Kujisikia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Nusu ya wanawake wote wajawazito hupatwa na tatizo la kujisikia kichefu chefu na kutapika; ni mojawapo ya dalili kuu za ujauzito.

Husababishwa na kuongezeka kwa hormone mwilini, mara nyingi huanza katika wiki ya sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku.

Madaktari wengine huwa wanaamini ya kuwa ni dalili nzuri kwani humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi vizuri.

Kwa wanawake wengine tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito. Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.

Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kinakuja na kuondoka lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari.

Vitu vya kufanya kusaidia au kupunguza tatizo hili

  1. Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha.
  2. Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
  3. Kula mkate wa kukausha(toast au crackers) au matunda yaliyokaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
  4. Kunwya maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
  5. Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.
  6. Pumzika vya kutosha na pata usingizi wa mchana.
  7. Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au ac au nje sehemu zenye upepo. Kwasababu joto huzidisha tatizo hili. Pia usiende sehemu zenye watu wengi.
  8. Ndimu, tangawizi zinasaidia, pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon) kupunguza kichefu chefu.
  9. Kula viazi vya kukausha na chumvi.
  10. Fanya mazoezi.
  11. Usilale baada ya mlo
  12. Usiache kula
  13. Usile au kupika vyakula vyenye pili pili (spicy) au mafuta mengi.
  14. Usinywe kahawa au vinywaji vikali
  15. Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
  16. Fungua madirisha au Tembea nje ili kupata upepo na oxygen ya kutosha.
  17. Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye 8 ounces ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.

ya Apple Cider Vinegar

18. Kunywa chai za Rasberry leaf, Spear mint/ pepper mint, Anise seed, Fennel seed kabla ya kuamka asubuhi.

chai ya raspberry leaf

chai ya anise seed

chai ya fennel seed

Umwone daktari kama:

Unatapika kupita kiasi mpaka unashindwa kubakisha chakula au maji tumboni au kama kutapika kunaambatana na homa au maumivu.Mwanamke, Uzazi na Afya ("Healthy Living"): Afya
 
namshukuru sana mungu mie ishu ya morning sickness sinaga kabisa kwangu ishu ni diabetes gestosis na hii hunipelekea kichwa kuuma ama mwili kuchoka sana. najua sababisho ni hormones ila kama kuna mwanamake yyte humu anatatizo hili basi ni vyema sana akajitahd sana kwenye namna ya ulaji yaani ale vyakula ambavyo si vya wanga kupita kiasi ama vya mafuta. pia ajiahd kwenye mboga mboga kwa wingi na matunda.

pia kufanya mazoez hasa ya kutembea ni muhimu zaid kwake ili kuburn excess calories ila tu kama itakuwa imeambatana na bp basi ni vyema akawa anapumzika huku anakula kidogo kidogo mara kwa mara. pia akumbuke kwasababu ya damu kuwa na sukari mtoto huwa mkubwa zaid so akiwa anaenda klinik aongee na dr wake juu ya njia ya kujifungulia na muda.
 
Asante kwa ushauri
 
Mie mimba niliyokuwa nayo nilikuwa naishiwa na nguvu kweli yaani pumzi mpaka nilikuwa nakaa popote nilipo kupata ahueni. Pia kichefuchefu nilipata kweli kwa vyakula vya mchuzi yaani nyama nyama hizi, sikuzipenda kabisa.

Thanks Dr.MziziMkavu kwa mada nzuri!!
 
Habari zenu wakuu.

Kuna ndugu yangu mjamzito anapata tabu sana, ana mimba ya miez miwili tu,lakini hali chakula na akila anatapika sana. Kitu chochote akiweka mdomoni anatapika, yawe matunda, juice, hali ni hile hile.

Pia siku nzima anajisikia vibaya, anaumwa na mchovu sana, hali hii imempelekea kukonda.

Naombeni msaada wenu.
attachment.php

HALI ya kusikia kichefuchefu na hatimaye kutapika ni tatizo ambalo huwaathiri wanawake kati ya asilimia 50 hadi 80 wanaopata ujauzito duniani kote. Hali hii inaitwa morning sickness, yaani ugonjwa wa asubuhi. Unaitwa hivyo kwa sababu mara nyingi kichefuchefu husumbua zaidi asubuhi ingawa kinaweza kutokea mchana ama muda wowote.

Kichefuchefu kinatoka na nini? Wanawake wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili kwa karne nyingi, lakini chanzo chake hakifahamiki vyema ingawa kumekuwepo na nadharia nyingi ambazo bado zinafanyiwa kazi.

Inadhaniwa kwamba tatizo hili husababishwa na mabadiliko ya kifizikia na kikemikali tumboni; kuongezeka kwa homoni na kuongezeka kwa hali ya mjamzito kusikia harufu mbaya.

Nadharia moja kuhusu chanzo cha tatizo hili ni ile inayoonesha kwamba linatokana na kuongezeka kwa homoni aina ya estrogen na progesterone, humfanya mwanamke kusikia harufu mbaya huku tindikali pia ikiwa imeongezeka tumboni.

Inaaminika pia kwamba hali ya uchovu na hisia nzito ama mawazo mengi ambayo mara nyingi humpata mjamzito, vinachangia pia tatizo hili. Nadharia kuhusu homoni ambazo huwa nyingi zaidi wakati wa ujauzito, ndizo zinazozungumzwa zaidi kusababisha kichefuchefu.

Homoni za Progesterone zina tabia ya kulainisha misuli ya mwili na hii hufanyika ili kupunguza maumivu ya uzazi kwa kusaidia misuli ya tumbo la uzazi kulainika. Vile vile homoni hizi huathiri pia baadhi ya misuli kama vile tumbo na utumbo mwembamba.

Homoni za progesterone hupunguza kasi ya mfumo mzima wa uyeyushaji wa chakula mwilini, hali ambayo husababisha tumbo pia lisifanye kazi ya kutoa uchafu tumboni haraka na hivyo kuongezeka kwa tindikali nyingi.

Nadharia nyingine ambayo pia hukubalika na wasomi ni kwamba tatizo la kichefuchefu husababishwa na kujirundika kwa kitu kiitwacho kwa kitaalamu, human chorionic gonadotopin (hCG) kwenye tumbo. hCG huanza kuzalishwa baada ya mwanamke kunasa mimba na huendelea kuongezeka hadi mimba inapofikisha wiki 12 ambapo kasi ya hCG huanza kupungua.

Kwa wanawake wengi ni kipindi hiki pia ambacho tatizo la kichefuchefu huanza kupungua pia. Kuna nadharia nyingine ambayo pia hutajwa na wajuzi wakisema kuwa kichefu chefu chanzo chake ni kupungua kwa sukari mwilini, hasa katika wiki za awali za ujauzito.

Pia kuna nadharia inayoonesha kwamba wanawake wenye kawaida ya kula vyakula vyenye mafuta mengi huathirika zaidi kulinganisha na wale wanaokula vyakula visivyokuwa na mafuta.

Hata hivyo, tatizo hili la ‘ugonjwa wa asubuhi' si kitu kibaya kwani tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanawake wengi wanaokumbwa na tatizo hili ni mara chache kuwa na matatizo ya mimba kuharibika (miscarriages).

Pia madaktari wengi wanaamini tatizo hili na dalili nzuri kwamba baada ya mwanamke kuzaa, kuta za tumbo la uzazi hujengeka vyema.

Ingawa baada ya wiki 12 tatizo hili mara nyingi huanza kupungua, lakini baadhi ya akina mama huendelea kutapika hadi siku ya kujifungua. Hali hii ikitokea mara nyingi huathiri shughuli za mama za kila siku katika maisha yake pamoja na familia yake. Kutapika kunaweza kuathiri mtoto tumboni?

Si mtoto tu, hata mama yake kama atatapika sana na kuishiwa maji na chakula mwilini, vitu ambavyo ni muhimu kwake na kwa afya ya mtoto. Katika hali kama hiyo mjamzito anaweza kupungua uzito kwa kasi, jambo ambalo halishauriwi.

Tatizo la kutapika mjamzito huchukuliwa kama la kawaida lakini kuna wakati huwa baya zaidi na huitwa kwa kitaalamu hyperemesis gravidarium (HG). Wawanake ambao hukumbwa na tatizo hili mara nyingi ni wachache, yaani kati ya asilimia 0.5 hadi mbili ya wajawazito wote.

Kama HG haitatibiwa inaweza kuhatarisha maisha ya mama na mtoto tumboni. Tatizo hili la HG hutokea pale mjamzito anaposikia kichefu kuliko kawaida na kutapika kunakozidi mipaka. Inaweza kusababisha mjamzito kuishiwa maji, kupungua uzito na kupoteza virutubisho vingi vya mwili.

Mama anapofikia hali hii inabidi amuone daktari haraka kwa uangalizi wa karibu. Dalili za HG ni pamoja na kichefuchefu kinachokithiri, kutapika kunakoendelea (zaidi ya mara 3 au 4 kwa siku), kupungukiwa na maji mwilini na kupungua kwa virutubisho vya mwili kutokana na kupungua kwa maji.

Dalili zingine ni kupunguka uzito ama kushindwa kuongezeka uzito, mapigo ya moyo kuongezeka, ngozi kuonekana kavu na kichwa kuuma, na wakati mwingine mjamzito anaweza kupata hali kama ya kuchanganyikiwa. Ili kujua kama mjamzito kapungukiwa maji la kufanya ni pamoja na kuvuta ngozi yake ambapo hurudi taratibu.

Lingine ni ngozi inaonekana ikiwa kavu, kupungukiwa machozi ama mate, ulimi kukauka, kuchanganyikiwa ama, mawazo mengi ama hasira, kupungukiwa na mkojo (kukaa muda mrefu bila kukojoa ama kukojoa mkojo ‘kiduchu') na mkojo kuwa wa rangi ya ugoro iliyokolea.

Kama mjamzito ana dalili hizo anatakiwa kumuona daktari haraka. Kuna hatua ambazo daktari atazichukua ili kusaidia tatizo lake na inasisitizwa kwamba hali ikifikia hivyo si tatizo la kupuuzia.

Namna ya kukabiliana na kichefuchefu Hatua za awali kwa mjamzito anayesumbuliwa na kichefu chefu ni pamoja na kwamba, kwa vile katika miezi mitatu ya mwanzo hadi minne, pua zake ni rahisi kusikia harufu, inashauriwa akae katika chumba chenye hewa ya kutosha ambacho hakisababishi hakikusanyi harufu kali kama vile mapishi ama sigara. Sambamba na hilo aepuke kukaa sehemu zenye harufu mbaya na inayokera pua.

Pili, aepuke kukaa eneo lenye joto kwa sababu joto linaaminika kuongeza kichefu chefu. Anashauriwa pia apendelee kula vitu vikavu, kama bisi, tambi, kaukau za chips na ikiwezekana afanye hivyo dakika 15 kabla ya kuamka kutoka kitandani asubuhi. Kwa hiyo ahakikishe vyakula vikavu haviko mbali na kitanda chake. Nne, ale chakula kidogo kidogo kila baada ya saa mbili ama tatu.

Tumbo linapobaki wazi kwa muda mrefu linaweza kuongeza hali ya kujisikia kichefuchefu. Ale chakula chenye protini ya kutosha na wanga (siyo mafuta) kwani hivyo vyote viwili husaidia kupigana na hali ya kichefuchefu. Pia chakula kisiwe na harufu kali ama kisiwe kimekaangwa sana. Vyakula chukuchuku vinafaa zaidi.

Tano, anyanyuke taratibu na asilale haraka haraka baada ya kula chakula na pia asiache kula bila sababu na hasa kula kile anachotamani. Katika hali ya kichefuchefu anashauriwa ajaribu kula hata kama si sehemu ya chakula ulichozea kila siku. Lingine ni kunywa maji nusu saa kabla chakula na nusu saa baada ya chakula.

Kwa lugha nyingine, asinywe maji pamoja na chakula. Ahakikishe unakunywa wastani wa glasi nane za maji kwa siku ili kuepuka hali ya kupungukiwa maji mwilini.

Kama harufu inamuudhi wakati wa kupika na yeye ndiye analazimika kupika, ajaribu kupikia sehemu yenye uwazi wa kutosha, madirisha makubwa ama hata nje ya nyumba. Kama inawezekana, atafute mtu mwingine amsaidie kutayarisha chakula.

Ajaribu pia kula chakula kilichopoa badala ya cha moto. Chakula kilichopoa kina harufu kidogo kulinganisha na cha moto. Pia inashauriwa kwamba chakula wakati huu kisiwe na chumvi nyingi. Harufu ya limao ama ndimu iliyokatwa inaweza kusaidia pia kupunguza kichefu chefu.

Anaweza pia kuweka limao kidogo kwenye chai yake au hata maji. Na mwisho mjamzito anayesumbuliwa na kichefuchefu apate muda mwingi wa kupumzika.

Kuongea mambo ya mimba na akina mama wengine wenye kujua tatizo lake kunaweza pia kusaidia hali ya kupunguza mgandamizo/ mawazo mazito kichwani, kwani kama ilivyoelezwa mwanzo, nadharia moja ambayo watu wanahisi kuwa inasababisha kichefuchefu ni hali hiyo ya mawazo mengi.

Vitu au dawa za kusaidia Tangawizi ni zao la asili ambalo mara nyingi linashauriwa katika kutibu kichefuchefu na kutapika kwa mwanamke mjamzito.

Baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa tangawizi inasaidia sana kupunguza kasi ya kichefu chefu kwa wanawake wajawazito. Mgonjwa pia anaweza kutumia kidonge cha Diclectin: Dawa hii muungano wa vitamin B6 na dawa zinazozuia mzio (antihistamine) aina ya doxylamine.

Dawa hizi zimetengenezwa viwandani kwa ajili ya kuzuia kichefu chefu na kutapika. Dawa hizi zimekuwa zikitumiwa zaidi nchini Canada na wanawake wengi wamesema kwamba zinawasaidia.

Hata hivyo, baadhi ya wanawake wamedai kusikia hali ya kizunguzungu wanapotumia aina hii ya dawa. Kadhalika kuna dawa mbalimbali ambazo madaktari wanaweza kumpa mgonjwa ili kusaidia katika tatizo hili.

Kumuona daktari Mbali na kumuona daktari kutokana na kutapika sana hadi kuonesha dalili ya kuishiwa maji ama kupungua uzito, inapaswa kumuona daktari endapo tatizo la kutapika halikomi baada ya kujaribu mambo ambayo tumeyaorodhesha hapo juu.

Pili mjamzito amuone daktari kama anatapika damu ama vitu ambavyo vinafanana na mbegu za kahawa. Mgonjwa akifika hospitali, daktari anaweza kutaka kujua historia ya ugonjwa wake, hususan kuhusu ni mara ngapi kwa siku kichefuchefu hutokea na kama kinakutokea kila siku ama la.

Anaweza kutaka kujua kama mgonjwa amekuwa akisafiri safiri, utaratibu wake wa kila siku kama umevurugwa, kama kuna hali inayomletea mawazo ama kumchanganya akili, aina gani ya chakula ambayo amekuwa akiitumia na kama yeye ama mumewe anavuta sigara. Makala haya yamepatikana kutokana na mtandao wa kompyuta.

Source:Habari Leo

Attachments

  • vomiting during pregnant3.jpeg
    vomiting during pregnant3.jpeg
    6.4 KB · Views: 5,400
MziziMkavu nadhani nilishawahi kusikia ukimsaidia mgonjwa kama huyu!mpe pole mgonjwa hio ni hali ya mpito atakuwa sawa baada ya muda kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni kigumu....kama hali kabisa ni hatari kwa afya ya mtoto anaweza kutumia cyclizin hydrochlorid peroral 50mg x 3 au metochlopramid hydrochlorid 10mg x 3 for 5 days itamsaidia kupunguza kichefuchefu na kutapika ili aweze kula.
ONYO:Metochlopramid hydrochlorid haitumiki kwenye third trimester ya ujauzito au wakati wa kunyonyesha....kwa ushauri zaidi akamuone daktari
 
Last edited by a moderator:

Shukran kwa ushauri mkuu
 
Mkuu gorgeousmimi Mwanamke mwenye mimba au hata asiyekuwa na mimba siwezi kumpa Ushauri

atumie Dawa za kizungu Drug kwa sababu nyingi za Dawa za kizungu zina Madhara

Side Effect mimi huwa ninaziita Dawa zakizungu ni dawazenye sumu ndani yake. Nitampa Ushauri wangu

Mwanamke mwenye Mimba ambaye anasikia Kichefu chefu au kutapika bora

atumie Tangawizi kuliko kutumia dawa za kizungu zenye Madhara ndani yake drug Side Effect

hebu tembelea bonyeza hapa source. Drug Side Effects | Drugs.com

Top 20 Side Effect Searches.

Angalia Faida ya kutumia Tangawizi kama dawa:

FAIDA ZA TANGAWIZI

Tangawizi ina faida nyingi sana kwa mwili wa mwanadamu. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo :

1. Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni,.

2. Kutibu tatizo la gesi tumboni

3. Kuondoa tatizo la msokoto wa tumbo (bila kuharisha)

4. Husaidia kuzuia kutapika.

5. Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli),

6. Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.

JAM YA TANGAWIZI.
Unaweza kutumia Jam ya Tangawizi kujitibu magonjwa mbalimbali kama ilivyo onyeshwa hapo juu.

JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA TANGAWIZI.

Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.

MUONGOZO WA KUJITIBU MAGONJWA MBALIMBALI KWA KUTUMIA TANGAWIZI.

Unaweza kujitibu magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao la Tangawizi kwa kufuata maelekezo yafuatayo :

KUJITIBU TATIZO LA KUVIMBIWA NA KUKOSA HAMU YA KULA.

Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa.

Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.

Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe.

Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza

hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.

KUJITIBU TATIZO LA MAUMIVU YA KUKOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.

KUJITIBU TATIZO LA KUHARISHA.
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.

MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASI

Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.

MAUMIVU MAKALI YA TUMBO

Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.

BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.

KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA

Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu

Unaweza pia kunitembelea Blog yangu kwa kubonyeza hapa.
FAIDA ZA KUTUMIA JUICE YA TANGAWIZI AU CHAI YA TANGAWIZI
 
Hakuna dawa isiokuwa na side effects MziziMkavu!
 
Last edited by a moderator:
Hakuna dawa isiokuwa na side effects MziziMkavu!
Niambie Dawa zangu hiz ninazotumia side Effect zake Dawa ya kwanza (1) ninatumia na Maji ya kunywa Dawa yangu ya Pili nia (2) Asali Dawa yangu ya (3) ni Tangawizi Dawa yangu ya (4) ni Kitunguu Maji Dawa yangu ya (5) ni kituınguu Saumu Dawa yangu (6) ni Manjano. Haya nimekupa dawa zangu hizo 6 Nitajia Side Efffect zake Madhara yake nitajie Kwa Binadamu? Bibie gorgeousmimi
 
Dr MziziMkavu mimi sitaki kubishana na wewe hata hizo dawa unazozitaja wewe zina madhara tena mengi tu,na mbaya zaidi nyingi hazijafanyiwa utafiti ili kujulikana side effects zake na interactions na madawa mengine na vyakula.Unajua mmea kama LOCUST HERB au mafuta ya kawaida ya samaki yenye OMEGA 3,pamoja na vyakula vyenye VITAMIN K vinaweza kumpa mtu interaction na mervan/warfarin na hata kuhatarisha uhai wa mhusika?
Nice day
 
Dr MziziMkavu mimi sitaki kubishana na wewe hata hizo dawa unazozitaja wewe zina madhara tena mengi tu,na mbaya zaidi nyingi hazijafanyiwa utafiti ili kujulikana side effects zake na interactions na madawa mengine na vyakula.Unajua dawa kama Johannessurt au mafuta ya kawaida ya samaki yenye OMEGA 3,pamoja na vyakula vyenye vitamin K vinaweza kumpa mtu interaction na mervan/warfarin na hata kuhatarisha uhai wa mhusika?
Nice day
Bibie gorgeousmimi Jina lako tu kwangu tosha kuwa wewe unabisha na kuniletea (Johannessurt au mafuta ya kawaida ya samaki yenye OMEGA 3,pamoja na vyakula vyenye vitamin K) Wapi na wapi na nilivyokuuliza mimi dawa zangu za Mitishamba ? Hebu nipe Side effect ya kutumia Maji ya kunywa ?Au Side effect ya kutumia Asali Safi ya nyuki? Dawa mbili tu nipe Madhara yake kwa kutumia Binadamu? ukinipa mimi sitoweza tena kuwapa hapa ushauri watu kutumia dawa zangu leo ndio itakuwa mwanzo na mwisho sitoweza tena kuwapa watu ushauri wangu watu kutumia dawa za Mitishamba nitakuwa nina chungulia JF Doctor na kuondoka zangu.
 
Bibie gorgeousmimi Jina lako tu kwangu tosha kuwa wewe unabisha na kuniletea ( Johannessurt au mafuta ya kawaida ya samaki yenye OMEGA 3,pamoja na vyakula vyenye vitamin K ) Wapi na wapi na nilivyokuuliza mimi dawa zangu za Mitishamba ? Hebu nipe Side effect ya kutumia Maji ya kunywa ?Au Side effect ya kutumia Asali? Dawa mbili tu nipe Madhara yake kwa kutumia kwa bindamu ? ukinipa mimi sitoweza tena kuwapa hapa ushauri watu kutumia dawa zangu leo ndio itakuwa mwanzo na mwisho sitoweza tena kuwapa watu ushauri wangu nitakuwa nina chungulia JF Doctor na kuondoka zangu.
Mimi sitaki kushindana wala kubishana kwasababu ndio unavyotaka wewe na mimi sijakuingilia ushauri wako unaotoa wa miti shamba nakupa mfano tu ya kwamba hata vitu vya kawaida sana ambavyo wewe huvitegemi kuwa na madhara vinaweza kuwa na madhara.Kwani vitamin K inatoka kwenye products gani?(mayai,broccoli,cauliflower n.k),Mafuta ya omega 3 yanapatikana wapi ofcoz kwenye samaki wa kawaida kabisa kama vibua.And by the way nani aloanzisha suala la side effect hapa?si ni wewe…Kama wewe una deal na mitishamba sawa hata mimi nadeal nayo lakini iliyopitia GOOD MANUFACTURING PRACTICE(GMP)….na nadeal na dawa za kawaida zinazojulikana sideeffects na zilizopitia GMP ….Everybody happy right!!Na MziziMkavu si lazima kila mtu akubaliane na wewe!
 
Asante nimekuelewa Dada yangu sawa tu hakuna tabu gorgeousmimi
 
Last edited by a moderator:
Nina ujauzito wa miezi minne ila nina tatizo la kutema mate hadi nahisi kero...naombeni msaada wa kumaliza hili tatizo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom