Kukanusha taarifa kuhusu tangazo la ajira serikalini

Gratius d4m9

Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
62
Reaction score
24
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

KUKANUSHA TAARIFA KUHUSU TANGAZO LA AJIRA SERIKALINI

Kuna tangazo ambalo linasambazwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari ‘’Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wote wanapaswa kuzipuuza. Matangazo yote ambayo hutolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni portal.ajira.go.tz.

Kama mnavyofahamu hivi karibuni Serikali ilitoa taarifa ya kusitisha Ajira mpya Serikalini kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa kama ambavyo taarifa ilivyotolewa hapo awali, kwa kuwa zoezi hilo bado halijakamilika tunaomba wananchi wote na wadau wa Sekretarieti ya Ajira waendelee kuvuta subira hadi pale zoezi hilo litakapokamilika na taarifa rasmi itatolewa na Mamlaka husika.

Sekretarieti ya Ajira inapenda kuomba radhi kwa wale wote waliopata usumbufu kutokana na tangazo hilo lenye nia ya kupotosha Umma. Aidha,tunaendelea kuwasisitiza wadau wetu wote kuwa, wanapoona matangazo ya kazi yanayodaiwa kutolewa na Sekretarieti ya Ajira katika baadhi ya mitandao ya kijamii wasiyokuwa na uhakika nayo wajiridhishe kwa kuangalia katika tovuti na portal ya Sekretarieti ya Ajira kabla ya kuyafanyia kazi.

Aidha, Sekretarieti ya Ajira inapenda kutoa taarifa kuwa haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wenye nia ya kuupotosha umma kupitia taarifa zinazosambazwa ambazo hazina ukweli.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Tarehe 30 Septemba, 2016
 
asanteeeeee,nilivyoona namba za mawasiliano ni za mitandao ya binafsi tu nilipata shaka,na email yao ndiyo kabisaaa,ya kitapeli,eheeeeh,na nyie mtuambie sasa mnaanza kuajiri lini sasa manake naona tantalila nyiiingi
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Kuna tangazo ambalo linasambazwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari ‘’Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wote wanapaswa kuzipuuza. Matangazo yote ambayo hutolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni portal.ajira.go.tz.

Kama mnavyofahamu hivi karibuni Serikali ilitoa taarifa ya kusitisha Ajira mpya Serikalini kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa kama ambavyo taarifa ilivyotolewa hapo awali, kwa kuwa zoezi hilo bado halijakamilika tunaomba wananchi wote na wadau wa Sekretarieti ya Ajira waendelee kuvuta subira hadi pale zoezi hilo litakapokamilika na taarifa rasmi itatolewa na Mamlaka husika.

Sekretarieti ya Ajira inapenda kuomba radhi kwa wale wote waliopata usumbufu kutokana na tangazo hilo lenye nia ya kupotosha Umma. Aidha,tunaendelea kuwasisitiza wadau wetu wote kuwa, wanapoona matangazo ya kazi yanayodaiwa kutolewa na Sekretarieti ya Ajira katika baadhi ya mitandao ya kijamii wasiyokuwa na uhakika nayo wajiridhishe kwa kuangalia katika tovuti na portal ya Sekretarieti ya Ajira kabla ya kuyafanyia kazi.

Aidha, Sekretarieti ya Ajira inapenda kutoa taarifa kuwa haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wenye nia ya kuupotosha umma kupitia taarifa zinazosambazwa ambazo hazina ukweli.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Tarehe 30 Septemba, 2016

Chanzo: Public Service Recruitment Secretariat - (PSRS)
 
Poleni ndugu zangu, kumbe ajira bado hazijatoka hazijatoka tu
 
Serikali ingeangalia utaratibu mzuri wa kuendelea na zoezi hili la uhakiki wa wafanyakazi hewa huku wakiendelea na taratibu za kuajiri, mtaani kumekuwa kugumu mno tunaishi bila ya matumaini. Tunaomba serikali yetu sikivu itusikie pia
katika hili.
 
KANUSHA TAARIFA KUHUSU TANGAZO
AJIRA SERIKALINI
eptember 30, 2016
ARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
KUKANUSHA TAARIFA KUHUSU TANGAZO LA AJIRA SERIKALINI
na tangazo ambalo linasambazwa kupitia adhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha bari ‘’ Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya fasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali pitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika mishi wa Umma inawatangazia watanzania nye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi
kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali rikalini.
tibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda wataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla wa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga upotosha Umma, hivyo wananchi wote napaswa kuzipuuza. Matangazo yote ambayo tolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira tika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane enye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira
w.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni rtal.ajira.go.tz.
ma mnavyofahamu hivi karibuni Serikali ilitoa rifa ya kusitisha Ajira mpya Serikalini kwa ajili
zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa kama bavyo taarifa ilivyotolewa hapo awali, kwa wa zoezi hilo bado halijakamilika tunaomba nanchi wote na wadau wa Sekretarieti ya Ajira endelee kuvuta subira hadi pale zoezi hilo kapokamilika na taarifa rasmi itatolewa na mlaka husika.
kretarieti ya Ajira inapenda kuomba radhi kwa le wote waliopata usumbufu kutokana na gazo hilo lenye nia ya kupotosha Umma. ha,tunaendelea kuwasisitiza wadau wetu wote wa, wanapoona matangazo ya kazi nayodaiwa kutolewa na Sekretarieti ya Ajira tika baadhi ya mitandao ya kijamii wasiyokuwa
uhakika nayo wajiridhishe kwa kuangalia katika uti na portal ya Sekretarieti ya Ajira kabla ya yafanyia kazi.
ha, Sekretarieti ya Ajira inapenda kutoa taarifa wa haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria le wote wenye nia ya kuupotosha umma pitia taarifa zinazosambazwa ambazo hazina weli.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Tarehe 30 Septemba, 2016
 
kufa hatufi ila chamoto tutakiona...huu mwaka wetu aisee...tutazisoma Namba zitaisha tutasoma na herufi zote irabu na consonant zitaisha....na Bado tutakisoma kichina na kijapan.....aisee tunalo na tutakoma mwaka huu....
 
Back
Top Bottom