Kukosekana kwa taarifa juu ya kinachojiri HESLB | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukosekana kwa taarifa juu ya kinachojiri HESLB

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mbute na chai, Sep 8, 2012.

 1. Mbute na chai

  Mbute na chai JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ndugu, rafiki, na jamaa Jforums, poleni sana hasa wanafunzi wanaongoja kwa hamu kujua kama wamepata mikopo toka HESLB. Ukimwa wa HESLB ni dharau ambayo taasisi nyingi zenye dhamana za serikali huwa nayo. Ni wazi kuwa mgawanyo wa fedha huitaji umakini, lakini umakini huu pasina taarifa ya hatua zilizofikiwa ni umakini gani? Serikali iliyo wazi, uwazi wake hujidhihirisha kupitia upatikanaji wa taarifa sahihi juu ya kinachojiri katika utendaji kazi wake. Dharau hii imejidhihirisha pale wanafunzi wanapoomba taarifa toka HESLB, kwani ni haki yao, na kupewa majibu ambayo ni ya mtu kujisikia (discretionary), yanayopelekea baadhi ya wanachama wa jf kuweka mada juu ya HESLB zilizowafanya waonekane waongo. Kwasababu hii, bodi ya mikopo elimu ya juu imepewa madaraka ya kupitiliza, hivyo ni wakati sasa serikali ipitie upya madaraka haya na kuweka mda maalum wa wanafunzi kutuma na kupata taarifa ya maombi ya mikopo. Na hii huonesha umaskini wa utumiaji wa elimu tunayoipata kwa manufa yetu na vizazi vijavyo kwani wafanyayo haya ni wasomi tena wenye shahada za uzamivu n.k. Tafadhali bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu toeni taarifa mmefikia wapi kwani baadhi ya vyuo huanza usajili juma lijalo mwezi huu wa tisa.
   
 2. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  tatizo serikali yetu ni kipofu na kiziwi, hawaoni wala kusikia
   
 3. Msherwa

  Msherwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 4, 2012
  Messages: 1,344
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  bora umenisaidia mkuu, coz nami nilidanganywa nikadanganyika na kujikuta nimepost nilichodanganywa. Watanganyika tumechoka kuwa Wadanganyika, HESLB semeni ukweli
   
 4. Geezzle

  Geezzle JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 834
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Wenye mamlaka ya kuona,kuskia na kuwajbka kwa hil,watoto wao hawana KABSA mpango na boom coz kuskul wao n 100% uhakika!kayumbaz kaz 2nayo kwel!hil liserikal bovu lnantia hasira!aaaaaaaargh!
   
 5. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  pole mkuu!! I hope before Wednesday next week mambo yatakua mambo
   
 6. S

  Suma mziwanda kageye JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaan 2meomba loan toka mwez wa5 alaf hao bod mwakajana niliwauliza pale nanenane dom kuhusu mkopo wakaniambia system ndo hua inagawa mkopo,sasa km system nikitendo cha kubonyeza k2 ambacho hakichukui hata wik.sio siri loan bord mna2boa kishenzi.
   
 7. T

  Tango one Member

  #7
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  achen tu wapendwa maana tanzania walikua wanaiongoza kama watu vipofu lakini si watanzania wa sasa tuna macho nauelewa wakutambua haki zetu na sio wakupelekwa tu walipaswa kutoa taarifa walipo fikia sio kukaa kimya nakuacha watu bila kuelewa wamesimama wp haya ni madhaaarau
   
 8. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,964
  Likes Received: 37,513
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa hii bodi ni janga la elimu ya juu.

  kwakweli wanakera sana.

  Wanafikiri hizo pesa ni msaada wanatupa.

  Ovyo kabisa hawa watu.
   
 9. BOFREE

  BOFREE Senior Member

  #9
  Sep 8, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 159
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ivi mbona kila mtu HESLB HESLB HESLB HESLB amjiu kama bodi ya mikopo wanasubiri mpaka TCUwamalize kila kitu, sasa ni jana tu ndio ilikua dedline ya watu kuomba vyuo mi sioni kama HESLB wana tatizo ila tatizo langu lipo TCU
   
Loading...