Kuki-magharibisha Kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuki-magharibisha Kiswahili

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Gurta, Oct 26, 2012.

 1. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wanabodi,

  Hebu leo tujadili mwelekeo wa lugha ya Kiswahili na hasa tukiangazia ukuaji wake kwenye msamiati na istilahi. Tunatambua kuwa lugha ya Kiswahili (pamoja na ukopaji na utohoaji ulijitokea katika ukuaji wake) ni lugha ambayo kwa sehemu kubwa imeundwa na lugha ya Kiarabu na lugha nyingine nyingi za Kibantu.

  Tunachokiona siku hizi ni kuhama kwa mwelekeo (paradigm shift), ambako tofauti na hapo kabla ambako kulikuwa na jithada kubwa ya kufanya Kiswahili kiwe cha 'kibantu' zaidi, lakini sasa ukuaji wake umebadili mwelekeo kuelekea kwenye kuwa cha 'kimagharibi' zaidi kwa kutohoa na kukopa kutoka hasa lugha ya Kiingereza katika kutosheleza mahitaji yake ya misamiati na kukuza istilahi yake.

  • Je, ni nini ni sababu kuu ya haya?
  • Na je ni maendeleo chanya katika ukuaji wa lugha hii inayotajwa kuwa lugha ya pamoja ya Afrika?
  • Nini kimetokea (au kinachokwamisha) ukopaji na utohozi kutoka lugha za Kibantu na Kiarabu?
  • Bado tunaweza kujivunia Kiswahili kama lugha ya KiAfrika?
  Karibu kwa mjadala!
   
Loading...