Mr Sir1
JF-Expert Member
- Sep 23, 2018
- 1,787
- 8,118
Japokuwa serikali kupitia Wizara ya Elimu iliasa juu ya shule kutokukomoa wazazi baada ya likizo hii ya lazima, nyingi ya shule imeenda kinyume kwa kuleta ujanja wa kuongeza lisaa limoja au mawili na baada ya hapo kupandisha ada kwa karibia 50%.
Mfano hai ni shule ya Genius Kings iliyopo Tabata.
Wamekaa wakatunga ujanja ujanja wa masaa kupelekea ada ya sehemu ya muhula iliyokuwa 440,000 kwenda mpaka kuwa 660,000 na hii sio kwa kipindi kimoja tu bali vipindi vyote kati ya June-Aug na Sept-Dec. Wanajaribu kufidia miezi mitatu ya kufungwa shule kwa kuibia wazazi kwa kiini macho cha jedwali la masaa.
Serikali ina haja ya kuingilia kati katika hili laa sivyo wazazi wengi watashindwa kupeleka watoto shule maana wengi wetu ni wahanga wa COVID baada ya shughuli nyingi za uchumi kudorora.