bidam90
JF-Expert Member
- Aug 28, 2013
- 273
- 203
Ni binti tuliojuana naye kwa muda wa kama miezi minne sasa, tulianza kufahamiana kupitia WhatsApp, tukachat muda mrefu mpaka kufikia kuwa wapenzi, japo tulikuwa mikoa ya mbali.
Tulitumiana picha na videos na kujuliana hali muda wote, basi tu ili tuzidi kuwa karibu japo hatukuwahi kuonana uso kwa uso! Leo ni siku ambayo sitoisahau maishani, mwangu! Nimefunga safari ya kuja kuonana nae, tulikutana na binti muda wa kama masaa mawili hivi, tukatembea na kuzungumza pamoja huku kila mmoja wetu akiwa mchangamfu kwa mwenzake.
Nilimuandalia na zawadi ndogo tu nikampa. Mida ya jioni ilipofika tuliachana na kila mmoja kuelekea nyumbani anakoishi. Nimefika nyumbani, nakuta message ya yule binti kwenye simu yangu ikisema "Samahani, moyo wangu umeshindwa kukupenda, naomba unisamehe".
Ilibidi nimpigie simu muda ule ule kumuuliza kwanini, lakini hakunipa jibu, aliniambiya tu hata yeye hajui moyo tu umekataa. Roho imeniuma sana. Najiuliza mpaka sasa ni nini alichotaka kuona kutoka kwangu, kama ni hali ya maisha nilimuelzea ukweli kitambo, muonekano wangu, ongea yangu vyote anavijua!
Roho inaniuma sana. Nimeshindwa kwakweli kukaa nalo moyoni nikaona nililete huku kwenu kwa ushauri.
Wadau, tatizo itakuwa nini? Au mnanishauri nini juu ya hili? Maana nipo njia panda.