Kukosekana kwa upinzani nchini ni sawa na mwili kukosa kinga za mwili

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Kinga za mwili ndio humfanya binadamu/mtu kuwa na afya na uwezo wa kufanya kazi. Kazi kubwa ya kinga mwilini ni kuukinga mwili na magonjwa na visababishi vyote vinavyoweza kuudhuru mwili. Mtu aliyepungukiwa au kukosa kinga za mwili anakuwa katika hatari kubwa ya kupata/kushambuliwa na kila aina ya ugonjwa, kwa kifupi mtu huyu hata afya yake hudhoofika na kumpunguzia uwezo wa kufanya kazi.

Katika nchi uwepo wa vyama vya upinzani ni sawa na kinga za mwili katika mwili wa binadamu. Vyama hivi vinafanya kazi kubwa sana ya kuilinda nchi dhidi ya virusi na bakteria vya watawala ili kuifanya nchi kuwa salama. Virusi kama rushwa, ufisadi, udikteta n.k haviwezi kuondolewa na chama tawala, lazima pawepo na vyama pinzani imara vitakavyoweza kusimama, kupigania na kukataa kwa dhati mambo hayo.

Leo Tanzania imeshuhudia viongozi mbalimbali wan chi wakijiuzulu, kushtakiwa au kuvuliwa madaraka sababu ya kazi kubwa ya upinzani kuionyesha serikali na chama tawala namna nchi inavyoangamizwa na kuliwa na watu wachache waliopewa dhamana. Mathali tumeshuhudia kazi kubwa ya upinzani ukiibua ufisadi wa Richmond, EPA, Buzwagi, ESCROW n.k kashfa ambazo zimeligarimu sana taifa fedha nyingi.

Binadamu/mtu anafanya kazi akiwa na afya bora na imara, halikadhalika leo tunaona kuna wakati mwingine watawala wanafanya jambo si kwa sababu ya utashi walionao bali ni kwa kuhofia upinzani au kwa ajili ya kupata kura. Hii ina maana kusingekuwa na upinzani watawala wasingefanya.

Mfano kuna maeneo ambayo yanatangazwa uchaguzi, kutokana na nguvu ya upinzani kuweza kushinda watawala hupeleka huduma katika eneo hilo ili waweze kuwashawishi wapiga kura hata kama hakukuwa na bajeti kwa wakati huo. Tumeshuhudia maeneo kadhaa barabara zikitengenezwa wakati wa uchaguzi. Lengo hapa si watu wapate barabara bali ni chama tawala kipate kura. Hii ndio nguvu na umuhimu wa upinzani imara katika nchi.

Wapo watu leo wanaamini Rais Magufuli anafanya vitu ambavyo wapinzani wamekuwa wakivipigia kelele kama vile Rushwa, uwajibikaji wa watumishi wa umma, uonevu kwa watu wa chini n.k. lengo si kujua anafanya au hafanyi bali kitendo cha watu kuhusianisha utendaji wa Magufuli na upinzani ni ushahidi tosha vyama vya upinzani ndio “KINGA YA NCHI” dhidi ya maovu kama zilivyo kinga za mwili mwilini dhidi ya maradhi.

Kuna wakati kila mmoja wetu apate fursa ya kutafakari na kuwaza kwa kina leo hii, hii nchi isingekuwa na vyama vya upinzani ingekuwaje? Je ingekuwa hivi kama ilivyo? Ingekuwa mbaya zaidi ya sasa? Au ingekuwa nzuri zaidi? Wakati ukijiuliza maswali haya, pia jiulize mwili usingekuwa na kinga dhidi ya magonjwa na viatarishi vyote vya kuudhofisha je ungekuwa na afya kama sasa? Nadhani jibu la swali hili la pili litasaidia kupata majibu ya maswali ya kwanza yanayohusu uwepo wa nchi bila ya upinzani.

Serikali na chama tawala wanapohatarisha au kudidimiza upinzani ni vema wakajua hawawakomoi tu viongozi wa upinzani bali wafahamu kuwa wanakata tawi la mti walilolikalia wakiwa juu ya mti, ni lazima tu wataanguka na wakiangua ni watakufa au wataumia. Huwezi toboa macho yanayokusaidia kuona wala kukata mikona inayokusaidia shughuli mbali mbali au kukata miguu inayokufanya utembee na kukimbia. Ni lazima serikali na chama tawala wakajua umuhimu na faida za uwepo wa upinzani imara.

Vile vile ni vema serikali na chama tawala ikatambua ili uwe na “KINGA IMARA ZA MWILI” lazima upate lishe na virutubisho vya kuimarisha “KINGA ZA MWILI”. Halikadhalika ili uwe na upinzani imara na wenye tija kwa nchi ni lazima pawepo na mazingira ya siasa safi, sharia na kanuni zinazoruhurusu vyama vya upinzani kutimiza wajibu wao na watawala wanaoheshimu sharia na kanuni za nchi na kuzifuata kwa matendo na si maneno.

Kila mwananchi ni muhimu akaelewa ili nchi iweze kusonga mbele kimaendeleo ni lazima pawepo na watu wanaoweza kuwasimamia, kuwakosoa, kuwashauri na kuwakemea pale wanapokosea watawala ili wafanye yale waliyotumwa na wananchi. Si kila mwananchi anaweza kusimama na kuikosoa au kuielekeza serikali bali vyama vya upinzani vina uwezo huo ambo pia huzaa faida kwa wananchi walio na vyama na wasio na vyama.

Narudia kusema “TAIFA LISILOKUWA NA UPINZANI NI SAWA NA MWILI USIO NA KINGA ZA MWILI”
 
Ondoa shaka mkuu , hakuna mtu yeyote mwenye nyama na mifupa mwenye uwezo wa kuua upinzani nchini Tanzania
 
Watakaosusia ni
CHADEMA
Tanganyika law society cha mwamikazi bi Karume.
 
Kuna wajinga na wapumbafu wachache wanafurahia ujinga huu, ama kwa njaa zao na ushabiki
 
Sio kwa upinzani wa style hii. Kila siku uko na bakuli unakinga ruzuku ambayo mgao wake unasimamiwa na huyo huyo unayempinga.
Halafu unategemea ruzuku hiyo hiyo kumtoa.
 
Sio kwa upinzani wa style hii. Kila siku uko na bakuli unakinga ruzuku ambayo mgao wake unasimamiwa na huyo huyo unayempinga.
Halafu unategemea ruzuku hiyo hiyo kumtoa.
Mtachonga sana lakini Mbowe ndo M/kiti wetu.
 
Cc CHAUMA bado tunashiriki uchaguzi na tutashiriki cha msingi tunaomba support yenu wana chadema
 
Back
Top Bottom