tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 26,021
- 25,425
Kukimbiza mwenge nchi nzima kwa kisingizio cha kufungua miradi ya maendeleo ni suala lililopitwa na wakati. Watetezi wa mbio za mwenge wanadai kuwa mwenge ni kwa ajili ya kuzindulia miradi ya maendeleo! Je, bila mwenge hiyo 'miradi' haiwezi kuzinduka? Hii ni sababu ya kizamani sana na ambayo haina mantiki yoyote katika karne hii. Kabla ya kungangania kukimbiza mwenge ni bora tukatafakari madhara yatokanayo na mbio za mwenge:
Mosi, shughuli ya kukimbiza mwenge husababisha kuenea kwa ukimwi kupitia kwenye mikesha ya mwenge. Angalau kila wilaya unakopita mwenge, wananchi hukesha kwenye mikesha ya mwenge huku wakishindwa kujikita kwenye shughuli za maendeleo. Katika mikesha hii ndipo wananchi hulewa na kufanya ngono zembe ambazo hupelekea kupata maambukizi ya zinaa, pamoja na ugonjwa hatari wa ukimwi.
Pili, wafanyakazi wa umma hupoteza muda wa kufanya kazi za maendeleo kwani mwenge ukipokelewa kwenye wilaya fulani shughuli zote za kimaendeleo husimama na badala yake watumishi wote hujikita ktk maandalizi ya mapokezi na kukimbiza mwenge. Hili ndilo kundi ambalo huathirika zaidi na mbio za mwenge. Mwenge unatarajiwa kupokelewa hapa majuma matatu yajayo. Lakini cha ajabu watu wameacha kufanya kazi kila siku wapo kwenye vikao vya maandalizi ya mwenge. Hivi ni tija kiasi gani itakayopotea kwa kutokufanya kazi kwa majuma matatu kwa kisingizio cha vikao vya maandalizi ya mapokezi ya mwenge huu wa kipuuzi?
Tatu, pamoja na upotevu wa muda wa kazi, watumishi wa umma, hasa walimu, hukatwa sio chini ya Tsh. 20,0000 kutoka kwenye mishahara yao kwa lazima kwa ajili ya kuchangia mafuta ya mwenge na viburudisho kwa wakimbiza mwenge. Hii huwatia hasara walimu na kuzidi kuwakandamiza kiuchumi, pamoja na kwamba mishahara yao ni duni sana.
Na nne, mwenge husababisha utoro kwa wanafunzi hivyo kuwarudisha nyuma kielimu na kusababisha matokeo mabaya kwenye mitihani yao. Mwenge ukifika kwenye wilaya, wanafunzi hutolewa madarasani na kuamrishwa kusimama barabarani kuushangilia mwenge; na ikiwa kuna mwalimu mkuu atakayeshindwa kuwatoa wanafunzi darasani, hufutwa kazi au kushushwa cheo. Aidha, wanafunzi husimamishwa masomo kwa muda wa takribani wiki nzima wakitunga na kujifunza nyimbo za kuusifia mwenge siku ya mapokezi na mkesha. Kibaya zaidi, wanafunzi, wengi wao wakiwa wa kike, hukesheshwa kwenye mikesha ya mwenge wakiimba nyimbo za kuusifu mwenge usiku kucha. Hapa ndipo wanafunzi wengi hupewa mimba zisizotarajiwa na hata kuambukizwa ukimwi.
Kuna haja ya serikali kuangalia upya falsafa ya mwenge hasa kwa kuzingatia madhara yatokanayo na mbio za mwenge ukilinganisha na makusudio yake. Katika karne hii ya dijitali, ni aibu kupoteza muda wa wananchi kwa kuwalazimisha kukimbiza moto kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu.
:yield: