SERIKALI INAKATAZA NDOA KWA WANAFUNZI WAKATI WANAFUNZI WAKIENDELEA ZA ZINAA NI SAWA NA KUSEMA SERIKALI INAPIGANA NA HAKI TU NA KURUHUSU UCHAFU UENEE
NANI VITA KATI YA HAKI NA BATILI.
KUKAA KIMYA KWA SERIKALI KWENYE ZINAA NI SAWA NA SERIKALI INARUHUSU ZINAA NA KUKATAZA NDOA.
KWENYE RIPOTI YA HIVI KARIBUNI YA UTAFITI WA VISABABISHI NA MADHARA YA NDOA ZA UTOTONI NCHINI Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kuwa anapozindua ripoti hiyo ni dhahiri anapinga kwa vitendo ndoa na mimba za utotoni kwani ni changamoto kwa maendeleo ya Tanzania.
waziri Ummy alisema Na ninanukuu “Tunataka Tanzania kuwa nchi ya viwanda, lakini hatutaweza kuwa na nchi yenye viwanda wakati watoto 36 katika kila watoto 100 nchini wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18 na watoto 27 wa kitanzania wanapata mimba kabla ya umri huo, hili ni tatizo kubwa ambalo athari zake zitaonekana baadae”anasema Waziri Ummy.
Katika kuhakikisha ndoa hizo zinakoma, Waziri Ummy ameanza kutumia marekebisho ya Sheria ya Elimu yaliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo June 2016 ambayo yanakataza mtu yoyote kumuoa mtoto wa shule ya Msingi au Sekondari kwani ni kosa la jinai lenye adhabu ya miaka 30 jela.
Nikirejea Tafiti zilizopita Kwa mgana Katika taarifa za Utafiti kuhusu mimba za utotoni kwa wasichana uliofanywa mwaka 2010 na Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), zinaonyesha mkoani Tabora pekee
Wasichana wa shule 819 walipata mimba kipindi cha mwaka 2006-2009. Na huko Morogoro kati ya
mwaka 2007-2009 wasichana wa shule 331 walipata mimba na kukatisha masomo yao. Bado takwimu toka Kitabu cha Takwimu za Elimu Tanzania (BEST 2005-2009) zinaonesha kuwa watoto wa kike
walioacha shule kuanzia mwaka 2005-2009 kwa sababu ya mimba za utotoni walikuwa 16,991. Na
katika shule za sekondari wasichana walioacha shule kutokana na mimba kwa mwaka 2009 tu walikuwa 49657.
Mfano mwingine tafiti niliyoifanya Mimi kijijini kwangu inaonyesha kuwa licha ya serikali kikataza wanafunzi kuolewa lkn takwimu zinaonyesha kuwa kati ya wasichana wastani wa 45 hadi 60 wanaoanza sekondari kidato cha kwanza ni 1 hadi 5 tu ndio wanaomaliza kudato cha nne. Na hali hii iko sehemu nyingi na hasa Shule zilizoko vijijini.
Ikiwa idadi ya wanafunzi waliopata mimba ni kubwa hivi ingawa hawakuolewa hii inaonyesha kuwa;-
1. Serikali imefanikiwa ktk vita yake ya kukomesha ndoa za utotoni. Lakini jee hadi hapo serikali imefadika na nini kwa wasichana kufukuzwa shule kwakuwa walipata mimba ingawa hawakuolewa?
2. Je jamii kuna faida yoyote tuliyopata kwa kufukuzwa shule wasichana waliopata mimba wakiwa shuleni.
3. Je jamii hatuoni kuwa tumekuwa wakichangia kukiuka haki za wasichana –hasa haki ya kupata elimu. Cha kusikitisha, maamuzi haya ya kuwafukuza shule wasichana yanawasukumia kwenye umasikini wa kudumu watoto wanaozaliwa na wasichana hawa, na hivyo kuendeleza duara la umaskini kwenye familia zao na taifa kwa ujumla.
Hitimisho.
Serikali imeshinda vita moja tu kwa kuingiza jamii kwenye upotofu/batili wa kukataza ndoa badala ya kukataza zinaaa na matokeo yake tatizo la mimba linaendelea kuongezeka.
Serikali pia itambue kuwakatiza masomo watoto wa kike kwa kosa la kupata mimba ni kuwalazimisha watoto kuwa masikini.
Serikali inadhihirisha pia kuwa vita hii inayopigana hayo ni ya mtazamo zaidi na haitokani na tafiti.
Na kwakuwa vita hii ni ya mtazamo serikali lazima ifanye tafiti ya kina na kujibu maswali kama vile ni wanafunzi wangapi wamefariki kwakuwa tu wao ni WANAFUNZI na vifo vyao vilitokana na mimba za mapema na si kwa sababu ya huduma mbovu zilizopo kwenye mahospitali yetu.
Serikali lazima ikiri kuwa kwa muda mrefu ilikuwa ikipigana na vita za kimtazamo ambayo ni dhahiri imeshindwa. Mifumo yetu badala ya kutafuta suluhu za tatizo hili imekuwa ni sehemu ya tatizo.
Ni busara kwa serikali kuchukuwa hatua ya kwanza ambayo ni kulitambua tatizo kwa kina na athari zake, bila kufata mkumbo wa mtazamo wa kufuata imani, mitazamo yetu na hisia zetu huku ukweli dhahiri ukiendelea kufichwa.
Kama tunaamini wanawake nchini Tanzania ni wengi zaidi kwenye jamii zetu na wana
mchango mkubwa sana kwenye maendeleo ya nchi yetu, hatuwezi kukwepa jukumu kubwa tulilonalo
la kuhahakisha watoto wetu wa kike wanaopata mimba wakiwa shuleni wanarejea darasani na
kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Na kama mimba hizo wanazipata pasipo kuolewa ni dhahiri kuwa ni kuruhurusu kuolewa hakuna nadharia na wala hakutokatiza ndoto za kuendelea kusoma ilimradi akishajifungua anarudi shuleni.
Ni kitu kinachowezekana. Nchi kadhaa ulimwenguni zimefanikiwa zikiwemo za majirani zetu
Wakenya, Zambia na Rwanda, ingaw nchi hizo hazijaruhusu ndoa bali hazijatilia mkazo katazo la kufanya zinaa kama hapa nchini kwetu lkn sisi tunaweza kutekeleza sera hii kwa uzuri zaidi maana tayari tuna
fursa ili tuwe mfano kwa nchi nyingine.
Ingawa tafiti nyingi zinasema kuwa moja ya sababu kubwa kwa watoto wa kike kujiingiza kwenye mapenzi mapema ni kutokana na umasikini. Lkn zipo tafiti zilizokosoa sababu hii. Moja ya tafiti hii ikiwa kufanya morogoro na bbc, iliyotaka kufahamu iwapo watoto wa kike wakipewa mahitaji yote muhimu kwao kama hawatoweza kuhisi kufanya mapenzi. Matokeo yake yalionyesha kuwa pamoja na umasikini lakini watoto wanajiingiza kufanya mapenzi kutokana na hisia za kimaumbile. Kwani ingawa wasichana wale walipewa mahitaji yote lkn mwisho wa siku walitamani kuwa na marafiki wa kiume.
Hivyo basi tusipo chukua hatua thabiti kivitendo ni
kuirudisha nyuma nchi yetu kimaendeleo. Maana kama wananchi wengi hawatapata elimu kikamilifu
nchi itakosa wataalamu, wazalishaji kwenye sekta muhimu za uchumi. Ni bora tukwepe gharama za
kukabiliana na ujinga kwa kuwekeza kwenye elimu ya watoto kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu kuolewa na
kuwarudisha shule watoto wetu wanaopata mimba wakiwa shuleni.