Kujisikia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)

KUTAPIKA WAKATI WA UJA UZITO (EMESIS GRAVIDARUM)

Kutapika ni dalili inayojitokeza kwa mama mjamzito hasa kipindi cha awali ingawa tatizo la kutapika au kuhisi kichefuchefu linaweza kutokea katika maradhi mengine mbali mbali tofauti na ujauzito.
Hali ya kutapika kwa mama mjamzito imegawanyika katika makundi mawili.Kwanza ni kichefuchefu na kutapika wakati wa kipindi cha mwanzo cha ujauzito ( Early pregnancy) na pili ni kipindi baada ya hicho cha awali (Late pregnancy).

Morning sickness.
Tatizo hili hujitokeza miezi ya awali ya ujauzito. Mara nyingi haziendelei baada ya wiki ya 12. Mama anakuwa na kichefuchefu na anaweza kutapika hasa wakati wa asubuhi.

Hyperemesis gravidarum
Tatizo hili linaambatana na mama kuishiwa maji mwilini kwa kutema mate,kutapika na kushindwa kula na wakati mwingine hulazwa hospitali,

Kutapika kunakoendelea wakati wa ujauzito (late pregnancy) huwa ni muendelezo wa hali hiyo.Tangu mwanzoni hali ya awali (Early pregnancy) hutokea mimba inapokuwa chini ya miezi minne lakini hii hali ya pili ‘Late pregnancy inatokea mimba inapokuwa zaidi ya miezi minne.Hapa mama huendelea tu kutapika na vilevile inahusiana na dalili za magonjwa mengine kama dalili za awali za kifafa cha mimba.

Yapo magonjwa mengine yanayosababisha kichefuchefu na kutapika ambayo yanaweza kumpata mama mjamzito na asiye mjamzito.

Magonjwa haya ni kama vile minyoo, maambukizi ya njia ya mkojo(Urinary Track infections),magonjwa ya ini(Hepatitis),ugonjwa wa kisukari (pale sukari inapokuwa juu) (Ketoacidosis of Diabetes),mkojo kuingia katika mfumo wa damu(uraemia),ugonjwa wa kidole tumbo (Appendicitis),vidonda vya tumbo (peptic ulcer) kuziba kwa tumbo (Intestnal obstruction) matatizo ya nyonga kifuko cha mayai (Twisted Ovarian cyst) na uvimbe katika kizazi (uterine fibroid).

Inaaminika kutapika kunasababishwa na kuongeza kwa hormoni ya eostrojeni. Baadhi ya akina mama wanaotumia vidonge vya majira hupata dalili kama za mama mjamzito. Pia hormone ya HCG inaweza kusababisha tatizo hili.

Tatizo hili linaweza kutokea katika mimba ya kwanza tu,wengine hutokea ya pili au wengine hutokea mimba zote.

Hali ya kisaikolojia (psychogenic) pia huchangia kuamsha kichefuchefu kwa kutotamani baadhi ya vitu au vyakula au harufu.
Mama akiwa na hali hii hasa vyakula vya wanga hasa nyakati za usiku,asubuhi ataamka na njaa na kichefuchefu na kuanza kutapika na kuchoka

Chakula cha wanga kama wali na ugali ni muhimu kwani vinatia nguvu na joto,vilevile uwepo wa vitamini B za kutosha nao husaidia sana.

Tatizo hili la kichefuchefu na kutapika pia huchangiwa na mzio (Allergies ) mbalimbali na tumbo kutofanya kazi vizuri (Decreased gastric motility).

Ufanye nini
Mara nyingi kichefuchefu cha kawaida hakiitaji tiba yoyote.Hata hivyo kichefuchefu kikali zaidi kinaitaji matibabu ya haraka. Hivyo ni vyema ukiwahi hospitali.

Matibabu
Matibabu hutegemea dalili. Hata hivyo mgonjwa anaweza kuongezea maji na kupewa dawa za kuzuia kichefuchefu pamoja na kutapika.
Pia ni vyema mgonjwa akijitahidi kula hasa vyakula vya jamii ya wanga pale anapopata nafuu. Maji ni muhimu. Tena mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza uwezekano wa upungufu wa maji iwapo hali itajirudia.
 

Attachments

  • kutapika.jpg
    kutapika.jpg
    17 KB · Views: 677
Kuumwa kwa kichwa wakati wa ujauzito




Wanawake wengi hupata tatizo la kuumwa kwa kichwa wakati wa ujauzito. Hili tatizo huweza kutokea wakati wowote wa ujauzito lakini mara nyingi hutokea wakati wa trimester ya kwanza (miezi mitatu ya kwanza) na trimester ya tatu (miezi mitatu ya mwisho) ya ujauzito.





Katika trimester ya kwanza kuumwa kwa kichwa mara nyingi husabababishwa na kuongezeka kwa hormone na damu inayosukumwa mwilini.


Kuumwa kwa kichwa kunaweza kuongezeka zaidi pale mwanamke mjamzito akiwa na stress, kukosekana kwa usingizi, uchovu, mafua, kuwa na low blood sugar(sukari isiyotosha kwenye damu), ukosekanaji wa maji ya kutosha mwilini(dehydration), kwa wale waliozoea kunywa kahawa kuacha kunywa kahawa kunaweza kusababisha kuumwa kwa kichwa.


Kuumwa kwa kichwa wakati wa trimester ya mwisho husababishwa na kuongezeka kwa uzito unaoweka stress kwenye mwili, mwili kutokuwa balanced, pamoja na wanawake wengine kuwa na high blood pressure wakati wa ujauzito(preeclampsia).


Mara nyingi mama mjamzito hashauriwi kunywa dawa zozote zile kwa kipindi hiki kwasababu kuna uwezekano wa dawa kupokelewa na mtoto na kumdhuru kwa namna moja au nyingine. Hii ni sababu maalaamu kujaribu kutumia njia natural kupunguza maumivu yoyote yale mama anayopatwa nayo kwa kipindi hiki.


Jinsi ya kupunguza au kuondoa maumivu ya kichwa wakati wa ujauzito.

Jaribu kutuliza misuli ya uso na kupumzika.


Uwe makini na madawa ya aspirin na jamii za dawa hii, kwa vile dawa yoyote uinywao inaweza kumuaffect mtoto.


Ukisikia maumivu jaribu kunywa maji glass 2 - 3, kwasababu wakati mwingine maumivu husababishwa na kukosa maji ya kutosha mwilini.


Fanya zoezi la kutembea halafu kunywa maji mengi ya kutosha.


Chunguza vyakula unavyokula unaweza ukawa unapata reaction.


Pumzika vya kutosha na kupata mazoezi ya relaxation.


Fanya mazoezi mara kwa mara kama unavyotakiwa kwa mama mjamzito.


Kula chakula chenye afya kwa mama mjamzito.


Unaweza kuweka kitambaa cha moto kwenye eneo la macho, pua na kichwa kama kuuma kwa kichwa kunasababishwa na mafua au weka kitambaa cha baridi kwenye sehemu inayouma kama ni maumivu ya kichwa ya kawaida.


Hakikisha unabalance kiasi cha sukari kwenye damu(blood sugar)yako kwa kula kiasi kidogo cha chakula kila baada ya muda mfupi badala ya kusubiri kwa muda mrefu halafu kula mlo mkubwa.


Ukipata massage ya shingo, mabega na uti wa mgongo itapunguza stress na kupunguza maumivu ya kichwa.


Pumzika kwenye chumba chenye giza halafu jaribu kuvuta pumzi na kuachia ili kuondoa stress mwilini.


Oga maji ya moto au baridi.


Baadhi ya vyakula vinaweza kuchangia kuumwa kwa kichwa. Unaweza kujaribu kuvitoa kwenye diet yako kuona kama vitasababisha kupunguza maumivu ya kichwa.


Hivi vyakula ni pamoja na:



Chocolate
Vinywaji vikali
Mtindi, jibini, sour cream
Karanga
Mikate yenye yeast
Nyama zilizowekwa kemikali ili kuzisaidia kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.(processed milk)


Ongea na daktari kama umejaribu vitu hivi na bado maumivu yapo au yanazidi au kuumwa kwa kichwa kunaambatana na kizungu zungu, kuvimba kwa mwili, maumivu kwenye maeneo ya juu ya tumbo au
kuongezeka kwa uzito ghafla.
 
VYAKULA MUHIMU WAKATI WA UJAUZITO.


Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu sana, kwani lishe hii hutumika kwa mama na mtoto anaendelea kukua tumboni. Kwa kawaida mahitaji ya chakula na virutubisho mwilini mwa mwanamke huongezeka wakati wa ujauzito na kadri ujauzito unavyoendelea kukua, virutubisho hivyo hutumika kujenga mwili wa mama na mtoto. Hivyo maamuzi ya lishe au lishe mama anayopata huathiri pia maendeleo ya mtoto anayekua mwilini mwake. Tutaona vyakula muhimu vya kuzingatia lishe bora wakati wa ujauzito na baadhi ya vitu vya kukwepa.

mjazito akipata mlo wenye mgoga za majaniMlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini;
Nafaka na Vyakula vya Wanga.
Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka mbalimbali(mahindi,mtama,ulezi n.k), viazi, ndizi, mihogo. Ni vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili(whole grains) kama mahindi, ngano na mchele usiokobolewa; cereals n.k.


cerealsNyama, Samaki na Vyakula vya Protini.
Hivi ni muhimu kwenye kuujenga mwili, hasa kipindi cha miwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya mtoto vinajengwa. Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri. Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi, senene, panzi na wanyama wengine ; vyanzo vya protini za mimea kama maharage, soya, njugu, njegere, karanga,korosho n.k . Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo vingine vya protini muhimu.

vaykula vya protini
maziwaVyakula vya Mafuta.
Hutumika kwenye kuupatia mwili nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili. Mara nyingi vyakula kama nyama, karanga, ufuta, alizeti,senene, panzi, samaki na matunnda kama maparachichi huwa na mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza mafuta yenye lehemu(cholesterol) nyingi.
Mboga za Majani na Matunda.
Matunda na mboga za majani ni sehemu muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula. Vitamini husaidia kuimarisha kinga ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili. Madini kama ya chuma, kalsiamu, zinki, madini joto(Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto tumboni mwa mama.


mboga za majaniVitamini B9 (Foliki asidi) na madini ya chuma hutolewa kama virutubisho ziada kliniki wakati wa ujauzito ili kutosheleza mahitaji ya mwili na kuzuia hatari ya upungufu wa damu kutokea.
matundaMaji

Maji ni muhimu kwenye mmenyenyo na unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya lita 2.3 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, soda, au maji yenyewe. Ni vema zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda.

Mfano wa Mpangilio wa Mlo.
Ili kuhakikisha mlo kamili mjamzito anaweza kufuata mfano wa mpangilio wa mlo ufuatao;

Mfano,

  • Mlo wa Asubuhi: A - Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi, B - Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua,Uji C - Karoti D - Mayai, E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya

  • Mlo wa Mchana: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa, B - Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi C - Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya.

  • Mlo wa Usiku: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa, B - Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati C - Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya Soya.

Vitu na Vyakula vya kuepuka/kupunguza


  • Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto. Haishauriwi kutumia pombe kabisa!
  • Uvutaji Sigara
  • Kupunguza unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.
  • Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi amabayo ni mbaya kwa afya.
 
Dah...hii ishu ya kutapika ilinisumbua sn. Natapika hd nakaa na nikienda hosp naambiwa hakuna matibabu. Aisee yaan ht huwa sisahau,miezi 9 yote mwendo wa kutapika ni uleule lkn nilikuwa nikitapika nakuwa poa kbs nafanya shughuli zangu km kawaida.
 
Jinsi ya Kupunguza Maumivu Wakati wa Kujifungua
attachment.php




Nimewahi kusoma habari za mkunga Kim Hildebrand Cardoso kutoka Berkeley, California nchini Marekani kuhusiana na uchungu waupatao wanawake wakati wa kujifungua na vifo vitokanavyo na uzazi. Ingawa sina cheti cha utabibu niliamua kujikita katika uchunguzi ili nijue kwanini akina mama wengi hasa Tanzania hupata matatizo wakati wa kujifungua?

Nilichogundua ni kwamba karibu kila msichana mwenye umri wa kuweza kubeba ujauzito anatambua matatizo ya mimba na maumivu makali wakati wa kujifungua, lakini miongoni mwa wanawake wenye kufahamu huo ni wachache wanaopewa elimu ya kupunguza uchungu wakati wa kujifungua na jinsi ya kudhibiti matatizo ya ujauzito.

Mpango wa hivi karibuni wa watalaamu wa nchini Marekani uliochapishwa na gazeti la The Daily Mail na The Daily Telegraph ulishauri kuongeza nasaha kwa akina mama wajawazito kwa lengo la kuwasaidia kupunguza hofu za uzazi zinazotajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa shinikizo la damu (blood pressure) wakati wa kujifungua na hivyo kuongeza hatari ya mwanamke au mtoto kupoteza maisha.

Kliniki nyingi hapa nchini kwa mujibu wa uchunguzi wangu zimekuwa hodari kuwapatia wajawazito majibu yatokanayo na vipimo na kutojali umuhimu wa nasaha, jambo ambalo huwafanya wakina mama wengi kukosa elimu ya kutosha kuwasaidia. Lakini upande wa pili, wajawazito nao wamekuwa wakishindwa kuwasiliana barabara na wakunga kwa lengo la kujifunza juu ya uzazi salama.

Kitalaamu kujua jambo kunaongeza hofu hasa ujuzi huo ukikosa maelekezo ya ziada kuhusu kinga. Kwa mfano ni hatari zaidi kwa mwanamke kusikia tu kwamba wakati wa kujifungua huwa na maumivu makali bila kuambiwa anawezaje kuyapunguza. Katika hali ya kawaida mwili ulioandaliwa kupokea pigo fulani kwa mfano, hujenga hali ya kinga ambayo husaidia kupunguza maumivu.

Hii ina maana kwamba uchungu wa mwanamke aliyeandaliwa kisaikolojia kukabiliana na maumivu wakati wa kujifungua utatofautiana sana na yule ambaye mwili wake hakuandaliwa kushindana na uchungu huo. (Hakikisha hili kwa kujiandaa kupigwa na pigwa ghafla, kisha upime mshtuko na maumivu yake.)

Wanawake wengi wanaokumbwa na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua kwa mujibu wa uchunguzi uliohusisha majibu ya wakunga katika Hospitali za serikali za jijini Dar es Salaam, Tabora, Kigoma na Mwanza ni wale wa uzazi wa kwanza. Sababu nilizozibaini mimi ni uhaba wa nasaha kama nilivyodokeza.
(Hapa nawaondoa wanaobeba mimba katika umri mdogo.)

Inaelezwa na wataalamu kwamba idadi kubwa ya wanawake wa kundi hilo wamekuwa wakipata aidha kifafa za uzazi au kushindwa kujifungua na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji ili kuwanusuru na kifo. Matatizo yote haya yanatajwa kutokea nyuma ya shinikizo la damu ambalo nimeeleza habari zake hapo juu kwamba huchangiwa kwa kiasi kikubwa na hofu.
Ukiachana na kundi hilo la uzazi wa kwanza, uchunguzi unaonyesha pia akina mama wanaotoka kwenye familia zenye migogoro ya ndoa, waliotelekezwa baada ya kupewa ujauzito na wasiopendwa na jamaa zao wanaongoza kupata matatizo wakati wa kujifungua. Hii inatoa sura kwamba ujauzito unahitaji zaidi faraja kuliko kitu kingine chochote.

Mtaalamu Joanne Lally kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii cha Newcastle na timu yake waliweza kubainisha mambo mengi ya msingi kuhusu uzazi salama, lakini kubwa kabisa ni faida za kumfariji mzazi mtarajiwa kabla ya wakati wa kujifungua. Kasoro kubwa ya wakunga na walezi wengi wanaohudumia wajawazito ni kuwavunja moyo na kutowajali, jambo ambalo huchangia matatizo wakati wa uzazi.

Nakumbuka nilimuuliza dada Husna (si jina lake halisi) aliyejifungua hivi karibuni mtoto aliyekufa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, nini kilimpata wakati anajifungua aliniambia hivi: Nilishikwa na uchungu saa saba mchana, wakati huo mume wangu alikuwa kazini. Majirani wakanikimbiza hospitali ya Mwananyamala. Nilifika nikiwa na maumivu makali ambayo sikuwahi kuyapata, nikawa nalia kuomba msaada wa manesi, lakini hawakunijali kabisa.

“Basi nikawa navumilia, uchungu ulipozidi ndo manesi wakaja, wakawa wananiambia sukuma, sukuma kwa nguvu huku wananitukana, kusema kweli nilizidiwa na uchungu mpaka nikapoteza fahamu nilipozinduka wakaniambia nilijifungua mtoto akiwa amefariki, kusema kweli niliumia sana.” Mwisho wa simulizi ya Husna.

Katika hali ya kawaida Husna na wanawake wengi huenda kujifungua huku wakiwa na historia kwamba kuna uchungu mkali wakati wa kujifungua, lakini ni kwa kiwango gani na wanawezaje kuupunguza? Hili ni swali gumu, na bila shaka ni wanawake wachache sana waliofundishwa elimu hii na kujiandaa kupunguza maumivu wakati wa kujifungu.


Namkumbuka muuguzi Stacey Rees wa Brooklyn, New York, katika mada zake juu ya uzazi salama alisema, kitu cha kwanza kabisa kukusaidia wakati wa kujifungua ni utulivu wa akili yako.
Hapa ina maana kwamba kila mjamzito anatakiwa kutafuta na kupewa utulivu ndani ya akili yake. Njia pekee itakayomsaidia ni kujifunza namna ya kupata majibu ya matatizo na wasiwasi wake juu ya ujauzito na kujifungua.

Inashauriwa kwamba kila mjamzito anatakiwa kutafuta mkunga au mshauri wake, atakayemuelimisha kuhusu mimba, kumfumbulia matatizo yake na kumpa ushauri juu ya mabadiliko ya mwili, maumivu, ikiwemo nasaha. Ni wazi kwamba maneno ya kusikia huwaogopesha wajawazito.
“Kama tumbo linakuuma chini ya kitofu inawezekana ukawa na tatizo.” “Unaumia upande gani? Huu, basi mtoto atakuwa amekaa vibaya tumboni.” “Amefariki wakati anajifungua.”
Hizi ni kauli mbaya kwa mjamzito kuzisikia inabidi aondolewe kwa kuambiwa maneno kama haya: “Usiogope, kama maumivu yanatokea mtoto anageuka tu, hata mimi ilikuwa hivyo wakati wa ujauzito wa x.” Aaah, siyo sana ukijitahidi kusukuma wala hutaumia sana.” Nasaha za aina hizi zinajenga sana imani ya mjamzito na kuongeza ujasiri wa kukabiliana na matatizo.

Katika Jarida la American Baby mtaalamu mmoja iliwahi kuandika faida ya mwanamke mjamzito kufanya mazoezi wakati wa ujauzito yenye lengo la kumuwezesha kuwa na pumzi ya kutosha. Wengi kati ya wanawake hupenda zaidi kula na kuwa wavivu kufanya kazi au mazoezi, jambo ambalo huongeza uzito wa mwili na kuathiri mfumo wa upumuaji. Haishauriwi mjamzito kushinda amelala au kukaa, ni vema akamuona madaktari amshauri kuhusu aina ya mazoezi kulingana na umri wa ujauzito wake. (Onyo mwanamke asifanye mazoezi bila ushauri.)
Lakini pia muuguzi Ina May Gaskin, anasema katika maneno yake kwamba kuamini kwamba ujauzito si tatizo ni njia ya kuujengea mwili uwezo wa kukabiliana na maumivu wakati wa kujifungua.Labda swali ni kwamba wanawake wangapi wanaosaidiwa kujiamini wakati wa ujauzito wao? Kipimo cha tatizo hili kinaweza kuwa ni kigumu lakini ikiwa mjamzito anaishi kwa hofu nyingi zitokanazo na matatizo ya kujifungua ni dhahiri hajiamini.

Njia nyingine ya kupunguza maumivu wakati wa kujifungua inatajwa kuwa ni kupenda mtoto atakayezaliwa. Mapenzi haya ya kupata mtoto anaweza kumsaidia mama mjamzito akavumilia na kuyaona maumivu kuwa si kitu zaidi ya kujifungua. Ushahidi wa hili unapatikana kwa wanawake wanaoamua kutoa mimba baada ya kutopenda kuzaa. Kwao maumivu huwa ni kitu kidogo ukilinganisha na nia yao ya kutoa mimba.

Aidha nilidokeza hapo juu umuhimu wa kufanya mazoezi, lakini ukweli ulio wazi umebainika kuwa wanawake wanaotembea tembea wodini au nje kipindi cha kuelekea kujifungua hupata nafuu ya maumivu, kuliko wanaoketi na kulia. Utafiti uliofanywa hivi karibuni na timu ya wataalamu nchini Marekani ulionyesha wanawake waliotazama picha za wapenzi wao wakati wanaugulia maumivu ya uzazi walitabasamu na kutulia, huku picha za watu waliowachukia zikitajwa kuwaongezea hangaiko.

Jambo kubwa la kukumbuka ni kwamba maumivu na presha ni vitu vinavyokwenda sambamba, hivyo haishauriwi kwa mtu mwenye maumivu kuwa na fikra mbaya, wasiwasi au kuogopeshwa. Nimalizie tu kushauri kwamba mjamzito anatakiwa kuwa karibu na wataalamu wa saikolojia ili kupata msaada wa kukabiliana na hofu ya uzazi ambayo ni hatari zaidi kwa uzazi salama.

Ushauri wa mwisho kama mwanamke anataka kupunguza maumivu wakati wa kujifungua awe hodari kuhudhuria kliniki na aweze kuuliza kila jambo analohisi linamtatizo. Lakini pia ni mwiko wa kitabibu kwa wakunga kuwatia hofu wajawazito kwa kuwaambia maneno ya kukatisha tamaa. Hata kama tatizo lipo mjamzito atiwe moyo wa kwa kuambiwa. “Mtoto amekaa vibaya, lakini ukifanya hivi na vile utajifungua salama tu.”

 

Attachments

  • Kujifunguwa.jpg
    Kujifunguwa.jpg
    32.4 KB · Views: 1,058
Jamani mke wangu ana mimba ya mwezi 1 na wiki 2 lakini hawezi kula chochote, kila anapoona chakula chochote kile anatapika, hawezi kunywa maji na wala kula matunda yeyote. Je nifanyeje?
 
Jamani mke wangu ana mimba ya mwezi 1 na wiki 2 lakini hawezi kula chochote, kila anapoona chakula chochote kile anatapika, hawezi kunywa maji na wala kula matunda yeyote. Je nifanyeje?




Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sitakagi kukumbuka karaha za vichefuchefu! Mimba zangu zote huwa natapikaaaaaaaaaaaa. Ni shidaaaaaaaa!

Me mwenyew nna mimba ya miez miwili ila kichefu chefu balaaaa.
 
Mimi sitaki kushindana wala kubishana kwasababu ndio unavyotaka wewe na mimi sijakuingilia ushauri wako unaotoa wa miti shamba nakupa mfano tu ya kwamba hata vitu vya kawaida sana ambavyo wewe huvitegemi kuwa na madhara vinaweza kuwa na madhara.Kwani vitamin K inatoka kwenye products gani?(mayai,broccoli,cauliflower n.k),Mafuta ya omega 3 yanapatikana wapi ofcoz kwenye samaki wa kawaida kabisa kama vibua.And by the way nani aloanzisha suala la side effect hapa?si ni wewe…Kama wewe una deal na mitishamba sawa hata mimi nadeal nayo lakini iliyopitia GOOD MANUFACTURING PRACTICE(GMP)….na nadeal na dawa za kawaida zinazojulikana sideeffects na zilizopitia GMP ….Everybody happy right!!Na MziziMkavu si lazima kila mtu akubaliane na wewe!

Janamke bishi hili!!
 
Jamani mke wangu ana mimba ya mwezi 1 na wiki 2 lakini hawezi kula chochote, kila anapoona chakula chochote kile anatapika, hawezi kunywa maji na wala kula matunda yeyote. Je nifanyeje?

Mkeo anaendeleaje kaka. Alijifungua mtoto wa kike?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom