Kujichubua sio urembo wala sio uzuri!

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,641
6,694
Ni nani huwadanganya enyi wanawake yakwamba eti kujichubua ndio unakuawa mrembo na mwenye mvuto?

Kiukweli ewe unayechubua ukikutana na mwalimu wa sanaa yaani nipishe na upite mbali kabisa

Nikupeni siri moja, sie vidume ndio tunapenda ngozi nyeupe ila sio iliyojichubua!
Ni nini kinakufanya ujichubue?
Au ndio umbumbumbu wa kutoelewa athari zitokanazo na crim za kujichubua?
Lakini mbona wasomi na wanaojielewa hujichubua, ivi nini kinawakuta hata mshindwe kujikubali na kujiamini?

Madhara yake ni makubwa,
Mtu anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)

Na mengine mengi kama kukataliwa na kubaguliwa na wanaume tunaojielewa!
 
yaan nikikuta mwanamke kajichubua ananikera mpk nataman kumuuliza mbona unajiharibu una tatizo gan maan sipend kama nini yaan
 
Ni interest ya mtu binafsi kujichubua na sio urembo wala uzuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom