiza mitaa ya Samora nilimwona yule mwanamke.Nilipomwona kwanza sikuamini maana sikuwa nimejua hatima ya kile kipigo na leo kumwona akiwa mzima wa afya na amezidi kuwa mrembo duh sikuamini macho yangu kweli nilianza kuongea naye huku nikiwa na uoga ndani mwangu.
  Story nyingi sana nikimlaumu kwanini hakuniambia kuwa ni mke wa mtu majibu yake yaliiacha hoi, eti kwamba yule sio mume wake ili alikuwa boy friend wake na walikuwa wameacha muda mrefu sana na kwamba huyo mwanaume bado anamfwatili akitaka warudiane ila yeye amemkatalia kabisa sasa siku hiyo alikuja nyumbani kwake na kuchukua simu yake na alipokuta sms zangu za mapenzi alikasirika sana ndipo wakaanza ugomvi akimwambia kuwa anakataa kumrudia kwakuwa anamtu mwenye kumpa kiburi amabaye ni mimi ndio ilipelekea kupokea kipigo cha mbwa mwizi na huyo mwanaume akaishia zake.
  Basi kwavile ilikuwa asubuhi tulipeana namba za simu na tulikubaliana kila mtu aendelee na kazi zake na tukutane baada ya kazi ili tuweze kuongea mengi.
  Jioni yake tulikutana alichokuwa akisisitiza yule dada ni kwamba niachane na yule **** alinieleza tena story nyingi kuhusu huyu mwanaume kitu nilichokuja kugundua baadae ilikuwa uongo kumbe bado anaishi naye na wana watoto wawili.
  basi jioni hiyo kama kawaida tukapeana pole kwa mapenzi motomoto. Na mimi kesho yake ilikuwa nisafiri kurudi Mkoa niliohamia kwa ahadi ya kuendelea na mipango ya kuoana.

  Kitu nilichiokuja kugundua baadaye ni kuwa huyu mwanamke alikuwa mwongo sana kumbe bado anaishi na huyo mwanaume na wanawatoto wawili ambao wanaishi kwa wazazi wake mkoani mwingine.
  Niliamua kuachanana naye na kuendela na maisha yangu ingawa nilikuwa nampenda sana hata mpaka sasa bado nampenda, ila nilijua sitaweza kuwa naye hivyo nilitafuta mke mwanamke mwingine na kuoana naye.

  Kweli nimemwacha ila wakati mwingine huwa nakumbuka huko nilikopitia naona ni maisha yenye raha na karaha.
   
 2. k

  kisukari JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  maelezo yako utafikiri ni hadithi.fundisho ni kuwa,wanawake nao wapo wenye mapenzi ya kichina,na usikurupuke tu kimapenzi,hata kama unampenda mtu,usiwe weak,kwani weakness nako,hiyo hiyo ndio ita ku cost.siku utakayomuona tena,jifanye kama humjui kabisa,you never know kwa uwongo wake huo,pengine anawapata wengi tu
   
 3. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mamaa sio hadithi.

  Asante kwa kuhitimisha pia kwa ushauri
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  duh. . .
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Una moyo mkuu kitalolo maana pamoja na onyo la kwanza bado umerudiana nae na kuendelea na mapenzi
  Licha ya kuambiwa ana mume na watoto wawili
  duh haya mambo haya ya mapenzi ni magumu sana aise
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Ukikutana naye tena atakwambia ameachana na yule mume wake na kwamba umsamehe kwa yote aliyokukosea..Na wewe utaamini na kuanza tena upya mapenzi...........
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  platozoom kweli kabisa akikutana nae tena atakuja na the same story twisted kiduchu
  atasema yule bwana amepata uhamisho ameenda mbali kabisa hata sijawahi kuwasiliana nae na kitalolo ataamini huo ujumbe na kuanza tena upya
  hata kama ni kufunga ndoa watafunga licha ya kwamba kashaambiwa ana watoto wawili
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...