kujiajiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kujiajiri

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by banga, Jan 31, 2012.

 1. b

  banga Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hallow great thinkers.
  natamani kuanza biashara ya kilimo cha matunda na ufugaji wa kuku chotara. naomba yeyote mwenye relevant information juu ya hili aniitaarifu kupitia beatricezuberi@yahoo.com.
  asanteni.
   
 2. snochet

  snochet JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 1,271
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  sio safe sana kutoa e-mail yako huku JF beatrice,pitia post za humu ndani ya forum hii utafute post yangu kuhusu kuku mmoja akuzalishie sh milioni moja..naamini itakusaidia
   
 3. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hata mimi hivi karibuni nimepost thread ya kuomba ushauri wa kuanzisha biashara ya kilimo, kwa vile tuna nia moja basi mimi na wewe tunaweza kuwa wajisirimali wa kuchangiana mikakati na michakato
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  HONGERA SANA KWA KUTAKA KUJIAJIRI MKUU

  MIMI NAKUSHAURI UFANYE YAFUATAYO
  1. KWENYE KILIMO CHA MATUNDA
  - Hakikisha matunda unayo lima unafanya packeging mwenyewe ndo uuze
  - Usilime then ukasubiria madalali wakutafutie soko kwa bei yao
  - Unaweza fanya simple packeging na ukawa unauza hapo utakuwa umeyaongezea sana thamani matunda yako na mtaji ukikuwa unaweza hata nunua yale magari ya kubebea vitu vya baridi kama samaki ukawa unabebea matunda yako yaliyo pakiwa na kuuza hata mwanza kama wewe uko dar
  [​IMG]

  ukipaki dizaini hiyo hakika utakuwa unafanya biashara iliyo enda shule, na utajitofautisha na wenzako

  [​IMG]
  Au dizaini hii,

  2. Kuhusu kuku
  Hta kwenye kuku jitahidi sana kufuga na ku process mwenyewe, unaweza anza kidogo kidogo, haya maswala ya kufuga tu na kusubiri wateja waje kununua ni ngumu sana

  - Razima ujitofautishe na wenzako, ni kwa kivipi wateja watakuja kununu kuku wako na wasununue za wenzako? kuna kitu gani cha ziada kwenye kuku wako?
   
Loading...