kujenga karibu na nguzo kuu za umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kujenga karibu na nguzo kuu za umeme

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kede, Jun 28, 2012.

 1. K

  Kede Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 31
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  jamani naomba msaada,sheria ya ujenzi karibu na nguzo kuu za umeme inasemaje?
   
 2. s

  straity Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unapozungumzia kujenga karibu na nguzo kubwa za umeme inamaanisha umejenga kwenye Right of Way (RoW) ya eneo la TANESCO, haya maeneo yana ukubwa tofauti kulingana na umeme unaopita hapo, i.e kuna umeme wa Kilovoti 11 ambao unahitaji Way Leave ya Metre 3 X 3 yani kila upande uache mita 3, umeme wa kilovoti 33 inatakiwa mita 5 kila upande, na kilovoti 66 inatakiwa njia ya mita 15 kila pande na kilovoti 132 njia yake ni mita 20 kila pande yani kushoto na kulia, na Kilovoti 220 njia ni mita 30 kila upande wakati kuna line mpya ambazo tanzania ndio tunataka kuzianzisha za kilovoti 400 ambazo njia yake ni mita 45 kila upande.Sasa kisheria TANESCO huwa hawana sheria (legal aspect) ya kumiliki haya maeneo ingawaje huwa ni yao kwa kununua kutoka kwa wananchi pale wanapotaka kupitisha line zao za umeme, yani ni lazima walipe compensation (fidia) kwa wamiliki wa mwanzo ndio waweze kujenga katika maeneo hayo. Lakini ieleweke kwamba nao wanamiliki bila sheria yoyote kwahiyo wakitaka kukubomolea kama utakuwa umejenga kwenye eneo hilo wanachofanya wanaomba Eviction Order kutoka either manispaa au City kulingana na eneo lilipo.Hii ni tofauti na Tanroads ambao wao wanamiliki kisheria kabisa maeneo yao ya Road Reserve.
   
Loading...