Kuna kuku ambao wao wakitaga mayai, huyatoboa na kuyafyonza wenyewe. Kuku hao, huatamia majivu au majani na kutotoa hewa.
Kuku hawa, huwafanya wafugaji kuwa makini sana pale wanapoona kuku hawa wanaingia bandani kwenda kutaga. Lengo la kuwa makini ni kwenda kuokota mayai pindi tu kuku wamalizapo kutaga. Maana ukichelewa kidogo tu, unakuta ameshalipasua tayari kwaajiri ya kufyonza.
Je, tuendelee kuwa makini kusubiri kuku watage ili tuokote mayai tuyaweke sehemu salama yawe mengi na kuku wakianza kuatamia tuyarudishe wayaatimie ili huko mbele tukapate vifaranga wengi?
Au tuwaache kuku watage na wafyonze mayai waliyoyataga ili baadae waje kuatamania majivu?