Ndio, tena ufanye haraka.
ukiangalia ligi ya ulaya sebuleni kwako na mke wako unaonekana
huwez angalia mpira na mkeo nyumban, mengine ni sawa lakin c mpira!!!
huwez angalia mpira na mkeo nyumban, mengine ni sawa lakin c mpira!!!
Kama mkeo nae shabiki?
Usikubali kuogopa kumuonyesha mke wako au girlfriend wako unampenda kisa unaogopa washikaji au ndugu watakusema umekaliwa naye.
Ni tabia mbaya sana unakuta mtu mzima eti anajitamba mbele za wanaume eti "mimi bwana mwanamke hawezi niuliza niko wapi" sasa ndugu yangu wewe ndio ulimtongoza mwenyewe tena ulimsumbua hasa msichana wa watu leo hii anakupigia simu anakuuliza uko wapi unaanza kupanic.
Tusifanye vitu ili kuwaridhisha washkaji huko viringeni, tufanye vitu kuwaridhisha wake zetu, imefikia wakati mwanaume usipokaa bar mpaka saa nane au saa saba usiku unaonekana na ukiangalia ligi ya ulaya sebuleni kwako na mke wako unaonekana pia au usipokua na demu wa nje eti wewe sio mjanja.
Huu ni upuuzi tubadilikeni jamani. Ndio sikatai usikae na washikaji lakini usipitilize sasa.
Naona huruma sana unakuta mtu kavaa lipete likubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia.
Tatizo hakuna...tatizo ni kuchochea ugomvi kwa wanaume wenzio kumbe kwako ni mume mtiifu...kwani kuna tatizo mtu akiosha na kupiga deki nyumbani kwake?!!!...mimi napika, nafua nguo...hakuna kazi nayoipenda kama kuogesha watoto wangu!
Tatizo hakuna...tatizo ni kuchochea ugomvi kwa wanaume wenzio kumbe kwako ni mume mtiifu...
ivoo, haya.tinna mrembo.. sasa mwanaume hataki aulizwe yuko wapi na mke wake si kituko hicho. Tena napaaza sauti katikati ya wanaume wenzake. Ni ujinga sana. Sasa asiulizwe yuko wapi kwani yeye ni nani hapa daslam. Mengi mwenyewe anaulizwa na Jaki.
hili tunalifanyaga mamawatoto akitupanda kichwani, nyumbani hakulaliki, gubu!
Naona huruma sana unakuta mtu kavaa lipete likubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia.
Hakikisha umekaa mkao wa kukaliwa
Kwahiyo pesa ikionekana nyumbani ruksa kushinda bar siyo?Ukiona mtu anazo hizo tabia ujue ni wale walio balehe maumbo ila akili zao bado ni za kitoto.
Tena hata hawajui maana ya ndoa, mke wala baba wa familia ni nini! Yaani kwa ujumla hata hawajui kwa nini wako duniani yaani hawa ni watu wanaojaza dunia bila kuwa na impact hata kwa viumbe waliovileta!
Bibi yangu alikuwa anawakemea wajukuu zake wa kiume akiwaambia hata ng'ombe ana thamani! Atakupa maziwa, nyama na mengineyo lakini si nyie mnaoshinda baa nyumbani wala pesa haionekani nyumbani!
siku utapishana na mume mwenzio kwa mlango ohooo!