Kujiunga NHIF ni kiasi gani?

JAMBONIA LTD

JF-Expert Member
Jan 22, 2014
576
263
Habari ndugu!
Nataka kujua gharama za kujiunga na bima ya afya NHIF kama mwanachama binafsi kiwango cha chini ni shilingi ngapi kwa mwaka?
 
unaweza kulipa nusu kwa miezi 6?

unailipa pamoja.. siku moja..

na ukilipa hautibiwi hadi zipite siku 21..
na baada ya hapo unaanza tibiwa.. mwaka wa kwanza haitibu magonjwa makubwa wala vipimo vikubwa...

mwaka wa pili ndio inatibu magonjwa makubwa
 
baada ya malipo huchukua muda gani kupata kadi?
 
Utatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 1.5 milion kwa mkupuo (hakuna instalment), kwa mwaka wa mkwanza hutoweza kufanyiwa operation ya magonjwa makubw kama ya figo, moyo na mengine

Nb; nilipata maelezo haya ofisini kwao arusha kaloleni
 
unailipa pamoja.. siku moja..

na ukilipa hautibiwi hadi zipite siku 21..
na baada ya hapo unaanza tibiwa.. mwaka wa kwanza haitibu magonjwa makubwa wala vipimo vikubwa...

mwaka wa pili ndio inatibu magonjwa makubwa
Sasa huo mwaka wa pili inakuwaje wakati ukilipa milion 1.5 inadumu kwa mwaka mmoja tu?
Au ndo inabidi ulipe 1.5 nyingine?
Naomba kueleweshwa mkuu
 
Sasa huo mwaka wa pili inakuwaje wakati ukilipa milion 1.5 inadumu kwa mwaka mmoja tu?
Au ndo inabidi ulipe 1.5 nyingine?
Naomba kueleweshwa mkuu

1.5m ni kila mwaka..

mf. mwaka 2018 unalipa 1.5m ( hii ya mwaka wa 1 hautaruhusiwa kutibiwa magonjwa makubwa sababu ndio unaanza)
mwaka 2019 unalipa 1.5m ingine hapa una renew na unatibiwa magonjwa makubwa
mwaka 2020 unalipa 1.5m ingine hapa unarenew tena na unatibiwa magonjwa makubwa
mwaka 2021 unalipa 1.5m hapa una renew tena na unatibiwa magonjwa makubwa
 
Back
Top Bottom