Kukatwa mshahara bila ridhaa ya mtumishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kukatwa mshahara bila ridhaa ya mtumishi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kimali, Nov 3, 2011.

 1. K

  Kimali Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni jambo la kusikitisha jinsi Watanzania, hasa sisi watumishi wa serikali, tunavyoendelea kukandamizwa na baadhi ya viongozi wa serikali walio madarakani lakini tanaogopa kutoa malalamiko adharani na badala yake tunatoa malalamiko kimya kimya kisa tunaogopa kuchukuliwa hatua au kuhusishwa na suala la uvunjivu wa amani.

  Ninasema hivi kwa kuwa mwezi uliyopita Octoba 2011, watumishi wengi wa serikali za mitaa/halmashauri nchini wamekatwa kiasi kikubwa cha fedha toka kwenye mishahara yao, na mimi ni mmoja wao, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba tulipojaribu kumuuliza Mwajiri wetu juu ya kitendo hicho hatukupata majibu ya kuridhisha hadi sasa. Hata chama chetu cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(TALGWU) hawajazungumza chochote kuhusiana na jambo hili.

  Je kwa kuwa jambo hil linahusu mkataba wa mtumishi na mwajiri ninaweza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Mkurugenzi wangu mimi peke yangu bila kuwahusisha watumishi wengine? Make naona watu wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea na hatujui hatima ya makato hayo!!!
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukataji wa fedha za mtumishi bila makubaliano na ushirikishaji ni uvunjifu wa sheria.

  Kiasi "kikubwa" ulichokatwa wewe kinafikia shilingi ngapi?
   
 3. K

  Kimali Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nimekatwa sh. 170,000 kati ya laki 589,000.00 na hivyo kubakiwa na sh. 419,000.00 tu!
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mbona kidogo hizo, pata control sheet utaona kwanini zimekatwa. Kama umelipa kodi na makato mengine yote ya kisheria na bado ukakatwa kiasi hicho inawezekana wamekuwekea makato ya mkopo au mengineyo on top of makato halali kwa bahati mbaya. Ungeweza kutulia na kupata ufafanuzi kabla hata ya kulalamika. Pole sana.
   
Loading...