Kukata umeme kwenye taasisi za umma wananchi ndo wanaoumia na si waliozembea kulipa

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
728
Hivi karibuni tumeshuhudia kutekelezwa kwa agizo la mkuu wa nchi la kuwaruhusu TANESCO Kukata huduma za umeme katika taasisi za umma zenye madeni sugu ambapo kule Arusha Jeshi la Polisi na Hospitali za serikali wamekatiwa umeme.

Binafsi naona wanaoumia kutokana na kadhia hii sio wale waliozembea kulipa madeni hayo bali wanaoumia ni wananchi wanaotafuta huduma katika taasisi hizo mfano wagonjwa.

Badala ya kuzikatia umeme serikali ifuatilie wale waliopelekea upotevu wa fedha za kulipia huduma hizo ili wawajibishwe kuliko kufanya wanayoyafanya sasa.
 
Hivi karibuni tumeshuhudia kuyekelezwa kwa agizo la mkuu wa nchi la kuwaruhusu Tanesco Kukata huduma za umeme katika taasisi za umma zenye madeni sugu ambapo kule Arusha Jeshi la Polisi na Hospital I za serikali wamekatiwa umeme.
Binafsi naona wanatumia kutokana na kadhia hii sio wale waliozembea kulipa madeni hayo bali wanatumia ni wananchi wanaotafuta huduma katika taasisi hizo mfano wagonjwa.
Badala ya kuzikatia umeme serikali ifuatilie wale waliopelekea upotevu wa fedha za kulipia huduma hizo ili wawajibishwe kuliko kufanya wanayoyafanya sasa.
Kwa kiasi fulani,naweza kukubaliana na wewe. Kuna kitu kinazungumzwa sana na jamii kuhusu aina na nani awajibishwe. Mfano, tumeona ubaini wa vyeti feki hadi watumishi 300 katika Wilaya moja. Hivi,kwa mtizamo wa kawaida,hakuna Mwajiri aliyehusika katika kuruhusu kwa maslahi binafsi ajira za hawa watu 300? Kwa nini asichukuliwe hatua?
 
Ni maamuzi ya kijinga kabisa kukata Umeme hospitali ya wilaya na kusababisha huduma kama upasuaji kushindikana na wananchi kupoteza maisha kisa DMO fedha za Umeme aliidhinisha kulipa wahudumu posho za safari
 
Hao ndo walipaswa kuwajibishwa lakini naona mzigo huo unawarudia wananchi ambao maskini hawakuhusika kwa lolote
 
Back
Top Bottom