Kujifananisha na mwingine

Kujifananisha na mwingine

habari ya hapa

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
12,788
Reaction score
8,755
Kuna tabia ambayo huwatesa watu, hata mie ilishawahi kunisumbua sana, kitabia chenyewe nikujifananisha na watu wengine. Mfano; Mwenzi wako ana ukaribu na mtu fulani, wewe badala ya kushughulikia tatizo ili amani ichukue mkondo wake, waanza kumtazama huyo mtu halafu wajifananisha naye. Pengine ukampima na kujifananisha kutokana na muonekano wako ukilinganisha na yeye, pia waweza kuweka kigezo cha fedha, nakujiuliza kama anakuzidi ama unamzidi. Kwa kutizama sura, mavazi na kadhalika, vyaweza kukutesa akili. tabia hii si nzuri cha msingi wekeza upendo na mambo yatakaa sawa. Huwezi kujifananisha na mtu mwingine, vilevile kwa mwenzi wako, haipendezi pia haitakiwi kumlinganisha na yeyote yule. Kila mmoja yupo tofauti kwa sababu kadhaa. Pamoja na ukweli kwamba suala la kumtazama mtu na kumuona anakuzidi linaweza kukupa unyonge lakini kuna kaujinga kakupindukia (ambacho wengi wetu tunacho).

Watu wengi husumbuliwa na mawazo kuwa wenzi wao wanaweza kuwaacha na kwenda kuanzisha uhusiano na wengine wenye ubora kuliko wao. Kama mpenzi wako aliwahi kuvutiwa na mtu mwingine kabla yako, huwezi jua, muhimu ni kuzingatia kile ambacho amevutika kwako. Zingatia kuwa endapo mwenzi wako angekuwa amedata kwa mtu mwingine tofauti na wewe, huwezi jua lakini ukweli ni kwamba msingekuwa na uhusiano wa kimapenzi mlionao leo. Achana na mawazo yasiyojenga, amini kuwa mwenzako amedata kwako ndiyo maana leo mpo pamoja. Jenga utaratibu mzuri wa kuheshimu jinsi mwenzako alivyo. Kadhalika jiamini kwamba duniani hakuna mtu bora kama wewe, kwa hiyo usiishi kwa kumuogopa mtu kutokana na fedha zake ama sifa nyingine yoyote. Dunia imeumbwa na vitu tofauti, hivyo na watu wametofautiana!!!
 
Back
Top Bottom