Kuku wangu wanakufa msaada tafadhali

Papizo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
4,944
1,431
Wakuu hapa kati nilikuja na uzi wa kusema natafuta kuku wa kienyeji wasiochanjwaa....

Niliweza kufanikiwa kununua kuku sehemu tofauti na wengine nilipata kutoka mbeya ila walivyofika nikawachanganya bila kuwapa chanjo wala dawa zaidi ya alovera

Now kuku wanakufa vibaya sanaa wanamafua na nilikuwa kama na kuku 50 mpaka sasa wamekufa 9 na nimewapa kila aina ya dawa zaidi napigiwa simu naambiwa kuku hawali wanazidi kuzoofika kila siku naomba msaaada wenu tafadhali..

Msaada wenu wa haraka tafadhali...
 
Unapigiwa simu mkuu ?? Jiandae kupoteza banda zima

Mkuu wengine sio muda wote tupo karibu so inakuwa mtihani saa zingine kufatilia si unajuwa tena hali ilivyo kimaisha
 
Jaribu kuwa tenganisha wale wanao dhoofu na walio vizuri, then watafutie antibiotics kama vile Amplollium 20% au CDC, uwe unawachanganyia kwenye Maji kwa mda wa Siku 7-14 wote, wale waliodhoofu sana jaribu kuwapa antibiotics za binadamu( fragile) kwa kuwa nywesha nusu kidonge au kidonge kizima kulingana na ukubwa wa kuku
 
Pole mpambanaji!!!!!
Ugonjwa ukiingia kwa kuku huwa unabakisha mmoja tu wa kuja kuwasimulia wengine utakaowaleta.
Jitahidi kuwa na rekodi ya tarehe unayowachanja na ile utakayowachanja tena.
Chanjo muhimu ziko tatu, kideri, ndui na gombolo.
Zingine xipo pia usisahau antibiotics utakazoshauriea na wataalamu wa mifugo.

Usikate tamaa
There's no easy task
 
Gombolo inatibu nini
 
Acha telephone farming,hakikisha umeshuhudia mizoga au ht hao kuku wanapoumwa na sio kuambiwa na mfanyakazi.

Watenge wagonjwa,wape antibiotic kwanza,homa ikipungua wape chanjo husika.

Zingatia usafi wa banda na next time nunua vifaranga cuz ni rahisi kufuatilia malezi kuliko kuku wakubwa.
 
Pole mpambanaji!!!!!
Ugonjwa ukiingia kwa kuku huwa unabakisha mmoja tu wa kuja kuwasimulia wengine utakaowaleta.
Jitahidi kuwa na rekodi ya tarehe unayowachanja na ile utakayowachanja tena.
Chanjo muhimu ziko tatu, kideri, ndui na gombolo.
Zingine xipo pia usisahau antibiotics utakazoshauriea na wataalamu wa mifugo.

Usikate tamaa
There's no easy task
nimecheka sana hahahhahaha eti anabaki mmoja wa kuwasimulia kizazi kijacho.
 
Kinyesi ni cha kijani chenyewe....na wanaahusha mabawa
kwa dalili hizo huo ni ugonjwa wa kideri ambao kuku wakiwa na vimelea vya hao virus kupona ni nadra sana.hivyo jaribu kuwapa pilipili kichaa huwa inasaidia,na kama hawakupewa chanjo basi huenda wakabaki waliochanjwa pekee.
 
Back
Top Bottom