Hawa Bodi ya Mikopo kama wanasoma huku tafadhali rekebisheni system yenu, inasumbua sana, na number ya simu mliyoweka haipatikani.
Aactually mmeweka number moja tuu ambayo ni +255 22 550 7910, hiyo number inapigwa na Tanzania nzima haipatikani kabisa, tukija ofisini kwenu, mlinzi anakwambia tumeambiwa tuwaambie mjaribu kupiga mara nyingi mpaka ipatikane, (kumbuka siku zinaisha maana deadline yenu ni tarehe 30)
Ukikutana na mlinzi kashiba vizuri na ana raha siku hiyo anakuruhusu uende reception, kimbembe ndio kinaanzia hapo reception sasa. Pale reception wanajibu majibu ya hovyo sana, tena hata hakuangalii usoni, wakati anakujibu anasoma gazeti na hawana msaada kabisa na watu zaidi ya wao kusoma gazeti, unauliza kitu kama mbona nimelipia lakini kila nikitaka kuingia kujaza form inakataaa? husaidiwi unajibiwa utumbo na mtu anaendelea kusoma gazeti.
Kuna kaka pale na dada wa kiarabu, ni shidaaa, afadhali huyo kaka anakujibu angalau vizuri japo hawana msaada, huyo dada wa kiarabu anajibu utumbo mmoja tuu anakuwa hana habari tena na wewe na akiona unamuuliza sana hakujibu chochote anaendelea kusoma gazeti. Hii ni mbaya sana. Watu wengi wanalalamika, maana watu wametoka mbali wanapoteza nauli zao kuja mpaka kwenu halafu mnashindwa kuwasaidia.
Eti majibu yenu ni nyie hamna uwezo wa kuwasaidia zaidi ya kuendelea kupiga simu, sasa apige vipi simu wakati simu yenyewe haipatikani na hata ikipatikana haipokelewi. Kwa kweli mnatunyanyasa sana wanafunzi!
Basi ingekuwa afadhali mchukue hayo malalamishi myapeleke kwa wausika wakati mwanafunzi anasubiri jibu, hamfanyi hivyo nyie mnajibu ndio tulivyoambiwa tuwajibu hivyo, na hamruhusiwi kuonana na wafanyakazi face to face, ni kitu gani hichi jamani?? Kama mnasoma hapa tunaomba mjirekebishe please!!:A S cry: