Kujivua Gamba na Mustakabali Wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujivua Gamba na Mustakabali Wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Haki Yetu, May 2, 2011.

 1. H

  Haki Yetu Senior Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninaandika maoni haya kwa msaada mkubwa sana wa makala ya "CCM, Kikwete na Mafisadi" iliyoandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema namba 183, la aprili 27. Mwandishi wake amechambua mambo vizuri na ninawaomba wadau wajaribu kuisoma wakiweza. Kwa kuwa CCM ni chama tawala, kuyumba kwake kunafanya nchi kuyumba pia. Falsafa yake ya Kujivua gamba hakika kutaacha madhila kwa chama.

  Mwandishi alitumia mfano wa kibiblia kuonesha ugumu uliopo kwa chama tawala. Wana wa Israel wakati wakitoka utumwani Misri walifika bahari ya Sham, walishindwa kuendelea mbele sababu ya bahari na pia walishindwa kurudi nyuma kwani majeshi ya Misri yalikuwa yanakuja kwa kasi. Wasomaji wa biblia wanajua hatima yao ilikuaje.....! Katika kujivua gamba, hali inaonyesha kuwa Chama kimefika njia panda. Kwenda mbele inaonekana kuwa giza na halikadharika kurudi nyuma nako ni giza. Kwa yeyote mwenye akili ataona kuwa hata suala la kuwaandikia barua hao wanaoonekana kuwa ni magamba imekua ishu nzito.

  Hivi unaweza vipi kuwatenganisha baadhi ya hao watuhumiwa (magamba) na mkulu mwnyewe. Hata kujiuzulu kwa Sekretariet na Kamati kuu kwa dai kuwa vyombo hivyo vimeshindwa kumsaidia Mkulu nacho pia ni kiini macho tu. Kwani ni nani aliyeiteua hiyo Sekretariet? Kama imeshindwa kazi tatizo ni la nani jameni? Unafiki mtupu......!

  Aidha, hao wanaoshikiwa bango kuwa ni magamba hawakutajwa na kupelelezwa na chama chenyewe bali kutuhumiwa kwa uzito na vyama vya Upinzani. Wote tunajua orodha ilikuwa ndefu na mkulu akiwemo. Tusisahau pia kuwa hawa magamba wana ukwasi mkubwa na pia wana mtandao wao ndani na nje ya Chama. Nguvu ya mtandao hata mkulu naye anaifahamu vizuri kwani hadi sasa anakula tamu na chungu yake. Na kipindi hichi cha umaskini na kupanda kwa gharama za maisha utaona hawa magamba wanaweza kufanya nini muda utakapowadia.

  Sasa kwa jinsi hali hiyo ilivyo, tunaona kabisa kuwa hali ilivyo si shwari kabisa. Huwezi kupendekeza nini kifanyike, zaidi ya kusubiri jibu lipatikane kwani TIME WILL TELL
   
Loading...